Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Matajiri wapi hao wa kuwatoa kimaisha maskini? Hawa wahindi, wachina na warabu?Tajiri anaelipa ujira wa buku 6 kwa masaa 12 ndio atakaemtoa mtu katika umaskini?Nyie ndiyo Magufuli alikuwa anawaita '"WANYONGE" na mkakubali kuwa Magufuli ni Rais wa wanyonge.
Ni upumnavu kukubali kuitwa MNYONGE. Mungu alituumba binadamu na akatuwezesha kwa kutupatia ubongo. Ukitumia ubongo wako vizuri unaweza ukajinasua kimaisha.
Magufuli alikuwa añatamba kuwa ana uwezo wankumfanya tajiri aishi ka shetani. Kwangu hii haikuwa sawa. Alipaswa aseme ana uwezo wa kumfanya maskini aishi kama tajiri ndiyo ange make sense.
Muacheni Samia atuongezee matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hawa wakiongezeka ndiyo watawaajiri maskini na maskini wanaweza kutoka kimaisha kupitia matajiri. Kamwe umaskini na unyonge siyo kitu cha kujivunia
You are completely doomed kama unafikiri hao matajiri wa bongo wana msaada na masikini zaidi ya kuwanyonya na kuwa paralyse kiuchumi. Zaidi ya kunyanyasa wabongo impact ya hao matajiri ni ndogo sana kwenye mafanikio ya mtu mweusi.