PreGE2025 Samia Squad yaanzishwa, lengo kuu ni kumsifu Rais Samia ili kujipatia hela za kujikimu

PreGE2025 Samia Squad yaanzishwa, lengo kuu ni kumsifu Rais Samia ili kujipatia hela za kujikimu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Squad hiyo imekusanya Wanamuziki kadhaa wakiwemo na wale waliochoka kama Mwinjuma Muumini, lengo ni kutunga nyimbo za kusifu na kuabudu kwa nia ya kupata hela za kulisha familia.

Taarifa kamili hii hapa

View attachment 3326364View attachment 3326365

Ujumbe: Ukiwa Mwanaccm halafu huna hela basi wewe utakuwa fala sana.
Tatizo la afya ya akili ni kubwa nchini ipo haja zinunuliwe machine maalumu kwa ajili ya kuchambua akili za wanaoingia Dar na Dodoma
 
Squad hiyo imekusanya Wanamuziki kadhaa wakiwemo na wale waliochoka kama Mwinjuma Muumini, lengo ni kutunga nyimbo za kusifu na kuabudu kwa nia ya kupata hela za kulisha familia.

Taarifa kamili hii hapa

View attachment 3326364View attachment 3326365

Ujumbe: Ukiwa Mwanaccm halafu huna hela basi wewe utakuwa fala sana.
Hii ya kuanzisha vitu kwa majina ya viongozi haiko sawa....
 
Hawa ni aged 45-50+ 😂 nchi imeozaa KABISA .
 
Kuna haja sasa ya watu wenye uelewa na maarifa kuingia kwenye active politics kuliokoa hili Taifa na huu ujinga.

Kukaa pembeni na kuona siasa hazituhusu ndio kunatokea shida kama hizi sasa.
Maalim comments yako imeniliza sana nimelia mnooo mbona umeandika ukweli mgumu hivi , ngoja nilie tena
 
Maalim comments yako imeniliza sana nimelia mnooo mbona umeandika ukweli mgumu hivi , ngoja nilie tena

Inasikitisha sana mkuu, duniani kwingineko watu wenye nyadhifa kwenye utumishi wa umma wanafikiria future ya Mataifa yao na vizazi vyao.
Watu wako serious na future za mataifa yao, watu wanandoto ya future ya watu wao namna inapaswa kuwa.

Huku tunawaza maisha binafsi na familia zetu ilihali umepewa dhamana ya kutumikia umma, na sio kuzifanya ofisi za umma kama biashara binafsi.

Watu wenye uelewa kukaa pembeni na kuona siasa aziwahusu madhara yake ni kuruhusu mfumo na mifumo kutekwa na wajinga wanaowaza leo yao na sio Kesho ya Taifa na vizazi vijavyo.

Leo hii kuna shida ya ajira kwa vijana wahitimu lakini ukimuuliza Waziri au yeyote mwenye husika juu ya mpango madhubuti ya Kesho kumaliza au kupunguza tatizo utakutana na blah blah.

Ni wakati wa Watanzania wote kuamka na kuona umuhimu wa kuwa serious na masuala muhimu ya Taifa hili Kwa manufaa ya wengi (Watanzania) sio kakikundi cha watu wachache waliouteka mfumo.
 
Hata Wageni ruksa

Screenshot_2025-05-08-14-16-17-1.png
 
Back
Top Bottom