Samia Suluhu Hassan Hili la Humphrey Polepole Halitapita hivihivi

Kipindi kile yupo kwenye system alikua ana enjoy tu kaja kuuona uzalendo baada ya mambo kwenda mrama bongo kikubwa uzma tu hata leo hii ikitokea samia kikwete akatekwa watu watasema free kikwete
Kikubwa uzima wakati huo uzima unategemea siasa na viongozi? Uongozi mbovu unaua maelfu ya wananchi kila siku ila kwa mtu asiyejua kufikiri nje ya box ataona mambo yako sawa tu.
 
Amina. sio kwa huyo tu. Awarudishe wote waliopotea katika kung'ang'ania kwake madaraka. Bila kuwasahau wale wa 29 Oktoba 2025, vile vifo vya vijana wetu.

Sio huyo tu wapo wengi waliopotea na kuuwawa
Ukweli damu za wafu hao zitamlilia milele

Walipotea na kuuwa wakiacha wazazi, ndugu, marafiki, familia zikiwahitaji na kuwategemea
Huzuni na simanzi zao hazitofutika katika mioyo na akili zao, ni maumivu makubwa

Na bado vitendo hivyo vinafanyika pasipo kujua nani atafuata na mwisho wake lini
 
Ukweli kwao ni mwiko yaani kiongozi wao kila analotenda lipo sahii hakuna wakupinga
 
Haki ya Mungu tena nakwambia hili halitapita hivi hivi. Ni either umtafute na arudi akiwa hai au ulipe gharama ya uhai wake.
Hilo ni moja tu.Yapo mengi zaidi.Kwa muda huu alivyojitawaza kuwa rais hawezi kukuelewa.Tumuombe Mungu ampe uhai ili mwaka 2031 tum-zoom atakavyokuwa anajibebabeba kwa huruma.
 
Itakuwa kuna mission kapewa sehemu maana ccm kwa vimichezo hawajambo
 
Limepita la Kolimba, Kigoma Malima, Ali Juma, Magufuli na wengine wengi tu
Huyo slowslow aliekula nao na kuinjoi viete zao, hana umuhimu wowote alipata alichostahili.
Weka akiba ya maneno,
Vizazi vyako visije pata tabu ya kujua laana ilitokea wapi.
 
Ingawa hakustahili kupatwa na yaliyompata ila ukweli ni kwamba Humphrey Polepole amevuna alichokipanda, watu kama akina Ben Saanane, Mdude tusiwaweke kundi moja na Polepole. Hii kitu inanikera sana watu wanachanganya mafaili kwenye hili suala.... Nisiwe mnafki binafsi Polepole namuhurumia lakini sio sana, nguvu yangu ya maombi na huruma naitumia kwa watu kama Chaula, Tundu Lissu, Mdude, Ben Saanane.
 
Polepole Mungu amsaidie ila dunia duara kipindi wanapotea akina Ben saanane chini ya his former boss ambae nae ni marehemu hakuwahi kuwaongelea baada ya Magu kufa ndio anakumbuka uzalendo.Utawala wa Magu ulikuwa utawala wa kidikteta sema watanzania wakafumbia macho sababu alidili na mafisadi yanayotokea sasa ni matunda ya utawala wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…