GE2025 Samia Suluhu Hassan ni Mgombea Halali Kikatiba na kihistoria

GE2025 Samia Suluhu Hassan ni Mgombea Halali Kikatiba na kihistoria

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mwaka 1995 na 2000: Benjamin Mkapa alipata uteuzi wa pili bila upinzani mkubwa ndani ya chama.
Kukwepa swali la msingi la fomu ilichukuliwa unafifisha nguvu ya hoja yako ambayo ninataka kuiunga Mkono. Ebu jibu swali hili la msingi na Mimi niwe na pweinti za kutumia kuitetea hoja hii Mkuu.
 
Wewe na Polepole nani anaijua katiba ya CCM?
We acha upumbavu, Polepole aliokotwa tu Magu, wenzako tulinaijua CCM kindakindaki tulianza tukiwa chipukizi wa CCM, baadaye umoja wa vijana mpk utuzima, Polepole anaijua katiba kuzidi wengine kwa kuwa aliwahi kuwa mwenezi au? We upuuzi.
 
Huenda una umr mdogo hujui vitu vingi halafu unataka mijada.

Mwaka 1995 na 2000: Benjamin Mkapa alipata uteuzi wa pili bila upinzani mkubwa ndani ya chama.

Mwaka 2005 na 2010: Jakaya Kikwete alipendekezwa na vikao vya chama kuwa mgombea kwa vipindi vyake viwili bila upinzani wa maana.

Mwaka 2015 na 2020: Hayati Magufuli alipendekezwa na chama kwa vipindi viwili. Kipindi cha pili akiwa mgombea pekee, bila kupingwa ndani ya chama.

Utaratibu huu unaonyesha kuwa ndani ya CCM, rais aliyeko madarakani kwa muhula wa kwanza huwa na nafasi ya kupitishwa kuwa mgombea pekee,
Uteuzi wa kwanza Samia aliupata lini? Lini aliwahi kuomba kugombea urais kwa kuchukua fomu na kutafuta wadhamini na akapitishwa kuwa mgombea wa CCM kwa awamu ya kwanza?

Tafuta mifano mingine, acha kuchanganya mambo.
​
 
Wanaukumbi.

Mchakato wa Rais Samia kupitishwa kuwa mgombea pekee wa CCM kwa uchaguzi wa 2025 ni wa kihalali kwa mujibu wa Katiba ya CCM, na umefuata historia na utaratibu wa chama uliodumu kwa miongo kadhaa. Wanachama wa CCM, viongozi wa chama, na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuelewa kuwa kuteuliwa kwa mgombea mmoja haimaanishi kukandamiza demokrasia, bali ni matokeo ya mshikamano wa chama na imani kwa uongozi uliopo.

Utaratibu huu unaonyesha kuwa ndani ya CCM, rais aliyeko madarakani kwa muhula wa kwanza huwa na nafasi ya kupitishwa kuwa mgombea pekee, kama anatimiza masharti ya kikatiba na hajatenda kosa la kimaadili au kisiasa lililofifisha imani ya chama kwake.

CCM kwa miaka yote imekuwa na utaratibu usioandikwa moja kwa moja, lakini uliojengeka kwa misingi ya muendelezo wa uongozi uliopo madarakani. Mifano ya kihistoria ni kama ifuatavyo:

Mwaka 1995 na 2000: Benjamin Mkapa alipata uteuzi wa pili bila upinzani mkubwa ndani ya chama.

Mwaka 2005 na 2010: Jakaya Kikwete alipendekezwa na vikao vya chama kuwa mgombea kwa vipindi vyake viwili bila upinzani wa maana.

Mwaka 2015 na 2020: Hayati Magufuli alipendekezwa na chama kwa vipindi viwili. Kipindi cha pili akiwa mgombea pekee, bila kupingwa ndani ya chama.

Humphrey Polepole, ambaye kwa wakati huo alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, na mjumbe wa vikao vya juu vya chama, aliunga mkono mchakato huo bila kupinga kwamba ulikuwa “haramu” au wa kibaguzi kisiasa. Hivyo basi, endapo anahoji uhalali wa Rais Samia kuwa mgombea pekee leo, anapaswa pia kuhoji uhalali wa mchakato wa Magufuli mwaka 2020 — ambao yeye binafsi aliushiriki kikamilifu.
Uhalali unatokana na mchakato halali.Huwezi kuteua mtu na kumtangaza bila kipitia process kadhaa afau useme ni halali
 
Miaka 6 akiwa makamu wa raisi ,miaka 4 akiwa raisi ,kihesabu ni miaka 10, mchakato uanze upya wanaotaka uraisi wachukue form wachujwe na wakapigiwe kura, tusitumie kichaka cha cha kuiita awamu ya sita wakati ni awamu ya tano iliyomaliza muda wake, ili kumpa mtu miaka 15 ya uongozi
 
Huenda una umr mdogo hujui vitu vingi halafu unataka mijada.

Mwaka 1995 na 2000: Benjamin Mkapa alipata uteuzi wa pili bila upinzani mkubwa ndani ya chama.

Mwaka 2005 na 2010: Jakaya Kikwete alipendekezwa na vikao vya chama kuwa mgombea kwa vipindi vyake viwili bila upinzani wa maana.

Mwaka 2015 na 2020: Hayati Magufuli alipendekezwa na chama kwa vipindi viwili. Kipindi cha pili akiwa mgombea pekee, bila kupingwa ndani ya chama.

Utaratibu huu unaonyesha kuwa ndani ya CCM, rais aliyeko madarakani kwa muhula wa kwanza huwa na nafasi ya kupitishwa kuwa mgombea pekee,
hawa wote walichukua fomu wakajaza na kupata wadhamini.
pia awamu zao za kwanza walichujwa ndani ya chama kwa kugombea na makada wengine
nyie mnataka huyo mama awe rais mara mbili kwa dezo tu? pumbafu kabisa
 
Angalia ulivyokuwa punguani Polepole kwa ni Mungu kila atakachasema unakubali tu bila hata kutumia akili zako kidogo alizokupa Mungu..

Ngoja nikupe darsa.

1. Katiba ya CCM na Uteuzi wa Mgombea Urais

Kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 (Toleo la 2022):

Ibara ya 39(1) inasema:
“Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya CCM hupendekezwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.”

Ibara ya 40 inaeleza utaratibu wa uteuzi kuwa ni kupitia vikao halali vya chama, ambapo jina la mgombea hupitishwa baada ya mchakato wa ndani, ikiwa ni pamoja na mapendekezo kutoka mikoa, Kamati Kuu (CC), na hatimaye NEC na Mkutano Mkuu.

Katika mazingira ya Rais aliyepo madarakani, hasa katika kipindi cha muhula wake wa kwanza, historia inaonyesha kuwa CCM imekuwa ikiteua mgombea huyo kuwa mgombea pekee kwa kipindi cha pili — hali hii si mpya, si haramu, na wala haijakiuka Katiba ya chama..

Sasa endelea kumsikilza Polepole Mungu wako.
Ritz we ni mkongwe sana humu ila mda mwingine unaongea pumba sana
 
We acha upumbavu, Polepole aliokotwa tu Magu, wenzako tulinaijua CCM kindakindaki tulianza tukiwa chipukizi wa CCM, baadaye umoja wa vijana mpk utuzima, Polepole anaijua katiba kuzidi wengine kwa kuwa aliwahi kuwa mwenezi au? We upuuzi.
Kwa hiyo mimi kuuliza kati ya Polepole na mleta mada nani anaijua vizuri katiba ya CCM ndio kunanifanya mpuuzi? Kama tu kuuliza hili swali unaniita mpuuzi, je nitakosea kukuambia wewe ni mjinga? Kumbuka mjinga sio tusi, ni hali ya kutokujua jambo. Ukielimishwa hutakuwa mjinga tena
 
Miaka 6 akiwa makamu wa raisi ,miaka 4 akiwa raisi ,kihesabu ni miaka 10, mchakato uanze upya wanaotaka uraisi wachukue form wachujwe na wakapigiwe kura, tusitumie kichaka cha cha kuiita awamu ya sita wakati ni awamu ya tano iliyomaliza muda wake, ili kumpa mtu miaka 15 ya uongozi
Utaratibu huu unaonyesha kuwa ndani ya CCM, rais aliyeko madarakani kwa muhula wa kwanza huwa na nafasi ya kupitishwa kuwa mgombea pekee, kama anatimiza masharti ya kikatiba na hajatenda kosa la kimaadili au kisiasa lililofifisha imani ya chama kwake.
 
We una hangaika bure hayo yote wanayajua issue ni kwamba kifo cha Magu kimeharibu mipango yao. Wana mtu wao hao wanaolialia sasa wanaona mpk 2030 mambo mengi yatakuwa yameshabadilika. Hakuna anayelinda katiba hapo hao wanafikiria kutumia matumbo. Kwanza hawakutaka kabisa Samia awe walitaka kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania waziwazi, leo ndio wanajua katiba ya chama? Wanafki wakuda hao. Pili hawakutegemea pengine km angegombea mwaka huu 2025, sasa ndio wamepanic kabisa, Samia kwa uwezo mkubwa aliouonesha ningesikitika sana binafsi km asingegombea, huyu mama ametuliza nchi, ameunganisha nchi, hana ukabila, hana ukanda, maendeleo anayapeleka mikoa na kanda zote bila ubaguzi, watanzania tunataka turudi kwa mtu km yule mbaguzi, aliigawanya nchi ktk kanda, alieneza ukabila waziwazi ndio maana mara baada ya kufa tu mitandao ilijaa post za kikanda, za kikabila. Magufuli leo hii nchi ingeshaparanganyika, aliigawa nchi. Tumshukuru Mungu kutupatia Samia tuwapuuze hao washenzi.
Na ameshatuahidi watanzania katiba mpya -- wahuni wanataka wamtoe tusipate katiba mpya hilo halikubaliki
 
hawa wote walichukua fomu wakajaza na kupata wadhamini.
pia awamu zao za kwanza walichujwa ndani ya chama kwa kugombea na makada wengine
nyie mnataka huyo mama awe rais mara mbili kwa dezo tu? pumbafu kabisa
Ibara ya 39(1) inasema:
“Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya CCM hupendekezwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.” Ulivyokuwa punguani unaona fomu ni katiba.
 
Utaratibu huu unaonyesha kuwa ndani ya CCM, rais aliyeko madarakani kwa muhula wa kwanza huwa na nafasi ya kupitishwa kuwa mgombea pekee, kama anatimiza masharti ya kikatiba na hajatenda kosa la kimaadili au kisiasa lililofifisha imani ya chama kwake.
Lini alichukua form na kutafuta wadhamini? Tusigeuze uraisi kama mali ya mtu ,
 
Back
Top Bottom