GE2025 Samia Suluhu Hassan ni Mgombea Halali Kikatiba na kihistoria

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mwaka 1995 na 2000: Benjamin Mkapa alipata uteuzi wa pili bila upinzani mkubwa ndani ya chama.
Kukwepa swali la msingi la fomu ilichukuliwa unafifisha nguvu ya hoja yako ambayo ninataka kuiunga Mkono. Ebu jibu swali hili la msingi na Mimi niwe na pweinti za kutumia kuitetea hoja hii Mkuu.
 
Wewe na Polepole nani anaijua katiba ya CCM?
We acha upumbavu, Polepole aliokotwa tu Magu, wenzako tulinaijua CCM kindakindaki tulianza tukiwa chipukizi wa CCM, baadaye umoja wa vijana mpk utuzima, Polepole anaijua katiba kuzidi wengine kwa kuwa aliwahi kuwa mwenezi au? We upuuzi.
 
Uteuzi wa kwanza Samia aliupata lini? Lini aliwahi kuomba kugombea urais kwa kuchukua fomu na kutafuta wadhamini na akapitishwa kuwa mgombea wa CCM kwa awamu ya kwanza?

Tafuta mifano mingine, acha kuchanganya mambo.
​
 
Uhalali unatokana na mchakato halali.Huwezi kuteua mtu na kumtangaza bila kipitia process kadhaa afau useme ni halali
 
Miaka 6 akiwa makamu wa raisi ,miaka 4 akiwa raisi ,kihesabu ni miaka 10, mchakato uanze upya wanaotaka uraisi wachukue form wachujwe na wakapigiwe kura, tusitumie kichaka cha cha kuiita awamu ya sita wakati ni awamu ya tano iliyomaliza muda wake, ili kumpa mtu miaka 15 ya uongozi
 
hawa wote walichukua fomu wakajaza na kupata wadhamini.
pia awamu zao za kwanza walichujwa ndani ya chama kwa kugombea na makada wengine
nyie mnataka huyo mama awe rais mara mbili kwa dezo tu? pumbafu kabisa
 
Ritz we ni mkongwe sana humu ila mda mwingine unaongea pumba sana
 
We acha upumbavu, Polepole aliokotwa tu Magu, wenzako tulinaijua CCM kindakindaki tulianza tukiwa chipukizi wa CCM, baadaye umoja wa vijana mpk utuzima, Polepole anaijua katiba kuzidi wengine kwa kuwa aliwahi kuwa mwenezi au? We upuuzi.
Kwa hiyo mimi kuuliza kati ya Polepole na mleta mada nani anaijua vizuri katiba ya CCM ndio kunanifanya mpuuzi? Kama tu kuuliza hili swali unaniita mpuuzi, je nitakosea kukuambia wewe ni mjinga? Kumbuka mjinga sio tusi, ni hali ya kutokujua jambo. Ukielimishwa hutakuwa mjinga tena
 
Utaratibu huu unaonyesha kuwa ndani ya CCM, rais aliyeko madarakani kwa muhula wa kwanza huwa na nafasi ya kupitishwa kuwa mgombea pekee, kama anatimiza masharti ya kikatiba na hajatenda kosa la kimaadili au kisiasa lililofifisha imani ya chama kwake.
 
Na ameshatuahidi watanzania katiba mpya -- wahuni wanataka wamtoe tusipate katiba mpya hilo halikubaliki
 
hawa wote walichukua fomu wakajaza na kupata wadhamini.
pia awamu zao za kwanza walichujwa ndani ya chama kwa kugombea na makada wengine
nyie mnataka huyo mama awe rais mara mbili kwa dezo tu? pumbafu kabisa
Ibara ya 39(1) inasema:
“Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya CCM hupendekezwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.” Ulivyokuwa punguani unaona fomu ni katiba.
 
Lini alichukua form na kutafuta wadhamini? Tusigeuze uraisi kama mali ya mtu ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…