GE2025 Samia Suluhu Hassan ni Mgombea Halali Kikatiba na kihistoria

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
SAsa MBONA mnaogopa kufanya uchaguzi WA ndani?


Bro Alex on da beats
 
Ibara ya 39(1) inasema:
“Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya CCM hupendekezwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.” Ulivyokuwa punguani unaona fomu ni katiba.
Uongozi ni mchakato kaka, kuchukua form ni sehemu ya mchakato, kupendekezwa na halmashauri kuu pia ni mchakato, tusiweke shortcut kwenye kupata mgombea
 

Vijana wote wa ccm ambao mnajibu hoja za pole pole mnajibu kwa mihemuko na sio kwa facti, hoja hapa iko hivi:

1 .Mama Samia amechukua form ya kuomba kugombea Urais kupitia ccm? Yes/no

Mama Samia alipita bara na visiwani kuomba wadhamini? Yes/no

Marais wenzake waliopita walifanya hilo zoezi la kuchukua form au hawakufanya?

Ajenda ya Mkutano mkuu ilikuwa ni kumchagua kaimu mwenyekiti au kupitisha majina ya mgombea urais?


Na mwisho, kwanini mpaka leo msajili wa vyama yupo kimya ? Haha
 
H
Hakuna mahali Katiba imevunjwa !
Wakae kwa kutulia tu !
 
Lini alichukua form na kutafuta wadhamini? Tusigeuze uraisi kama mali ya mtu ,
Usiwe punguani kijana tumia akili yako Magufuli amekufa unataka achukue fomu?

Niambie Rais yupi awamu yake ya pili alichukuwa fomu?

CCM kwa miaka yote imekuwa na utaratibu usioandikwa moja kwa moja, lakini uliojengeka kwa misingi ya muendelezo wa uongozi uliopo madarakani. Mifano ya kihistoria ni kama ifuatavyo:

Mwaka 1995 na 2000: Benjamin Mkapa alipata uteuzi wa pili bila upinzani mkubwa ndani ya chama.

Mwaka 2005 na 2010: Jakaya Kikwete alipendekezwa na vikao vya chama kuwa mgombea kwa vipindi vyake viwili bila upinzani wa maana.

Mwaka 2015 na 2020: Hayati Magufuli alipendekezwa na chama kwa vipindi viwili. Kipindi cha pili akiwa mgombea pekee, bila kupingwa ndani ya chama.
 
Ibara ya 39(1) inasema:
“Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya CCM hupendekezwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.” Ulivyokuwa punguani unaona fomu ni katiba.
wewe ni boya kweli, kuchukua fomu ya kuomba urais na kuzunguka bara na visiwani kupata wadhamini haimo kwenye katiba?
 
ama mchakato huu ni haramu, basi uharamu huo ulianza tangu miaka mingi, hasa mwaka 2020 ambapo Polepole mwenyewe alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu na NEC iliyompitisha Magufuli kuwa mgombea pekee. Haikuwahi kusemwa kuwa ni kuvunja katiba, bali kuliitwa “mshikamano wa chama.”

Kama Polepole anakataa uhalali wa Samia kupitia vikao hivyo, anapaswa pia kukiri kuwa alishiriki katika kuhalalisha mchakato aliouita sasa "haramu", hivyo kuonesha ukinzani wa kisiasa usio wa kikatiba wala wa kihistoria.
 
Hata Magufuli hakupitshwa kihuni kiasi hiki kupitia mkutano ambao hauna agenda ya uchaguzi.
Usijifanye hujui Msoga ana malengo yake sawa na ule mtandao wake kabla ya kuteuliwa.
 


Maswali yangu umeelewa? Jibu Hoja
 
wewe ni boya kweli, kuchukua fomu ya kuomba urais na kuzunguka bara na visiwani kupata wadhamini haimo kwenye katiba?
Usiwe punguani wewe hayawani.

Utaratibu huu unaonyesha kuwa ndani ya CCM, rais aliyeko madarakani kwa muhula wa kwanza huwa na nafasi ya kupitishwa kuwa mgombea pekee, kama anatimiza masharti ya kikatiba na hajatenda kosa la kimaadili au kisiasa lililofifisha imani ya chama kwake.
 
Hata Magufuli hakupitshwa kihuni kiasi hiki kupitia mkutano ambao hauna agenda ya uchaguzi.
Usijifanye hujui Msoga ana malengo yake sawa na ule mtandao wake kabla ya kuteuliwa.
Kama mchakato huu ni haramu, basi uharamu huo ulianza tangu miaka mingi, hasa mwaka 2020 ambapo Polepole mwenyewe alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu na NEC iliyompitisha Magufuli kuwa mgombea pekee. Haikuwahi kusemwa kuwa ni kuvunja katiba, bali kuliitwa “mshikamano wa chama.”
 
Naenda kunywa kahawa tarudi kuwajibu Chadema-Kata.
 
Hupati uteuzi kwa kuandika mandishi mengi yasiyo na point hata moja
 

Mhula wa urais una miaka mingapi kikatiba?

President by default unaita mhula, kwa katiba ipi imehesabu ni mhula wake wa kwanza.

Sawa hata ukisema ni mhula:
Amewaomba lini wana CCM kuwa anataka kuendelea/kuanza?

1: Unaenda kumkabidhi mtu nchi bila yeye kuomba na kuonyesha utayari, mwaka kesho akiondoka bila kuaga utamtafutia wapi na kwa ushahidi gani?

2: Watu tumekuwa machawa mpaka tunapitiliza, nchi yetu imekuwa kitu kidogo mpaka tunamkabidhi mtu kuiongoza bila kuombwa, bila wadhamini wa anakotokea?

3: Wewe unaweza kumpatia mtu sasa hivi bila dhamana/bila kuandika dhamira, bila mashahidi wowote shilingi milioni moja na useme unadhamana nae ya kukopeshana hiyo pesa? Je nchi?


4: Mdhamini wake ni nani?
Dhamira kaionyesha wapi?
Unafirki msingi wa katiba kuhitaji uchaguliwe kutoka kwenye chama ni nini? Mnafanya auto-pilot?

5: Kama kwenye chama kwenyewe umeruka ukuta, je utashindwa kuruka ukuta kwenye kuendesha nchi?

NB: Tangu mmekuwa machawa na kuwekeza kwa watu binafsi badala ya chama, serikali na mifumo yake ni shida tupu. Mnamilikisha vitu vya jumuiya kwa mtu ili kumtukuza yeye wakati mifumo inabaki inaelea na kuonekana haipo na haiwajibiki.
 
Vikao vya ndani inakuwaga na kanuni, taratibu na miongozo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…