GE2025 Samia Suluhu Hassan ni Mgombea Halali Kikatiba na kihistoria

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Huu ndo muhula wake wa kwanza kama rais wa kuchaguliwa hvyo natarajia ccm itampitisha tena 2030

Chura kiziwi mikumi tena,ccm hoyeee
 
Kwenye rangi nyekundu....''hakuchaguliwa kama Raisi kwa muhula unaokwisha bali alikuwa Raisi kutokana na katiba baada ya Raisi aliyekuwepo madarakani kufariki.''
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hususan Ibara ya 37(5), pale ambapo Rais aliyeko madarakani hufariki dunia, Makamu wa Rais huapishwa kuwa Rais na kumalizia kipindi kilichobaki cha muhula wa urais wa aliyefariki. Hii ina maana kwamba:

-
Rais Samia Suluhu Hassan, baada ya kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mnamo Machi 17, 2021, aliapishwa rasmi kuwa Rais mnamo Machi 19, 2021
- Kisheria, hakuchaguliwa kwa muhula mpya, bali alichukua nafasi ya Rais Magufuli na kumalizia awamu ya tano ya uongozi ambayo Magufuli alikuwa ameianza mwaka 2020.

-
Kwa hivyo, kipindi cha uongozi wa Rais Samia kuanzia 2021 hadi Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ni mwendelezo wa awamu ya tano, si awamu mpya ya sita.


Kwa sasa, Rais Samia anamalizia muhula wa pili wa Magufuli, lakini kisheria ni sehemu ya awamu ya tano ya urais. Iwapo atagombea na kushinda uchaguzi wa 2025, ndipo ataanza rasmi awamu yake ya kwanza kama Rais aliyechaguliwa moja kwa moja na wananchi.
 
Mkuu
Mkuu hebu tufidiishe vizuri kikwete katika vipindi vyake viwili alipendekezwa kama usemavyo je hakuwa anatafuta wadhamini ndani ya chama?
 
hayo mambo ndo yanawakumba wapinzania miaka na miaka -- kama sasa yanatokea ndani kwenu ni maendeleo kwa taifa -- walikua nyuma nyuma hawa
 
Mkuu kama usemavyo kuhusu kikwete na Mkapa ja hao waheshimiwa hawakuwahi kupita wilayani na mikoani kupata wadhamini ndani ya chama?
 
Ewaaah !
Na huo ndio Ukweli mchungu !
Ndio maana tunawaambia wanafiki wenye kumsagia kunguni huko Chamani kwamba wakae kwa kutulia !
Kwa maana hakuna mahali Katiba imevunjwa 😄🤷🏿‍♂️👍
 
hii sio kweli 🤣
 
 
Reactions: jjt
lkn kwa utaratibu gani|?ishu sio kuwa mgombea binafsi|?but utaratibu kumpata ndo watu wanasema umekosewa
 
Upumbavu
 
Huu ni upotoshaji wa makusudi unaofanywa na machawa.

Kwa kuwa amekuwa madarakani kwa miaka 4+, inahesabika kama muhula kamili

Katiba inasema hivi:-

Ibara ya 40 (4)
"Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu."
 
Ukweli ni upi?
Ukweli ni kuwa kama Makamu atachukua Urais na kuhudumu Kwa zaidi ya miaka mitatu, basi atahesabika amefanya kazi Kwa mhula mzima wa miaka mitano.

Hivyo Samia hiki ni kipindi chake Cha mwisho na si Cha mwanzo!
 
Reactions: Lax
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…