GE2025 Samia Suluhu Hassan ni Mgombea Halali Kikatiba na kihistoria

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Acheni longolongo toeni form za kugombea Urais watu washindanishwe.
Muhura alioshika kikatiba umeisha baada ya mtangulizi wake kuondoka.
 
Samia kapitishwa kinyume Cha Sheria japo kuwa Kuna vichaa wachache wanapindisha ukweli.Bora apumzike kabla hatujakinukisha kupinga utaratibu mbovu uliotumika kumpata MGOMBEA Hatuko tayari hata kidogo
 
Mkutano Mkuu, hata ajenda tu ya kumpitisha mgombea haikuwepo. Wajumbe hawakuwa na taarifa ya jambo hilo kujadiliwa, na hata kutajwa tu kwenye mkutano huo!

Bado mtu unaona ulaghai wa aina hii watu hawawezi kuelewa maana yake ni nini?
Mnawadharau sana waTanzania, huku wenyewe mkiwa wajinga wakubwa.
 
Huu uzi mzito sana kwako nakushauri tu rudi kwenye mipasho au endelea kuwa msomaji.
"Huu uzi mzito..."? HAAAAaa!
Hzi tabia za ulaghai laghai hata katika maswala mazito ya nchi...; hizi tabia huwa mnafunzwa wapi nyinyi?
 
Ibara ya 40 inaeleza utaratibu wa uteuzi kuwa ni kupitia vikao halali vya chama, ambapo jina la mgombea hupitishwa baada ya mchakato wa ndani, ikiwa ni pamoja na mapendekezo kutoka mikoa, Kamati Kuu (CC), na hatimaye NEC na Mkutano Mkuu.
Samia "alipitia vikao halali gani vya chama" na jina lake kupitishwa?
Unajuwa kusoma na kuelewa kilicho andikwa ambacho wewe mwenyewe unakiwasilisha ili kutetea hoja yako?
 
Alichaguliwa lini kuwa Rais kwa huo muhula wa kwanza unaousema? Samia aliapishwa kuwa Rais kumalizia awamu ya Tano ya Urais baada ya Rais aliyekuwepo madarakani kufariki, na hiyo ni kwa Mujibu wa katiba.
 
Mbona hamba hoja hapo?
watakuja kujisifu baadae kwamba CCM ni moja na ina uimara na tofauti zao ni kipindi cha kupata mgombea tu baada ya hapo wapo pamoja -- sio kama wale wengine (chadema) kutwa walikua wanatufatilia sisi wakakosa hata muda wa kujenga chama chao, angalia kwa mfano mwenyekiti wao alikua na kesi mahakamani( muda huo TAL atakua kasharudi uraiani) lakini mwenyekiti mstaaffu wao hakwenda kutoa support mahakamani lakini kwa nguvu na ukubwa wa ccm alifika kuhudhuria uzinduzi wa dira --- siii siiemu oyeee --- oyeee

mkuu hiki nilichoandika juu lazima wafanye mkuu --- hii walilizingatie na kuna wananchi watawaunga mkono kwenye hoja hiyo mkuu
 
Alichaguliwa lini kuwa Rais kwa huo muhula wa kwanza unaousema? Samia aliapishwa kuwa Rais kumalizia awamu ya Tano ya Urais baada ya Rais aliyekuwepo madarakani kufariki, na hiyo ni kwa Mujibu wa katiba.
ule ndo muhula wake wa kwanza according to katiba ya nchi
 
Na bahati nzuri sana, ukimuacha Polepole HAKUNA Mwana CCM anayepinga uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais wa CCM. Kinachoshangaza sana, wanaopinga ni Wana Chadema ambao wao kwanza wamesema HAWASHIRIKI Uchaguzi Mkuu,lakini ndio wamekuwa mstari wa mbele kufuatilia kwa karibu mchakato wa CCM kutafuta wagombea wao! Mambo ya ajabu kabisa!!
 
Kwa mujibu wa katiba ya chama chake ni haram!

Kwa mujibu wa dini yake ni haram pia!
 
Cha kufurahisha ni kuona wafuasi wa Chadema wamejikita kupambania uchaguzi wa CCM.😀
 
Wewe punguani kweli kosa langu lipo wapi?
Jamaa akusemehe bure maana ww ni mzee, wewe ni tunda la propaganda za zamani, kwenye dunia hii digital ww ni bendera fuata upepo hujui lolote.
 
Cha kufurahisha ni kuona wafuasi wa Chadema wamejikita kupambania uchaguzi wa CCM.😀
Hawapambanii bali wanawazodoa mlivyo analogia kwenye ulimwengu huu digital. Yaani usidhani mnafuatiliwa kwa ubora, bali ni kwa ajili ya kuwadhihaki. Na uzuri mnajaa vizuri kwenye mfumo, maana huku hamna nguvu ya vyombo vya dola.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…