MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,952
- 10,500
safari hii ICC mmeitafuta wenyeeewe kwa lazima haijalishi ni umeolewa unampikia vizuri ICC inakuhusu tu.
Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, (CCM), Mh. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15/10/2020 amewambia wakazi wa Chunya mkoani Mbeya kuwa wasipige kura kwa Chama Kingine kwa sababu hata wakipiga kwingine Chama Cha Mapinduzi kinaenda kuunda serikali.
Amesisitiza kuwa watashinda vikubwa sana Tanzania, na amefananisha kupigia kura kwa chama kingine kama kitendo cha kumwaga sukari Ziwa Viktoria na kutegemea maji yatakuwa matamu, ambacho ni sawa na kupoteza sukari yako.
Mh. Samia amesisitiza kuwa maendeleo watakayoyaleta sio kwa wana CCM peke yake na wale ambao hawatokipigia Chama Cha Mapinduzi basi kura yao itawasuta pale watakapokuwa wanaletewa maendeleo.
mwenzenu analia kuibiwa na dola yote ipo mikononi mwake. na nyie iandaeni