Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

Mkuu yani kabisa tume huru mlitaka ije mezani kama ugali?

Walichofanikiwa mashabiki wa chadema kupigania kwa nguvu zote kwa miaka 5 hii nibkujadili kingereza cha Magu tu. Hakuna mengine.

Ulitaka nini kifanyike labda?
 
Mkuu yani kabisa tume huru mlitaka ije mezani kama ugali?

Walichofanikiwa mashabiki wa chadema kupigania kwa nguvu zote kwa miaka 5 hii nibkujadili kingereza cha Magu tu. Hakuna mengine.
Hiyo nguvu utaiona soon..
 
Hakuna yoyote anayeweza kubisha kama hamtatangazwa. Hata Lissu na CDM wanajua hilo.

Lakini cha kujiuliza nini kitatokea baada. Kumbuka moja kati ya vutu ambavyo hamuwezi ni kufanya mambo kwa siri, vitendo vyenu mnafanya hadharani bila uwoga. Je jumuiya za kimataifa zikiwatenga mtaweza kumaliza miradi mlianzisha?

Mtafanya nini TL baada ya uchaguzi? TL anaonyesha dalili kwamba anaweza ku mobilize vijana waliokata tamaa.

Je mtabadili katiba ili JPM aendelee muhula wa 3 na 4 n.k?
View attachment 1601260

Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, (CCM), Mh. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15/10/2020 amewambia wakazi wa Chunya mkoani Mbeya kuwa wasipige kura kwa Chama Kingine kwa sababu hata wakipiga kwingine Chama Cha Mapinduzi kinaenda kuunda serikali.

Amesisitiza kuwa watashinda vikubwa sana Tanzania, na amefananisha kupigia kura kwa chama kingine kama kitendo cha kumwaga sukari Ziwa Viktoria na kutegemea maji yatakuwa matamu, ambacho ni sawa na kupoteza sukari yako.

Mh. Samia amesisitiza kuwa maendeleo watakayoyaleta sio kwa wana CCM peke yake na wale ambao hawatokipigia Chama Cha Mapinduzi basi kura yao itawasuta pale watakapokuwa wanaletewa maendeleo.
 
Wanasema anayejiona amesimama aangalie asianguke.. Unaweza ukajiaminisha una polisi, NEC etc LAKINI MUNGU AKIAMUA KUWASHUSHA KWA KIBURI INAKUWA
 
Anachomaanisha ni kuwa, amewaomba watu wa vyama vingine wasio ccm wawapigie kura. Then akasema ata wasipokipigia chama cha ccm kitashinda. Hapa ni kwa sababu anaamini na anaimani kuwa wanachama wa ccm na wengine labda wasio na vyama wanatosha kuwapa ushindi. Ndo maana anasisitiza watu wa vyama vingine waelewe kuwa wasipo wapa ccm n sawa na kupoteza kura zao tu.
 
Upe mtando huu heshima take tafadhali ,sema mtandao pendwa zaidi ,Tanzania,Africa. Na karibia na duniani.
Ninaukubali na natambua mchango wake katika swala zima la kupashana habari na kwamba ni mtandao unaowapa nafasi watumiaji wake kujadili mambo yao bila wasiwasi, sema kunu jamaa hapo juu alitaka kujifanya mbabe, kwamba anaweza kufichua mambo mazito ya Dada samia, ndo nakwambia aende kwenye mitandao mikubwa Kama ana nguvu sio huku anakolindwa.
 
Ushindi wa CCM kilichobaki ni asilimia tu ila ni dhahiri.
 
Watoke hazarani watwambie maamuzi wanayowenyewe au nisanduku lakura
 
Sasa kama kura zikiwa nyingi kwa chama kingine wao watashinda vipi?

Hii ndo ishara ya kwamba Uchaguzi wetu hauamuliwagi kwa wingi wa kura za halali za kwenye maboksi
Asituvunje moyo sisi tupige kura wanatapatapa kwamaana nimemshangaa igp nayeye anazungumza kwanadharia kunataarifa hii hizotaarifa jamani nisiri yapolice kama umezipata kazi yakokamata hiyo nidalili kunawatu watabambikwa kesi hapa iliwaseme tulisema mm najuwa ulipewa cheo narais niwtz tumekupa asingekuwa rais bila sisi wananchi kumpa tunakuomba usimuonee mtu
 
Najiuliza tu kama akina Lipumba, Lissu na Seif wangetamka maneno hayo ingekuwa sawa!

Nchi hii inaweza kuwa na sheria nzuri kabisa lakini kwa kuwa zina-apply selectively, zinaonekana kutofanya kazi!! Maneno alosema mama Samia si ya kutumika katika nchi inayopta viongozi kupitia chaguzi!!
 
Eti naskia Kasimu Majaaliwa kule Pemba kwenye mkutano wake na vikosi aliwaambia kuwa 95 Alishinda hatujampa, 2000 alishinda hatukumpa, 2005 kashinda hatukumpa, 2010 alishinda hatukumpa, 2015 alishinda hatukumpa, na mwaka huu atashinda na hatutompa, kweli?

Damu ikimwagika basi na viongozi kama hawa yakwao imwagike tu
 
Back
Top Bottom