Samia Suluhu tumseme kwa mengine sio hili la kutumia watu jini Makata mtoa roho

Samia Suluhu tumseme kwa mengine sio hili la kutumia watu jini Makata mtoa roho

Kuna dada nimeona mtandaoni anadai eti alikuwa anaumwa.

Akasema eti Samia Suluhu Hassan alimtumia jini Makata ambalo kidogo limtoe roho. Akadai eti amerudi na amepona yupo lelelelee. Jini makata Samia alitoe wapi labda jini maimuna. Makata? 🤣🤣. Kwanza jini Makata ukilishika bila kuliamkia au ikiwa na janaba linakunyonya damu unakufa.

Sasa wakuu, mimi haya mambo ya kusema Samia anaweza kutuma jini makata hilo napinga. Kwanza jini makata atalitumaje? Kwa ndege?

Kwani majini yanaheshimu watu waliojipachika Urais hadi ayatume yakubali?

Tumseme kwa mauaji ya 29.10.2025 na kudumaza Miradi ya maendeleoya Tanganyika. Tumshinikie amrudishe Mdude nyagali, Soka, na walio muua Mzee kibao wachukuliwe hatua. Haya ndo yanafanya nimuombee mabaya.

Lakini hili sijui la kutumia majini makata yauwe wanaharakati hana ubavu huo. Mwanamke mwenyewe anaogopa mende, Jini ndo ataligusa. Mnampa ushujaa asiokuwa na uwezo nao.
View attachment 3692049
Hii imeenda
 
Back
Top Bottom