DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa serikali yake itajenga uwanja mkubwa wa michezo katika eneo la Msoga, Chalinze, mkoani Pwani iwapo atapata ridhaa ya wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akizungumza leo Jumapili, Septemba 28, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Msata, Dkt. Samia amesema ujenzi wa uwanja huo ni sehemu ya heshima na shukrani kwa Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye anatoka katika eneo hilo.
“Hii ni shukrani yetu kwa utumishi wa Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Mengi tumeyapa jina Kikwete lakini sio Msoga, hapa hatukufanya kitu. Kwahiyo uwanja ule tutauweka Msoga kuonesha shukrani yetu,” amesema Dkt. Samia.
Pia Soma: GE2025 - Kikwete: Wabunge wote wa Pwani bunge lijalo watatoka CCM, hatuko tayari kuchanganya pumba na mchele