GE2025 Samia: Tutajenga uwanja mkubwa wa michezo Msoga kumuenzi Kikwete

GE2025 Samia: Tutajenga uwanja mkubwa wa michezo Msoga kumuenzi Kikwete

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
“Hii ni shukrani yetu kwa utumishi wa Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Mengi tumeyapa jina Kikwete lakini sio Msoga, hapa hatukufanya kitu. Kwahiyo uwanja ule tutauweka Msoga kuonesha shukrani yetu,” amesema Dkt. Samia.

Ajabu ni kwamba huyo JK mwenyewe hajafanya jambo kubwa kama hilo huko Msoga...
 
Huko Msoga kuna timu /uhitaji wa uwanja mkubwa ? Si bora hizo Kodi zao wanazotoa (pesa ni za kwao na sio za watawala) wangewasaidia kupata mashine ya ku-process coconut iwe by products tofauti ikiwemo sukari na mafuta...
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa serikali yake itajenga uwanja mkubwa wa michezo katika eneo la Msoga, Chalinze, mkoani Pwani iwapo atapata ridhaa ya wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza leo Jumapili, Septemba 28, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Msata, Dkt. Samia amesema ujenzi wa uwanja huo ni sehemu ya heshima na shukrani kwa Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye anatoka katika eneo hilo.

“Hii ni shukrani yetu kwa utumishi wa Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Mengi tumeyapa jina Kikwete lakini sio Msoga, hapa hatukufanya kitu. Kwahiyo uwanja ule tutauweka Msoga kuonesha shukrani yetu,” amesema Dkt. Samia.

Pia Soma: GE2025 - Kikwete: Wabunge wote wa Pwani bunge lijalo watatoka CCM, hatuko tayari kuchanganya pumba na mchele​
Washauri wa huyu mama watakuwa na matatizo ya afya ya akili!

Sasa uwanja wa mpira unamsaidia nini mwananchi wa msoga?!

Atleast angewadanganya kuwapa kiwanda cha kusindika juice ya nanasi wangepata ajira..
 
Back
Top Bottom