GE2025 Samia: Tutajenga uwanja mkubwa wa michezo Msoga kumuenzi Kikwete

GE2025 Samia: Tutajenga uwanja mkubwa wa michezo Msoga kumuenzi Kikwete

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Washauri wa huyu mama watakuwa na matatizo ya afya ya akili!

Sasa uwanja wa mpira unamsaidia nini mwananchi wa msoga?!

Atleast angewadanganya kuwapa kiwanda cha kusindika juice ya nanasi wangepata ajira..
Wakibeba zege ya kujenga si ndiyo ajira hizo
 
Tanzania itapata uhuru wa kifikra siku ambayo tutachagua kurudisha fahamu duniani, kwasasa tuendelee kwanza kuhangaika na mawingu, huku real men and women wakiendelea kuandika historia,

They create history Kwa dunia, huku wakitulaghai na mbingu,
Religion is the opium of the people"

Siku tutakapoelewa kuwa hatuna tofauti na wanyama wa porini, tutajifunza maana ya kila mmoja kujiwekea mipaka ya mawindo..

Kwasasa acha wawinde kwenye mipaka yetu, huku sisi tukitafuta thawabu za kuiona pepo, noble men huondolewa Kwa vita sio umbea wa maneno

Nimechanganyikiwa
 
Bahati mbaya sana, hii ni taswira halisi ya uwezo wa mtanzania. Wachache wenye uwezo above average, wengi wetu uwezo anaonyesha maza ndio uwezo wetu, we're not far off.
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa serikali yake itajenga uwanja mkubwa wa michezo katika eneo la Msoga, Chalinze, mkoani Pwani iwapo atapata ridhaa ya wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza leo Jumapili, Septemba 28, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Msata, Dkt. Samia amesema ujenzi wa uwanja huo ni sehemu ya heshima na shukrani kwa Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye anatoka katika eneo hilo.

“Hii ni shukrani yetu kwa utumishi wa Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Mengi tumeyapa jina Kikwete lakini sio Msoga, hapa hatukufanya kitu. Kwahiyo uwanja ule tutauweka Msoga kuonesha shukrani yetu,” amesema Dkt. Samia.

Pia Soma: GE2025 - Kikwete: Wabunge wote wa Pwani bunge lijalo watatoka CCM, hatuko tayari kuchanganya pumba na mchele​
Ndio maendeleo wayatamanio WaTz? Kazi kweli huyu!
 
Estadio di msoga, stede de kikwete, dimba la msoga, kikwete stadium, msoga arena, kikwete complex, signal msoga. Jakaya mrishmo kikwete stadium, JK park, nadhani haya ni majina ya uwanja huo, wachague moja
 
Back
Top Bottom