GE2025 Samia: Tutajenga uwanja mkubwa wa michezo Msoga kumuenzi Kikwete

GE2025 Samia: Tutajenga uwanja mkubwa wa michezo Msoga kumuenzi Kikwete

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ngoja niwaambieni kitu wakuu .

Huo mpango wa ujenzi wa uwanja wa mpira Kikwete alishakuwa nao kitambo sana , almost 15 years ago.

ENeo lilishatengwa na Barabara ilishajengwa tena kwa kiwango cha lami.

Kwa wapitaji wa njia ya Moshi , ukishapita njia panda ya Chalinze mjini unaenda mbele kama KM 9.5 ndiyo unafika Kijiji cha Msoga ,pale kunabarabara mbili zilizojengwa kwa kiwango cha lami zote zikiwa mkono wa kushoto kama tunaelekea Moshi au Tanga ukiwa unatokea njia panda ya Chalinze .

Moja ya njia hizo inaelekea kwenye makazi ya Rais Mstaafu JK ambayo ukinyooka nayo utafika hadi kwenye shule ya msingi Msoga na ndipojengwa Hospital ya Msoga na Barabara nyingine ni ya shortcut inayokwenda kukutana na Barabara ya Morogoro.

Lengo la uwepo wa hiyo Barabara husika hayakuwa kwa ajili ya shortcut kama wengi wanavyodhania , hayo yalikuwa ni maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya huo uwanja ambao ukishakuwa kwenye mipango karibu miaka 20 iliyopita so siyo story mpya kwa wafuatiliaji wa mambo.

i dont believe that, nimeitumia hiyo njia mara nyingi tu kama short cut kuungana na morogoro rd badala ya kuzungukia chalinze na ilijengwa na Magu akiwa bado waziri nafikiri kwa nia hiyo, ramani ya huo mchepuko iko tangia mkoloni aliyechora ramani ya nchi nzima, kila kitu kilishafanywa na mkoloni hakuna jipya …
 
i dont believe that, nimeitumia hiyo njia mara nyingi tu kama short cut kuungana na morogoro rd badala ya kuzungukia chalinze na ilijengwa na Magu akiwa bado waziri nafikiri kwa nia hiyo, ramani ya huo mchepuko iko tangia mkoloni aliyechora ramani ya nchi nzima, kila kitu kilishafanywa na mkoloni hakuna jipya …
Unaonekana unapenda mabishano ya kiswahili aisee 🤣🤣

Hiyo shortcut iliyokuwepo tangu enzi za mkoloni ilikuwa wapi?

Ile njia imepanuliwa almost miaka 20 iliyopita.

Raia wanalipwa fidia watu wanashiriki kuidhinisha ,hiyo nikuonyesha hapakuwa na njia rasmi ,punguza ujuaji itakusaidia kujifunza
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa serikali yake itajenga uwanja mkubwa wa michezo katika eneo la Msoga, Chalinze, mkoani Pwani iwapo atapata ridhaa ya wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza leo Jumapili, Septemba 28, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Msata, Dkt. Samia amesema ujenzi wa uwanja huo ni sehemu ya heshima na shukrani kwa Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye anatoka katika eneo hilo.

“Hii ni shukrani yetu kwa utumishi wa Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Mengi tumeyapa jina Kikwete lakini sio Msoga, hapa hatukufanya kitu. Kwahiyo uwanja ule tutauweka Msoga kuonesha shukrani yetu,” amesema Dkt. Samia.

Pia Soma: GE2025 - Kikwete: Wabunge wote wa Pwani bunge lijalo watatoka CCM, hatuko tayari kuchanganya pumba na mchele​
Mnamuenzi huyu jizi kwa lipi au ni mambo yenu binafsi mliyoyageuza ya taifa?
 
Sawa. Lakini nashauri badala ya kujenga uwanja kumuenzi rais mstaafu, tukajenge lami Kiteto au Nachingwea ili wananchi waepuke na adha ya usafiri hasa msimu wa mvua.
 
Sawa. Lakini nashauri badala ya kujenga uwanja kumuenzi rais mstaafu, tukajenge lami Kiteto au Nachingwea ili wananchi waepuke na adha ya usafiri hasa msimu wa mvua.
Kiteto aisee hapana..kule kwa kweli wanastahili hilo
 
Akina mwashambwa na TAKATAKA zingine hapo vimesikima vigeregere vyao vinavyoambatana na machozi ya kububujikwa.

Huyu bimkubwa hadhi yake ni udiwani hata ubunge sidhani kama anaweza kuwasemea shida wananchi wake, the way alivyo hata sera zake hazina mvuto kwa wenye akili timamu, hajui hata kudanganya.

Babalevo anaweza mpita akili huyu mtu
Hata udiwani au ubalozi wa nyumba kumi hastahili
 
Utaujengea wapi wakati wenye nchi yao wanaichukua 29th ??
 
Back
Top Bottom