mkorinto,
Umenielewa vibaya boss.. Siwezi tumia hicho kifaa hata kwa amri ya mahakama. Na nimesema kabsa hapo mimi ni mtumiaji wa Samsung hasa A-series na Nokia.
Pili ukishataja masuala ya super amoled hio tayari ni sofware na mimi nimezungumzia hardware, maana haina ubishi software na perfomance ya A10 haiwezi simama na A70
Na kama umenisoma vizuri pia nimezungumzia muonekano wa mbele tu, ambao ndio hubeba physical credit za simu na nikijua kabsa muonekano wa nyuma unatofautiana.
Mwisho kabsa, kutofautisha water drop na semi circle ni mpaka uangalie vizuri na tena uwe ushaziona zote mbili
Nimezungumzia hizi sababu A-series nimezitumia kuanzia 2015 ila za mwaka huu kwa mtazamo wangu wamezingua kuchanganya low na mid-range kwenye Series moja.
Rudi nyuma kidogo ukumbuke kila mwenye kipato cha chini aliyekuwa anajitutumua kununua Samsung basi utamkuta na J-series, kipato cha kati A/C-series na kipato cha juu S/Note-series.
Ila leo hii wote wamejaa kwenye A-series, maana wenye uwezo wa S na Note-series n wachache mno.
Sio mbaya sababu simu zinauzika, ila kwa hii series tayari wapenda/watumiaji wa mid-range washaichukulia low end japo kuna shughuli kama A80 ni habari nyingne na hata price tag yake inagonga 1M na point kadhaa.
siwezi fananisha samsung na tecno mzee, sijanyimwa tech kiasi hicho,