Samsung A-series za 2019 naona kama zishaanza kuwa yeboyebo

Samsung A-series za 2019 naona kama zishaanza kuwa yeboyebo

Kalale tu uchambuzi wako sio wa kisayansi
Hiyo Samsung inaizidi nini Tecno?

Screenshot_20191110-002203.png


Screenshot_20191110-002148.png
 
Samsung hata afanyeje kwa upande wangu series ya S yenye mwunekano poa, edge tamu ni S6 Edge, S6 Edge Plus, na S7. Juzi nimeshika S10 Plus, nimeichezea yani sioni tofauti na J6 Plus yangu.

Ingekuwa maamuzi yangu hizi high end angetofautisha hizi za kawaida upande wa user interface. Simu software, namna una navigate kwa mfano Android 9 ni sawasawa mwenye simu ya laki 2 na ya milioni 2. So boring
Nimeshawahi kumiliki S7 Edge, S8+ na Note 9 pamoja na matoleo mengine ya zamani.
Chaguo langu bora kati ya hizi itabaki kuwa S8+.
Simu tamu sana hii.
 
reyzzap, Mbona ni nzuri tu mkuu mimi natumia A10 iko poa sana sidhani kwa price yake kuna kampuni imetoa simu yenye specification nzuri kama hiyo.

Kwenye charge inachukua kama masaa 2 kujaa ila ikijaa unaweza kwenda hata 2 days kama sio heavy user.pia kamera yake ni nzuri kwa price, yaani hii simu kiufupi ni nzuri hata games kubwa zote unaweza kucheza bila shida.

Sikatai flagship ni nzuri zaidi ila wametuwekea midrange nzuri wateja wao kwa bei nzuri mi nadhani ni simu nzuri hata kwenye mauzo nusu ya mwaka huu 2019 imeshika namba 2 ya kwanza iphone XR nitaweka details.

Screenshot_20191029-190333_YouTube.jpeg
 
Tish,
Mkuu ukiangalia vizuri hakuna sehemu nimeiponda hii simu na siwezi fanya hivyo sababu ni kweli ni nzuri kwa namna yake. Kitu kikubwa nilichozungumzia ni wao kuishusha kutoka Mid-range smartphone kuja kwenye low end.

Ni kweli tunasema hii simu ni nzuri, lakini kwa nini kwenye matoleo ya Samsung ya mwaka huu hii simu ndio ya mwisho kwa ubora? Unadhani J-series zingebaki hii simu ingekuwa ya mwisho? Hakika wangeacha J-series ishike nafasi ya low end kama mwanzo, hizi A-series zingemkimbiza hata zaidi ya hapo.

Ubora wa hii simu (kwa mtazamo binafsi) na uzuri wa hii simu (machoni kwa mtu) na bei yake ndogo ndio kumeifanya iuzike sana. Hilo halina ubishi, lakini pia hadhi ya hii simu kuwa ya mwisho kwenye matoleo yao kunaifanya watumiaji wengi wanaichoka wengine hata kuichukia mapema.

Hili nalo halina ubishi, Samsung A10 inaongoza kwa mauzo by shipment lakini inaongoza pia mauzo ya second hand hili tunashuhudia kwenye page za mauzo ya simu used hata hapa kwetu chukulia tu mfano Facebook, kupatana nk matangazo yake ni mengi zaidi ya simu nyingne specificaly Samsung, na watu wanauza kwa discount kubwa, na wengi kuonesha kama tatzo si hela ni simu anakuambia exchange allowed, why?

Kwahiyo kaka,
Hii simu sio mbaya, ila wao wenyewe wameishusha hadhi. Mfano kwanza kuifanya itumie LCD display wakati wenzake wanatumia Amoled, pili kuiwekea plastic cover wakati wenzake wanatumia glass, tatu position ya speaker iliyo kwa nyuma kitu kinachoifanya iwe na speaker quality ndogo kulinganisha na wenzake (simu siku hizi wanaepuka kuweka speaker kwa nyuma sababu zinakuwa nyembaba sana kwahiyo speaker nayo itakuwa nyembaba hivyo kupoteza ubora, matokeo yake wanaweka speaker kwa pembeni).

Ukizungumzia battery hii ina 3400 mAh kama sikosei na A70 ana 4500mha, umeona hilo gap? Kwanini nasema wameamua kuishusha hadhi wenyewe? Tunavyojua jinsi miaka inavyoenda basi unaboresha toleo la simu.

Kwanini Samsung,

A-series ya mwaka 2016 itumie Amoled display halafu ya 2019 miaka mitatu baade unarudi tena nyuma unatumia LCD teknolojia ya mwaka 1992?

Samsung A9 Pro 2016 ina 5000 mha ukiwa unaweza piga hata siku 3 data on na A10 ya 2019 unaweka 3300 mha?

Simu ya 2016 utengeneze body kwa glass na metal/alluminium ya 2019 utumie plastic?

Sijazungumzia speaker, processor/chips, camera 16MP vs 13MP,
RAM 2GB vs 4GB,
selfie 5MP vs 8MP,

Ya 2016 ina fingerprint na ya 2019 haina

2016 ina support fast charga na ya 2019 haina

2016 ina 367 ppi ya 2019 271 ppi

ya 2016 ina Full HD ya 2019 haina, autofocus nk.

Na hata leo ukienda dukani bei ya A9 pro 2016 inaikimbiza mpaka Samsung A30 na sehemu nyingne hata A40

Umeona sasa boss nini nazungumzia.
 
reyzzap, Bila shaka umeizungumzia A10 hapa ndio inaongoza kwa kuuzwa kuliko simu zote, mpya na mkononi.

Kifupi simu imetembea vilivyo, nadhani kutokana na wengi kuimudu. Embu ingia mtandaoni tafuta A20 kupanda juu. Usome utakutana na matangazo mangapi. Kadri zinavyopada zinapingana na maelezo yako mkuu kwamba zinauzika sana mtandaoni. Leo hii maduka ya Tecno na Infinix hali imekuwa sio hali.sababu malaika wa peponi kashuma kuzimu kuchukua masalia.
 
Back
Top Bottom