Tish,
Mkuu ukiangalia vizuri hakuna sehemu nimeiponda hii simu na siwezi fanya hivyo sababu ni kweli ni nzuri kwa namna yake. Kitu kikubwa nilichozungumzia ni wao kuishusha kutoka Mid-range smartphone kuja kwenye low end.
Ni kweli tunasema hii simu ni nzuri, lakini kwa nini kwenye matoleo ya Samsung ya mwaka huu hii simu ndio ya mwisho kwa ubora? Unadhani J-series zingebaki hii simu ingekuwa ya mwisho? Hakika wangeacha J-series ishike nafasi ya low end kama mwanzo, hizi A-series zingemkimbiza hata zaidi ya hapo.
Ubora wa hii simu (kwa mtazamo binafsi) na uzuri wa hii simu (machoni kwa mtu) na bei yake ndogo ndio kumeifanya iuzike sana. Hilo halina ubishi, lakini pia hadhi ya hii simu kuwa ya mwisho kwenye matoleo yao kunaifanya watumiaji wengi wanaichoka wengine hata kuichukia mapema.
Hili nalo halina ubishi, Samsung A10 inaongoza kwa mauzo by shipment lakini inaongoza pia mauzo ya second hand hili tunashuhudia kwenye page za mauzo ya simu used hata hapa kwetu chukulia tu mfano Facebook, kupatana nk matangazo yake ni mengi zaidi ya simu nyingne specificaly Samsung, na watu wanauza kwa discount kubwa, na wengi kuonesha kama tatzo si hela ni simu anakuambia exchange allowed, why?
Kwahiyo kaka,
Hii simu sio mbaya, ila wao wenyewe wameishusha hadhi. Mfano kwanza kuifanya itumie LCD display wakati wenzake wanatumia Amoled, pili kuiwekea plastic cover wakati wenzake wanatumia glass, tatu position ya speaker iliyo kwa nyuma kitu kinachoifanya iwe na speaker quality ndogo kulinganisha na wenzake (simu siku hizi wanaepuka kuweka speaker kwa nyuma sababu zinakuwa nyembaba sana kwahiyo speaker nayo itakuwa nyembaba hivyo kupoteza ubora, matokeo yake wanaweka speaker kwa pembeni).
Ukizungumzia battery hii ina 3400 mAh kama sikosei na A70 ana 4500mha, umeona hilo gap? Kwanini nasema wameamua kuishusha hadhi wenyewe? Tunavyojua jinsi miaka inavyoenda basi unaboresha toleo la simu.
Kwanini Samsung,
A-series ya mwaka 2016 itumie Amoled display halafu ya 2019 miaka mitatu baade unarudi tena nyuma unatumia LCD teknolojia ya mwaka 1992?
Samsung A9 Pro 2016 ina 5000 mha ukiwa unaweza piga hata siku 3 data on na A10 ya 2019 unaweka 3300 mha?
Simu ya 2016 utengeneze body kwa glass na metal/alluminium ya 2019 utumie plastic?
Sijazungumzia speaker, processor/chips, camera 16MP vs 13MP,
RAM 2GB vs 4GB,
selfie 5MP vs 8MP,
Ya 2016 ina fingerprint na ya 2019 haina
2016 ina support fast charga na ya 2019 haina
2016 ina 367 ppi ya 2019 271 ppi
ya 2016 ina Full HD ya 2019 haina, autofocus nk.
Na hata leo ukienda dukani bei ya A9 pro 2016 inaikimbiza mpaka Samsung A30 na sehemu nyingne hata A40
Umeona sasa boss nini nazungumzia.