Sanamu ya Amani iliyowekwa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ina maana gani? Je, inauhusiano gani na utabiri wa siku za mwisho?

DANIELI 7​

Wanyama wanne wakubwa
1Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wa mfalme Belshaza wa Babuloni, Danieli aliota ndoto na kuona maono akiwa amelala kitandani mwake. Aliiandika ndoto yake hii:
2“Mimi Danieli niliona katika maono usiku, pepo nne toka pande zote za mbinguni zikiichafua bahari kuu. 3 Wanyama wakubwa wanne, wakainuka kutoka humo baharini, kila mmoja tofauti na mwenzake. 4 Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba, na alikuwa na mabawa kama ya tai. Nikiwa namwangalia, mabawa yake yalingolewa, naye akainuliwa na kusimama kwa miguu miwili kama binadamu. Kisha, akapewa akili ya binadamu.
 
Mbona hilo sanamu halina features zilizoelezwa kwenye bible...

Pia mnyama anayetajwa kwenye vifungu ulivyonukuu, anaonekana alikuwa ni mnyama anayewakilisha mambo fulani na wala si sanamu la mnyama....
 
Sanamu ya amani halafu inatisha hivyo....
 
Mbona hilo sanamu halina features zilizoelezwa kwenye bible...

Pia mnyama anayetajwa kwenye vifungu ulivyonukuu, anaonekana alikuwa ni mnyama anayewakilisha mambo fulani na wala si sanamu la mnyama....
Sifa ya The Beast mnyama aliyeongelewa ni anaviraka viraka vya viumbe wengine

Mabawa ya Tai
Mwili wa Chui
Mdomo wa Simba
Miguu ya Dubu.

2 Wakorintho 4:4 TKU " Mtawala wa dunia hii amezitia giza akili za wasioamini. Hawawezi kuona nuru ya Habari Njema; ujumbe juu ya uungu wa Kristo, taswira halisi ya Mungu. "
 
Huyo aliyeongelewa huko alikuwa hai, halikuwa sanamu...

Na usitarajie kuja kumuona huyo mnyama kwa macho, bali alitumika kama ishara kuelezea vitu/kitu/mtu ambaye atakuwa na tabia za muonekano huo ulioelezwa...
 
Huo ni uchambuzi wako , usi-command Kwa kusema usitarajie Yani kama unashurutisha

Haya ni mambo ya kiroho
 
Huyo aliyeongelewa huko alikuwa hai, halikuwa sanamu...

Na usitarajie kuja kumuona huyo mnyama kwa macho, bali alitumika kama ishara kuelezea vitu/kitu/mtu ambaye atakuwa na tabia za muonekano huo ulioelezwa...
Walokole akili zao kama vichaa.
 
Huo ni uchambuzi wako , usi-command Kwa kusema usitajie Yani kama unashurutisha

Haya ni mambo ya kiroho
Mambo ya kiroho yanaandikwa kwenye karatasi. Huu sasa ni wehu kiwango cha Dr Shika.
 
Walokole akili zao kama vichaa.
1 Wakorintho 1 : 20-25 " Yu wapi basi, mwenye hekima? Yu wapi basi, mwalimu wa sheria? Naye bingwa wa mabishano wa nyakati hizi yuko wapi? Mungu ameifanya hekima ya ulimwengu kuwa upumbavu.
Maana, kadiri ya hekima ya Mungu, watu hawawezi kumjua Mungu kwa njia ya hekima yao wenyewe. Badala yake, Mungu amependa kuwaokoa wale wanaoamini kwa njia ya kile ambacho wenye hekima wanakiona kuwa ni upumbavu, yaani ujumbe tunaohubiri. Wayahudi wanataka ishara, na Wagiriki wanatafuta hekima; lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa. Kwa Wayahudi jambo hili ni kikwazo, na kwa watu wa mataifa ni upumbavu; lakini kwa wale walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu. Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu kuliko nguvu za binadamu "
 
Akili yako haina akili, pole sana
 
Kwani mifupa kumbe iliubwa!? Mimi sikujua hilo. Kwa mujibu wa biology mifupa ni scientific process na siyo kuumbwa.
Nani aliiumba mifupa!?

Scientific process ipi?

Yaani wewe na hako kadigrii chako uchwara cha kata unataka kujitia unajua sana?

Haha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…