Sandaland: Makonda hana mamlaka ya kuingilia shughuli za chama cha soka, yeye ni ‘third party’

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwanasheria na Mwakilishi wa Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited, Cletus Tharcisiusy Nziku ametoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu iliyojitokeza juu ya ubora wa jezi za Timu ya Taifa, huku akisisitiza kuwa kauli zilizotolewa zikiponda ubora wa mavazi hayo si za kiungwana na hazipaswi kufumbiwa macho.

Amesema hakuna taratibu wala sheria zilizokiukwa na kwamba masuala ya viwango na ubora wa jezi yana mifumo yake rasmi ya kisheria na kikataba ya kuyashughulikia badala ya kuyajadili bila msingi.

Akiwasilisha vipengele vya kisheria, mwanasheria huyo amerejea Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 pamoja me Kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA Statutes), hasa Ibara ya 19(1).

Eleza kuwa vifungu hivyo vinataka kila shirikisho la soka nchini kuendesha na kusimamia shughuli zake za kibiashara, kiwekezaji na uendeshaji kwa uhuru kamili bila kuingiliwa au kupewa maelekezo na upande wa tatu (third party).

Ameongeza kuwa Waziri wa Michezo, Paul Makonda, ni upande wa tatu katika mkataba huo wa kibiashara ulilotiwa saini halali kati ya Kampuni ya Sandaland na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Soma: Sandaland Kuiburuza Mahakamani Wizara ya Michezo Kuhusu Jezi za Taifa Stars

Japo simpendi Bashite, lakini Waziri mwenye dhamana ana mamlakanna timu ya taifa. Sio vilabu; timu ya taifa. Yeye ndie anawasikisha bajeti ya michezo bungeni, ambayo ni pamoja na undeshaji wa timu ya taifa.
TFF inachukua hela serikalini kuendesha timu ya taifa. Pesa za nchi hizo, sio za GSM au Dewji.
 
Mwanasheria na Mwakilishi wa Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited, Cletus Tharcisiusy Nziku ametoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu iliyojitokeza juu ya ubora wa jezi za Timu ya Taifa, huku akisisitiza kuwa kauli zilizotolewa zikiponda ubora wa mavazi hayo si za kiungwana na hazipaswi kufumbiwa macho.

Amesema hakuna taratibu wala sheria zilizokiukwa na kwamba masuala ya viwango na ubora wa jezi yana mifumo yake rasmi ya kisheria na kikataba ya kuyashughulikia badala ya kuyajadili bila msingi.

Akiwasilisha vipengele vya kisheria, mwanasheria huyo amerejea Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 pamoja me Kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA Statutes), hasa Ibara ya 19(1).

Eleza kuwa vifungu hivyo vinataka kila shirikisho la soka nchini kuendesha na kusimamia shughuli zake za kibiashara, kiwekezaji na uendeshaji kwa uhuru kamili bila kuingiliwa au kupewa maelekezo na upande wa tatu (third party).

Ameongeza kuwa Waziri wa Michezo, Paul Makonda, ni upande wa tatu katika mkataba huo wa kibiashara ulilotiwa saini halali kati ya Kampuni ya Sandaland na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Soma: Sandaland Kuiburuza Mahakamani Wizara ya Michezo Kuhusu Jezi za Taifa Stars

Isije ikawa mshapeana mapesa mnatujazia mijadala tusau nchi yetu! hamueleweki kabisa muda wote matukio, nyie watu mtukome kama vipi hameni nchini kwetu mkabishanie huko
 
Japo simpendi Bashite, lakini Waziri mwenye dhamana ni bosi wa TFF, TFF ni taasisi ipo chini ya wizara yake. Anachokatazwa kuingilia ni kanuni na taratibu za mpira na mapato "mandatory" yale ya mpira.
Lakini mambo kama ya mikataba ya huduma au bidhaa, manunuzi au kama kuna upigaji maeneo hayo anahusika nayo.
Mkuu labda hujaelewa tu, FIFA wanaitambua TFF kama shirika huru la football Tanzania. TFF ndio wenye mamlaka kwa mujibu wa FIFA kusimamia mpira Tanzania na mambo yote ya kibiashara na kimkataba yanayohusu mpira wa miguu, serikali ni mdau tu na mshauri lakini sio msimamizi. Mambo ya mikataba kati ya TFF na makampuni ya uwekezaji hayawahusu Serikali hata kidogo.
 
1. Pesa ni ya Serikali, sio ya TFF peke yake.
TFF ina uhuru wa kiutawala (Article 19 FIFA), lakini jezi za Timu ya Taifa zinanunuliwa kwa kodi ya Watanzania. Kama Serikali ndio inayolipa maandalizi yote kuelekea AFCON 2027 ambayo Tanzania ni mwenyeji, ina haki ya kuuliza: "Mapato ya jezi yanaenda wapi?"

2. Uhuru sio Leseni ya Biashara ya Siri.
FIFA inasema TFF ichague mzabuni (Nike, Adidas) yenyewe. Sawa. Lakini FIFA haijasema mkataba usikaguliwe. Wizara haijafuta mkataba, imesema itaunda Kamati ya kuchunguza mkataba - hiyo ni uwajibikaji, sio kuingilia.

3. AFCON 2027 ni tofauti.
Tanzania sio mshiriki wa kawaida tu, ni MWENYEJI. Jezi itauzwa kwa mamilioni ya watalii. Kama mkataba wa sasa ni mbovu na nchi haipati faida, Serikali ikinyamaza ndio itakuwa imeshindwa kulinda maslahi ya Taifa.

4. FIFA haiwezi kutufungia kwa ukaguzi.
Adhabu 3 zilizotajwa hapo (kufungiwa, kukatwa fedha, kamati ya dharura) hutokea kama Waziri AMEFUTA uchaguzi wa TFF au AMEMVUA Rais wa TFF. Kuuliza "mkataba wa jezi umekula shilingi ngapi na nani kanufaika" sio kuingilia mpira, ni kuingilia matumizi ya fedha za umma.

TFF bado ina uhuru wa kuchagua jezi, lakini Serikali kama mfadhili mkuu ina haki ya kuhakikisha mkataba huo unamnufaisha Mtanzania, hasa kuelekea AFCON 2027
 
Waziri linap9kuja suala la timu ya taifa ( Acha vilabu) ni msimamizi wa timu husika. Kuna expenses zinatoka serikalini kugharamia timu husika. Huo mkataba sio wa Simba na Yanga. Ni mkataba wa timu ya taifa ya Tanzania ambayo inawndeshwa na pesa za walipa kodi. Waziri ana mandate kwenye hilo.
 
Watu wanashindwa kuelewa na kutofautisha kati ya vilabu na timu ya taifa. Timu ya taifa inamilikiwa na taifa, inagharamiwa na taifa, na waziri ni msimamizi wa timu husika maana ni ya taifa.

Timu inaendeshwa na kodi za watanzania; waziri ni "watch dog" wa timu, anaweza ingilia suala lolote linalohusu timu, isipokuwa masuala ya kikanuni na kiutaratibu za mpira za FIFA.
 
Mwanasheria na Mwakilishi wa Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited, Cletus Tharcisiusy Nziku ametoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu iliyojitokeza juu ya ubora wa jezi za Timu ya Taifa, huku akisisitiza kuwa kauli zilizotolewa zikiponda ubora wa mavazi hayo si za kiungwana na hazipaswi kufumbiwa macho.

Amesema hakuna taratibu wala sheria zilizokiukwa na kwamba masuala ya viwango na ubora wa jezi yana mifumo yake rasmi ya kisheria na kikataba ya kuyashughulikia badala ya kuyajadili bila msingi.

Akiwasilisha vipengele vya kisheria, mwanasheria huyo amerejea Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 pamoja me Kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA Statutes), hasa Ibara ya 19(1).

Eleza kuwa vifungu hivyo vinataka kila shirikisho la soka nchini kuendesha na kusimamia shughuli zake za kibiashara, kiwekezaji na uendeshaji kwa uhuru kamili bila kuingiliwa au kupewa maelekezo na upande wa tatu (third party).

Ameongeza kuwa Waziri wa Michezo, Paul Makonda, ni upande wa tatu katika mkataba huo wa kibiashara ulilotiwa saini halali kati ya Kampuni ya Sandaland na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Soma: Sandaland Kuiburuza Mahakamani Wizara ya Michezo Kuhusu Jezi za Taifa Stars

Attachments

  • GhfJRpEacAEgTRK.jpeg
    GhfJRpEacAEgTRK.jpeg
    19.3 KB · Views: 12
  • IMG-20260415-WA0001.jpg
    IMG-20260415-WA0001.jpg
    53.5 KB · Views: 12
Mkuu labda hujaelewa tu, FIFA wanaitambua TFF kama shirika huru la football Tanzania. TFF ndio wenye mamlaka kwa mujibu wa FIFA kusimamia mpira Tanzania na mambo yote ya kibiashara na kimkataba yanayohusu mpira wa miguu, serikali ni mdau tu na mshauri lakini sio msimamizi. Mambo ya mikataba kati ya TFF na makampuni ya uwekezaji hayawahusu Serikali hata kidogo.
Lakini Takukuru wanuwezo kisheiria kuchunguza mikataba ya Tff na ikikuta kuna rushwa imetumika Raisi na viongozi wenzake wa Tff wanaweza kufunguliwa kesi ya Uhujumu ushumi na rushwa na hao FIFA wasifanye lolote lile.
 
Waziri linap9kuja suala la timu ya taifa ( Acha vilabu) ni msimamizi wa timu husika. Kuna expenses zinatoka serikalini kugharamia timu husika. Huo mkataba sio wa Simba na Yanga. Ni mkataba wa timu ya taifa ya Tanzania ambayo inawndeshwa na pesa za walipa kodi. Waziri ana mandate kwenye hilo.
Kama ni hivyo inamaana wizara haijui kama TFF iliingia mkataba halali na Sandaland wa kutengeneza jezi za Timu za Taifa kwa ngazi zote? Maana kwa mujibu wa Makonda ni kama hatambua mkataba kati TFF na Sandaand ndio maana baada ya kuona jezi akashangaa?
 
Lakini Takukuru wanuwezo kisheiria kuchunguza mikataba ya Tff na ikikuta kuna rushwa imetumika Raisi na viongozi wenzake wa Tff wanaweza kufunguliwa kesi ya Uhujumu ushumi na rushwa na hao FIFA wasifanye lolote lile.
Hilo lipo wazi, ninachoshangaa mimi ni kwamba Wizara ilikuwa haijui kama kuna mkataba kati TFF na SANDALAND? Maana waziri mwenye dhamana anaonekana kushangaa na kukasirika baada ya kutambua Sandaland ndio anatengeeza jezi za timu ya taifa.
 
Back
Top Bottom