Sandaland: Makonda hana mamlaka ya kuingilia shughuli za chama cha soka, yeye ni ‘third party’

Sandaland: Makonda hana mamlaka ya kuingilia shughuli za chama cha soka, yeye ni ‘third party’

Mwanasheria na Mwakilishi wa Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited, Cletus Tharcisiusy Nziku ametoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu iliyojitokeza juu ya ubora wa jezi za Timu ya Taifa, huku akisisitiza kuwa kauli zilizotolewa zikiponda ubora wa mavazi hayo si za kiungwana na hazipaswi kufumbiwa macho.

Amesema hakuna taratibu wala sheria zilizokiukwa na kwamba masuala ya viwango na ubora wa jezi yana mifumo yake rasmi ya kisheria na kikataba ya kuyashughulikia badala ya kuyajadili bila msingi.

Akiwasilisha vipengele vya kisheria, mwanasheria huyo amerejea Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 pamoja me Kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA Statutes), hasa Ibara ya 19(1).

Eleza kuwa vifungu hivyo vinataka kila shirikisho la soka nchini kuendesha na kusimamia shughuli zake za kibiashara, kiwekezaji na uendeshaji kwa uhuru kamili bila kuingiliwa au kupewa maelekezo na upande wa tatu (third party).

Ameongeza kuwa Waziri wa Michezo, Paul Makonda, ni upande wa tatu katika mkataba huo wa kibiashara ulilotiwa saini halali kati ya Kampuni ya Sandaland na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Soma: Sandaland Kuiburuza Mahakamani Wizara ya Michezo Kuhusu Jezi za Taifa Stars

Lengo la hawa jamaa nikututoa kwenye mambo ya msingi ni upepo tuu huu
 
Watu wanashindwa kuelewa na kutofautisha kati ya vilabu na timu ya taifa. Timu ya taifa inamililiwa na taifa, inagharamiwa na taifa, na waziri ni msimamizi wa timu husika maana ni ya taifa.

Timu inaendeshwa na kodi za watanzania; waziri ni "watch dog" wa timu, anaweza ingilia suala lolote linalohusu timu, isipokuwa masuala ya kikanuni na kiutaratibu za mpira za FIFA.
Chivundu:
Umeweka vema mkuu
 
Hilo lipo wazi, ninachoshangaa mimi ni kwamba Wizara ilikuwa haijui kama kuna mkataba kati TFF na SANDALAND? Maana waziri mwenye dhamana anaonekana kushangaa na kukasirika baada ya kutambua Sandaland ndio anatengeeza jezi za timu ya taifa.
Kweli ni fedhea kama nchi kukubali jezi ya Taifa itengenezwe na kampuni za hazi ya chini, Taifa Stars imeshakua Timu kubwa kwasasa na inashiriki Mashindano makubwa kwanini Jezi zetu zisitengenezwe na Kampuni kubwa mfano Adidas, Nike, Puma?
 
Tff na mashirikisho mengine yote ya michezo kama pete, kikapu n.k yapo chini ya wizara ya michezo na utamaduni
Tff,TOC ni tofauti kabisa na michezo mingine hiyo michezo haitaki kabisa serikali za ndani kuingilia masuala yake ndio maana ni mashirikisho ya nguvu sana duniani.Ukizingua wanakupa ban bila shaka ulifuatilia ule mchakato wa uchaguzi wa TOC pamoja na bwana mmoja kuingilia lakini kafeli na huku TFF atafeli labda acheze figisu za ndani kwenye chaguzi za tff kuweka mtu wake.
 
anayeenda kupewa hiyo tenda ni arabs, ni kipi hamjakielewa bado khs kinachoendelea nchini? kama wewe siyo muslim arabs they put you out of business, kwanza waangalie sana wataishia kufwatwa na tra na kufungwa ...
Huu ndiyo ''utamu'' wa kukubali kuongozwa na wahuni. Hawana mpaka na kila mtu anafikiwa kwa wakati wake. Bila kuungana na kuondoa hawa wahuni hakuna kupumzika.
 
anayeenda kupewa hiyo tenda ni arabs, ni kipi hamjakielewa bado khs kinachoendelea nchini? kama wewe siyo muslim arabs they put you out of business, kwanza waangalie sana wataishia kufwatwa na tra na kufungwa ...
Kwani makomda ni muislamu mkubwa acha chuki binafsi kiongozi. Haya tupatie na ushahidi basi na ututajie ni muarabu gani anapewa hio tenda kama wewe umeelewa
 
Mm nachoshangaa n kuona naibu Waziri ameshirikishwa ila ofisi ya waziri haijashirikishwa 😂

Anyway, kiwake tuu, watajuana wnyw huko.
 
1. Pesa ni ya Serikali, sio ya TFF peke yake.
TFF ina uhuru wa kiutawala (Article 19 FIFA), lakini jezi za Timu ya Taifa zinanunuliwa kwa kodi ya Watanzania. Kama Serikali ndio inayolipa maandalizi yote kuelekea AFCON 2027 ambayo Tanzania ni mwenyeji, ina haki ya kuuliza: "Mapato ya jezi yanaenda wapi?"

2. Uhuru sio Leseni ya Biashara ya Siri.
FIFA inasema TFF ichague mzabuni (Nike, Adidas) yenyewe. Sawa. Lakini FIFA haijasema mkataba usikaguliwe. Wizara haijafuta mkataba, imesema itaunda Kamati ya kuchunguza mkataba - hiyo ni uwajibikaji, sio kuingilia.

3. AFCON 2027 ni tofauti.
Tanzania sio mshiriki wa kawaida tu, ni MWENYEJI. Jezi itauzwa kwa mamilioni ya watalii. Kama mkataba wa sasa ni mbovu na nchi haipati faida, Serikali ikinyamaza ndio itakuwa imeshindwa kulinda maslahi ya Taifa.

4. FIFA haiwezi kutufungia kwa ukaguzi.
Adhabu 3 zilizotajwa hapo (kufungiwa, kukatwa fedha, kamati ya dharura) hutokea kama Waziri AMEFUTA uchaguzi wa TFF au AMEMVUA Rais wa TFF. Kuuliza "mkataba wa jezi umekula shilingi ngapi na nani kanufaika" sio kuingilia mpira, ni kuingilia matumizi ya fedha za umma.

TFF bado ina uhuru wa kuchagua jezi, lakini Serikali kama mfadhili mkuu ina haki ya kuhakikisha mkataba huo unamnufaisha Mtanzania, hasa kuelekea AFCON 2027
Ajabu sana! Jezi zimeshatengenezwa, ndo mnaanza kubweka barabarani!
 
Kweli ni fedhea kama nchi kukubali jezi ya Taifa itengenezwe na kampuni za hazi ya chini, Taifa Stars imeshakua Timu kubwa kwasasa na inashiriki Mashindano makubwa kwanini Jezi zetu zisitengenezwe na Kampuni kubwa mfano Adidas, Nike, Puma?
Hazi= hadhi
 
Back
Top Bottom