Sandaland: Makonda hana mamlaka ya kuingilia shughuli za chama cha soka, yeye ni ‘third party’

Sandaland: Makonda hana mamlaka ya kuingilia shughuli za chama cha soka, yeye ni ‘third party’

Waziri linap9kuja suala la timu ya taifa ( Acha vilabu) ni msimamizi wa timu husika. Kuna expenses zinatoka serikalini kugharamia timu husika. Huo mkataba sio wa Simba na Yanga. Ni mkataba wa timu ya taifa ya Tanzania ambayo inawndeshwa na pesa za walipa kodi. Waziri ana mandate kwenye hilo.
FIFA haimtambui Makonda inaitambua TFF huyo dogo kakosa percent kwenye hilo dili la jezi ndio maana analeta gubu
 
Mwanasheria na Mwakilishi wa Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited, Cletus Tharcisiusy Nziku ametoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu iliyojitokeza juu ya ubora wa jezi za Timu ya Taifa, huku akisisitiza kuwa kauli zilizotolewa zikiponda ubora wa mavazi hayo si za kiungwana na hazipaswi kufumbiwa macho.

Amesema hakuna taratibu wala sheria zilizokiukwa na kwamba masuala ya viwango na ubora wa jezi yana mifumo yake rasmi ya kisheria na kikataba ya kuyashughulikia badala ya kuyajadili bila msingi.

Akiwasilisha vipengele vya kisheria, mwanasheria huyo amerejea Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 pamoja me Kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA Statutes), hasa Ibara ya 19(1).

Eleza kuwa vifungu hivyo vinataka kila shirikisho la soka nchini kuendesha na kusimamia shughuli zake za kibiashara, kiwekezaji na uendeshaji kwa uhuru kamili bila kuingiliwa au kupewa maelekezo na upande wa tatu (third party).

Ameongeza kuwa Waziri wa Michezo, Paul Makonda, ni upande wa tatu katika mkataba huo wa kibiashara ulilotiwa saini halali kati ya Kampuni ya Sandaland na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Soma: Sandaland Kuiburuza Mahakamani Wizara ya Michezo Kuhusu Jezi za Taifa Stars

Bashite amemdiss mwanasheria kuhusu KOKOTO.
 
Tff ya Kalia ina madudu mengi sana uchunguzi ukifanyika tutaona mengi mno..
 
Back
Top Bottom