Mkuu siku hizi migodi yote midogo ina uongozi sidhani kama hicho unachokiongelea kinawezekana tena kwa urahisi huo. Em fikiria mfano kitalu kina mwenye leseni, ndani ya eneo la leseni kuna watu wenye maduara(kama mwenye leseni hajaamua kuchimba mwenyewe na kuendesha kwa mwendo wa share 63 kwa 37). Na kwa kila duara linakuwa na mmiliki na vibarua wake na mlinzi(yuko answerable kwa mwenye leseni) na inspector(kukagua structure ya shimo na mali iliyomo) huyu ana report kwa wote, mwenye duara na mwenye kitalu.
So niambie kwa mlolongo huo wote ni vipi utamuua mwenzio isijulikane, kwanza kwa vibarua wenzio ulionao shimoni pili kwa mwenye duara tatu kwa inspector anaepaswa kuwa anazama shimoni mara kwa mara kukagua na mwisho mwenye leseni ambae ndo yuko answerable kwa serikali.
Unahisi kweli unachokiwaza kinaweza kuwa rahisi kiasi hicho! Labda sio kwa awamu hii ilivorekebisha mambo aisee!
Wizi hua unafanyika ila mara nyingi ni majambazi wanakuja na siraha kabisa wanawateka kitu ambacho sioni kikitokea Merarani. Ni sawa na kwenda kuivamia kambi ya jeshi