Saniniu Laizer aahidi kupata jiwe kubwa zaidi la Tanzanite na kuahidi kuiuzia Serikali kwa uzalendo

Saniniu Laizer aahidi kupata jiwe kubwa zaidi la Tanzanite na kuahidi kuiuzia Serikali kwa uzalendo

johnthebaptist,

Hii ni habari mbaya kwa vyama pinzani - hawakutaka mafanikio kwenye madini (ukuta waliupinga kabla hujajengwa na baada ya kujengwa waliubeza)
Muulize mbona kwenye migodi ya dhahabu,almasi,ruby,saphire mbona hawajajenga ukuta?au yale sio madini
 
Unachowaza hakipo hivyo ile migodi ya mererani ni mirefu zaidi ya mita 200 kwenda chini na njia sio mnyooko eti ukichungulia utaona mwisho.

Hiyo mle kuna migodi hadi mingine ina mitobozano chini kwa chini (kunawekwa grill kama lile la dirishani)hivyo pale juu mwanzo mwa shimo kuna kuwa ma kijumba(kama unavyoona choo)hivyo wale wazamaji wanaweza zama wakakaa hata siku 3 hadi 5 humo humo chini na kila kitu humo humo kama ni kitu kama sigara au bangi au batery za tochi, maji ya kunywa au balbu kama imeungua unamtuma nyoka (nyoka ni wale vijana wadogo dogo) hivyo kinachoendelea huko chini hao walinzi hapo juu ni ngumu sana kujua
Mita 200 ni mgodi ambao bado upo juu sana,mikanda ya mawe mingi ni meter 500 au 700 ndio uanze kupata madini..opec kuna migodi imeenda mita 2500
 
Ndo uzuri wa madini ukishauotea mwamba kila sururu na tindo unayopiga inatoka na mali. Safi sana Laizer piga kazi, pata pesa jenga nchi.
Chorongo zinaweza kuzama hata tatu mkapiga moto mkakuta ni korongo hewa halina madini,na huo mkanda wa laizer unaweza kukata au kuchukuliwa na mgodi wa pembeni...jirani yake angekua sunda ungesikia keshamfukuzia na kumpita na kuchukua njia
 
leo nilikuwa kwenye training moja hivi na kulikuwa na mtu mmoja mkubwa serikalini alikuwa anafanya presentation. alisema kabla ya ukuta mawe ukubwa wa aina hiyo yalikuwa yanapatikana ila yalikuwa yanauzwa kinyemela kwa kutoroshwa.
 
Mtu mwenye $5M liquid Cash mnamuita mdogo, ila mfanyabiashara mwenye $15000 anaitwa mfanyabiashara wa kati na kila siku TRA wapo naye
Siasa za hii nchi bhana.
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Huyu jamaa anajabali analikwangua kidogo kidogo. Ndyo maana mawe anayotoa yanastructure inayofanana. Huyu akibanwa anaweza kuja na jiwe la kubebwa na fuso.

Mtu anasbilion 7 anasema anatarajia kujenga mall unadhani mall ni kitu ya mchezo?
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Sasa hiyo sifa kuna mijitu imeenda tokea wadogo mgodini nakuzeekea huko lakini ata gram kumi hajawai pata.
 
Mtu mwenye $5M liquid Cash mnamuita mdogo, ila mfanyabiashara mwenye $15000 anaitwa mfanyabiashara wa kati na kila siku TRA wapo naye
Siasa za hii nchi bhana.
Tofautisha aina ya biashara na mtaji unatakiwa.

BTW, Huyu sio mfanyabiashara mdogo ni mchimbaji mdogo kulingana na Capital alowekeza kuchimba
 
baada ya ukuta ameshindwa kuyatorosha madini inabidi ayasalimishe hayo yalichimbwa tangu zamani yalihifadhiwa shimoni sasa jinsi ya kuyapitisha ndo mtihani so lazima ayasalimishe,
Miladi AYO anavyoshoboka na pesa ndo amekuwa ripota wake,hivi kwann watu wanashoboka na pesa
 
mi nawashauri tu serikali inavyohifadhi tanzanite -
angalia --ITALIAN JOB MOVIE
 
Me mwenyewe nineshangaa. Huwezi mwita Bilionea kama huyo mchimbaji mdogo. Kuna wachimbaji ambao miaka yote wanachimba kwa makarai, makoreo na machujio very locally na hawajawahi pata hata mil 20, sasa hao ni sawa na huyu jamaa? Je hao wengine wa kati na juu wote wanenpiga gap huyu Laizer?
Ungejiuliza kwanza mchimbaji mkubwa anafananaje......
hayo ni ma multi billionaire companies...
yenye mitaji mikubwa investment capital kubwa....
equipment za kutosha....
sio hiyo pinnut ya Laizer tudola tuchache unataka kumuita mchimbaji mkubwa haiwezekani....
jifunzeni kufanya comparison
 
Mwanzo nilimwelewa sana, ila sasa nahisi kunakitu hakipo sawa. Yani kila siku awe anapata yeyetu!! kwamba anaundugu nayo au mwenzetu anapua zilizoboreshwa so ni mwendo wa kunusa tu lipo uku or lipo kule!!? Kunanamna sio bule
 
Money laundering kwa maslahi ya watu fulani. Hamjashtuka tu.

Watu bwana!! Hivi mnajua maana ya money laundering? ML processing mnaijua? Sasa yeye anachimba madini kisha kuyauza, how is money that laundered?
Hebu mkajifunze vizuri kuhusu ML ndio mje hapa [emoji3525][emoji3525]
 
Watu bwana!! Hivi mnajua maana ya money laundering? ML processing mnaijua? Sasa yeye anachimba madini kisha kuyauza, how is money that laundered?
Hebu mkajifunze vizuri kuhusu ML ndio mje hapa [emoji3525][emoji3525]
Kuna vitu bavicha wanaongea inakufanya uamini wao vichwa vyao vipo kutenganisha masikio tu
 
Mita 200 ni mgodi ambao bado upo juu sana,mikanda ya mawe mingi ni meter 500 au 700 ndio uanze kupata madini..opec kuna migodi imeenda mita 2500
Nimempa mifano tuu hata kule block D nako imeenda chini sana kuliko hiyo ya lizer anayosema
 
Back
Top Bottom