Unachowaza hakipo hivyo ile migodi ya mererani ni mirefu zaidi ya mita 200 kwenda chini na njia sio mnyooko eti ukichungulia utaona mwisho.
Hiyo mle kuna migodi hadi mingine ina mitobozano chini kwa chini (kunawekwa grill kama lile la dirishani)hivyo pale juu mwanzo mwa shimo kuna kuwa ma kijumba(kama unavyoona choo)hivyo wale wazamaji wanaweza zama wakakaa hata siku 3 hadi 5 humo humo chini na kila kitu humo humo kama ni kitu kama sigara au bangi au batery za tochi, maji ya kunywa au balbu kama imeungua unamtuma nyoka (nyoka ni wale vijana wadogo dogo) hivyo kinachoendelea huko chini hao walinzi hapo juu ni ngumu sana kujua