Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Nimeiangalia video ya Mheshimiwa mbunge wa Arumeru namna alivyopanda juu ya meza yake na kusimama miguu kichwa chini. Siwezi kusema sikushangazwa sana kama wengi walioiona video hiyo kwa mara ya kwanza. Wanaonekana wabunge waliokaa jirani yake wanashangaa wakicheka kwa kustaajabishwa. Hata sauti ya kucheza ya Mheshimiwa Spika akimkataza mbunge huyo wa Arumeru asifanye kituko hicho, na yenyewe ni ya kucheka akiwa anashangaa haamini kile kinachokwenda kufanyika ndani ya ukumbi wa bunge.
Inaonekana mheshimiwa Mbunge amenyimwa kule kukua kisawasawa kabla hajapewa nafasi ya kuwa mbunge, ni kama vile kuna hatua maishani mwake imerukwa na akapewa ubunge kabla hajaipitia hiyo hatua. Bungeni ameingia mtu mzima wa umbo lakini ni mtoto wa kimaamuzi sawa sawa na mahali pale. Amefanya mpaka wataalam wa kutengeneza vibonzo wakitengeneza kimoja akiwa amesimama miguu juu kichwani pembeni ya viti vya Samia na Mzee Greenburg wa Royal Tour, eti wanamtazama wakimshangaa.
Naliona kosa linalofanyika mara kwa mara wakati wa teuzi za wagombea ubunge wa vyama vya siasa. Anachaguliwa kugombea aina ya mtu anayependwa na uongozi wa juu lakini hakubaliki miongoni mwa wajumbe wanaoteua. Anayeteuliwa mgombea asiyekubalika au asiyeenda sambamba na hulka za wapiga kura wanaomchagua!. Wajumbe wanaishia kupiga makofi ya kinafiki siku wanapotajiwa kuwa ndio anayekwenda kuwawakilisha katika uchaguzi mkuu na baadae bungeni.
Mbunge anayecheza sarakasi ndani ya ukumbi wa bunge sio tu ni aibu ya CCM bali pia ni aibu ya mifumo yetu ya kisiasa. Kwamba anakuwepo mgombea anayependwa na kukubalika miongoni mwa wapiga kura na pia anakuwepo yule anayekubalika miongoni mwa wanaokaa meza kuu. Ni hapa unapomuangalia mbunge huyu licha ya kuwasilisha hoja za msingi kwa mheshimiwa Spika lakini bado anazo hulka za ujana, hulka za mtu ambaye hajakomaa sawa sawa kichwani mwake. Bado mwili wake unachemkwa na damu ya ujana.
Hapa lipo la kujifunza na kulifanyia kazi. Kwamba sauti ya wengi siku zote huwakilisha maoni sahihi ya watu wa sehemu husika. Kwamba maoni na vionjo vya watu ni vya kuheshimiwa na sio kuwapelekea aina ya mbunge kwa kutazama vigezo vya wachache wanaokaa meza kuu.
Na ni hapa tunaweza kuuona uhalali wa malalamiko ya baadhi ya watanzania wanaposema kwamba uchaguzi wa 2020 hawana kabisa imani nao, wakimaaanisha rafu za kisiasa zilikuwa ni nyingi na za wazi. Sijawahi kukaa na watu wa jimbo lililomchagua mheshimiwa huyu kwenda bungeni, lakini nahisi kuna ile hali ya unyonge wa kuona liwalo na liwe kama wameamua kwenda na huyu kijana kama mbunge kwa miaka hii mitano inayomalizika 2025.