Sarakasi za Mbunge kijana na somo kwa vyama vya siasa wakati wa uteuzi majina ya wabunge

Imekuwa ni kawaida kwa vyama katika baadhi ya maeneo kuchagua watu wasio na weledi. Wakati mwingine waliokosa difa kabisa.

Tatizo hili hijitokeza pia hata kwa nafasi za wagombea wenza. Vyama vingi hufanya makosa katika hili
 
Kumuita mbunge kijana,wakati ni wa mwaka 72,sijui inakuaje?

Nadhani ana miaka 50 sasa.

Inaonyesha ni mtu wa mazoezi sana huyu mtu hasa ukizingatia umri.
 
Hizi ni athari za wabunge
Yah. Uchafuzi ule ungekuwa uchaguzi huru na wa haki, mbunge wa mbeya mjini angekuwa Sugu, zitto angekuwa bungeni, Mdee angekuwa mbunge halali wa kuchaguliwa, kina Mbowe, Heche, Mbatia etc wangekuwamo. Na bunge lingekuwa na heshima yake. Hakungekuwa na 'covid19', sarakasi wala kulia bungeni.

Maana pale pangekuwa na mapambano yenye tija, ya hoja dhidi ya hoja.

Hawa wanafiki wengine kina gambo hawangekuwamo. Lissu na Lema hawangekuwa ubelgiji/Canada, tungekuwa tunasikilizia nyundo zao huo Dodoma.
 
Aibu kwa taifa.
 
Umeandika meengi lakini na wewe unaongozwa na mihemko binafsi na imepelekea hata kutotambua yule mbunge hakuwa wa Arumeru bali mbunge wa Mbulu....
Sarakasi ya kujiaibisha ime-overshadow kile alichokuwa anakizungumzia, ndiyo pale unapotumia njia za kipuuzi kuwasilisha jambo la maana na kusababisha huo upuuzi ukalifunika hilo jambo.

Mleta uzi yuko sahihi kabisa kwa namna alivyolifafanua tukio zima.
 
... kama jiwe alivyokuwa akipiga pushups kwenye majukwaa. Utimamu wa mwili wa mwanadamu ni fumbo.
Naamini amekuelewa, big up GT kwa jibu mujarabu kabisa.
 
Hakika mkuu, tutashuhudia mengi, tuombe uzima tu,
 
Aaaaagh picha iko wapi sasa,wengine tupo Kandahar tuone MPalievunja records za mjengoni
 
Hakika huyu munger anaakili sana amekuwa mbunifu wa hali ya just sana ni miongoni mwa wabunge wachache wa chama cha kijani (green party) wanaojitambua na wenye ability ya kiwango cha juu katika kupeleka ujumbe HONGERA SANA MBUNGE FLATEI MASSAY KAZI NZURI
 
Aibu kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…