Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Sijui ni kwamba watu wameokoka sana hata sielewi kabisa.Miaka ya nyuma mkienda kwenye mkesha ama sikukuu ilikuwa ni lazima ushuhudie ngumi za wanaume zikipigwa katikati ya senta .

Haikuwa sio ajabu kuona wala kusikia kuwa akina J n p jana walizipiga kwenye mkesha.Ni miaka sasa imepita bila kusikia wala kuona ngumi zikipigwa asee hadi najiuliza ama tiyari dunia imegeuka kuwa paradiso?

Leo hii hata ukienda club hadi unarudi hakuna ugomvi wowote utakao ushuhudia asee.Zamani hata mkesha wa disco wa darasa la saba tu tulikuwa tunashuhudia ngumi zikipigwa sana tu.Tena ilikuwa marufu kidato cha nne kukesha kwenye mahafari yao lakini kwa sasa imekuwa kawaida tu madogo wanakesha na walimu wana amani tele.

Kipindi hicho hakuna mwalimu yeyote angeweza kubali kurusu eti tukeshe kwenye mkesha wa kidato cha nne.Pamoja na kwamba sisi tulikuwa tunaanza disco saa4 asbh hadi saa12 jioni lakini bado ngumi zilipigwa tu.

Enzi hizo kulikuwa na mbabe wa mtaa mzima au hata kijiji kizima anafahamika kabisa kuwa flani ndo mbabe wa huu mtaa/kijiji. sasa hivi ni hamna. Nimemiss zana ubabe wa enzi hizo.

Baba mdogo aliwapiga migambo hadi wakapoteana na hapo walikuwa wanne leo hii mgambo mmoja tu anakuijia na anaenda kakupiga jeck njia yote na unatii au yeye anakuwa na baiskeli anakuswaga kama ng'ombe na unakubali tu.Kunakipindi mgambo na police mmoja mwenye siraha walikuja kukamata waunza gongo kipigo walichopata hawakurudia kuja tena kukamata walio bahatika kutokupigwa ni hawa walikuwa na police kwenye kukamata lakini wale waliojitenga wakiwa na marungu tu walipigika vibaya mno vile hata simu hazikuwepo walipigwa mno.

DJ alikuwa akibadilisha wimbo bila mpangilio lazima kipigo kimuhusu na ma DJ wa kipindi hicho walikuwa wababe. Kuna mkesha mmoja zilipigwa kanisani padri anaendelea na ubatizo kisa jamaa mmoja alijamba tu...
tukiwa tunaimba kwaya mara wazamiaji wa kwenye mkesha wakanzisha huko ikabidi ibada isimame.. jenerata ikazimwa makusudi na wababe kukawa giza zilipigwa ovyo ovyo yani unatembea huku unarusha ngumi kujiokoa wachache walikuwa na tochi walisaidia japo nao walikuwa wanamulika watoke mbio hakuna namna..

Finaly Mkong'oto nilioupata mimi kwa kuanzisha vanga ilikuwa mwaka 2011 mr chocolate(Bob junio) walikuwa wamekuja na bonge la nyau mahala fulani kufanya show. kwnye mida ya usiku kama saa7 wakatoka club likabaki la manyani sasa........ nilipigwa na jamaa niliyedhani na mu mudu asee masela wangu wote wakaniachia msala siku 3 uso umevimba sitoki nje masela wananiuguza japo walinikimbia asee.

MAMBO YANABADIRIKA SANA
 
Siku izi hata kwenye sikukuuu za mwaka mpya baruti/ fataki madogo hawafanyi..

Kuchoma vibanda vya nyasi/ kuchoma matairi barabarani hazifanyiki...hope ELIMU imeongezekaa😅😅😅

Tulikua na crew yetu jioni mnatembea mmoja wetu ana piga kikumbo mtu then jamaa akimind mnampiga KARATE balaaa

Enzi izo mna chokoza watu ili muwapigee....nakumbuka Kuna siku mbabe mmoja alienda na crue akasema chukueni barafu/ ice cream...watu Kama 20 then akasema kila mtu ajilipie...muuza barafu/ ice cream akachezea kichapo zamani kulikua na ubabe sanaa
 
Umenikumbusha mbali sana , hata siku za x-mass mkono ulikuwa unaopigwa hadi sio poa , sisi home tulikuwa men 12 aisee tulikuwa tunapiga mkono mtu akizingua kata nzima walikuwa wanaelewa , unakuta tena zilikuwa fujo zinaanzia kwenye mpira au madamu kuna siku ndugu yetu anaenda skuli asubuhi jamaa anakuta wanamsubili ikabidi arudi home , tukaamsha wote aisee zilitembea pale jamaa walikalishwa ikabidi wakimbie .
 
Wakat huo hadi nilijihis kama tupo china maana kila mmoja lazima ujue kupigana,nilkuwaga mwoga sana lakin kuna huyo mjomba wangu alikuwa anapenda sana kunitest kila nikikutana na wa rika langu mpaka uoga uliniisha

Nakumbuka wakat fulani tukiwa wadogo tukawa tumeenda ukerewe likizo ya mwez wa 12,siku ya sikukuu nilishangaa kuona sentani wababa wazima wamevua mashati wanapigana mpaka wanatoka midamu tena wengi wengi,hakika niliogopa sana nilikuwa sijawah ona kitu kama hicho

Kuna kabila moja la wazinza hawa ndo walikuwa wananichekesha,kwanza hawa jamaa ni wachache afu wakiwa sehemu moja karibia wote wanakuwa kama ndugu maana huwa wanaoana sana,ikitokea kuna mchezo wa mpira wa miguu enzi hzo mpira auishi tena kipindi hicho walikuwa wanacheza watu wazima tena wana familia,basi ghafla utaona wanashikana wachezaji kwa wachezaji mashabiki nao wanaingia mara unaona jamaa anamrukia shemeji yake au wakwe kwa wakwe wanakwidana yaan ni full valangati au mtu na mjomba wake wanazikunja

Haya mambo yameisha baada ya watu kupata mwanga na kuwa na tamaa ya pesa ya kutaka kulipwa unapompiga,ataanzisha kesi na utamlipa kwa kuuza mali zako
 
Kweli umeonaa eee Kuna watu wachokozi na wagomvi mnoooo 🤣🤣

Uzao unanisumulia sehemu hasa tiktok ndio balaa, hadi vukundi vya kigangwe vya wanawake na viwanaume kuswutana, kutukananwa, kupelekana polisi kila vya kiugomvi huko tena live na wakijishana..

Siku moja niliingia nikakumbuka ile misuto ya barabarani watu kuviziana wakati wa kurudi home, inatangazwa na akina mie tunadanganya ili tusifatwe na mkoko au lichelewe au dreva wa home ataganda hadi tutoke kitaaa.. bali tutembee kurudi home tukaangalie ngumi.

Maisha hakika ya na badilika, sijui kama misuto bado ipo au laaaaa
 
Uzao unanisumulia sehemu hasa tiktok ndio balaa, hadi vukundi vya kigangwe vya wanawake na viwanaume kuswutana, kutukananwa, kupelekana polisi kila vya kiugomvi huko tena live na wakijishana..

Siku moja niliingia nikakumbuka ile misuto ya barabarani watu kuviziana wakati wa kurudi home, inatangazwa na akina mie tunadanganya ili tusifatwe na mkoko au lichelewe au dreva wa home ataganda hadi tutoke kitaaa.. bali tutembee kurudi home tukaangalie ngumi.

Maisha hakika ya na badilika, sijui kama misuto bado ipo au laaaaa
Zama zimebadilika...zamani mpaka wizi kwa kutumia Jiwe "FATUMA" vijana wa 2005's hawawezi kuelewaa 🤣🤣
 
Kuna jamaa(mbabe) alikuwa anachukua mke wa mshkaji.

Yule mshkaji akamwambia yule mbabe aachane na mke wake jamaa haskii

Yule mbabe akawa anatamba tu,siku moja akaenda mpaka kwa jamaa akawa anamtambia kwamba hamuachi mkewe na hafanywi chochote.

Yule mshikaj alivyoona dharau zimezidi akaingia ndani akatoka na mkuki akamchomeka mbabe kifuani,mbabe r.i.p
 
Back
Top Bottom