Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

😄😄😄 na unakuta ni watu wazima kabisa wana battle na wadada huwa nashangaa sana😁😁😁

Hii mtandao naamini hao lazima kuna wanao umia mioyo na kuharibu maisha yao kwa hayo kisaikolojia

Huku tu kuna watu wanahatafjga wakiyapata kama hawana mioyo inakuwa balaaa wakilalamika

Sio nzuri ila ndio maisha hayo
 
Umenikumbusha mbali sana , hata siku za x-mass mkono ulikuwa unaopigwa hadi sio poa , sisi home tulikuwa men 12 aisee tulikuwa tunapiga mkono mtu akizingua kata nzima walikuwa wanaelewa , unakuta tena zilikuwa fujo zinaanzia kwenye mpira au madamu kuna siku ndugu yetu anaenda skuli asubuhi jamaa anakuta wanamsubili ikabidi arudi home , tukaamsha wote aisee zilitembea pale jamaa walikalishwa ikabidi wakimbie .
Mlipigwa sana naikumbuka hio siku🤣
 
Sijui ni kwamba watu wameokoka sana hata sielewi kabisa.Miaka ya nyuma mkienda kwenye mkesha ama sikukuu ilikuwa ni lazima ushuhudie ngumi za wanaume zikipigwa katikati ya senta .

Haikuwa sio ajabu kuona wala kusikia kuwa akina J n p jana walizipiga kwenye mkesha.Ni miaka sasa imepita bila kusikia wala kuona ngumi zikipigwa asee hadi najiuliza ama tiyari dunia imegeuka kuwa paradiso?

Leo hii hata ukienda club hadi unarudi hakuna ugomvi wowote utakao ushuhudia asee.Zamani hata mkesha wa disco wa darasa la saba tu tulikuwa tunashuhudia ngumi zikipigwa sana tu.Tena ilikuwa marufu kidato cha nne kukesha kwenye mahafari yao lakini kwa sasa imekuwa kawaida tu madogo wanakesha na walimu wana amani tele.

Kipindi hicho hakuna mwalimu yeyote angeweza kubali kurusu eti tukeshe kwenye mkesha wa kidato cha nne.Pamoja na kwamba sisi tulikuwa tunaanza disco saa4 asbh hadi saa12 jioni lakini bado ngumi zilipigwa tu.

Enzi hizo kulikuwa na mbabe wa mtaa mzima au hata kijiji kizima anafahamika kabisa kuwa flani ndo mbabe wa huu mtaa/kijiji. sasa hivi ni hamna. Nimemiss zana ubabe wa enzi hizo.

Baba mdogo aliwapiga migambo hadi wakapoteana na hapo walikuwa wanne leo hii mgambo mmoja tu anakuijia na anaenda kakupiga jeck njia yote na unatii au yeye anakuwa na baiskeli anakuswaga kama ng'ombe na unakubali tu.Kunakipindi mgambo na police mmoja mwenye siraha walikuja kukamata waunza gongo kipigo walichopata hawakurudia kuja tena kukamata walio bahatika kutokupigwa ni hawa walikuwa na police kwenye kukamata lakini wale waliojitenga wakiwa na marungu tu walipigika vibaya mno vile hata simu hazikuwepo walipigwa mno.

DJ alikuwa akibadilisha wimbo bila mpangilio lazima kipigo kimuhusu na ma DJ wa kipindi hicho walikuwa wababe. Kuna mkesha mmoja zilipigwa kanisani padri anaendelea na ubatizo kisa jamaa mmoja alijamba tu...
tukiwa tunaimba kwaya mara wazamiaji wa kwenye mkesha wakanzisha huko ikabidi ibada isimame.. jenerata ikazimwa makusudi na wababe kukawa giza zilipigwa ovyo ovyo yani unatembea huku unarusha ngumi kujiokoa wachache walikuwa na tochi walisaidia japo nao walikuwa wanamulika watoke mbio hakuna namna..

Finaly Mkong'oto nilioupata mimi kwa kuanzisha vanga ilikuwa mwaka 2011 mr chocolate(Bob junio) walikuwa wamekuja na bonge la nyau mahala fulani kufanya show. kwnye mida ya usiku kama saa7 wakatoka club likabaki la manyani sasa........ nilipigwa na jamaa niliyedhani na mu mudu asee masela wangu wote wakaniachia msala siku 3 uso umevimba sitoki nje masela wananiuguza japo walinikimbia asee.

MAMBO YANABADIRIKA SANA
Ugomvi umemalizwa na kuku wa kfc 😂 sahizi vijana wote laini laini na wanaogopa kuumia sana wanakwepa shari kwa namna yeyote ile.
 
kama sio kigoma sijui
 
Ndio wale wabishi wa evolution theory waelewe binadamu tumetokana na manyani, tabia zilikuwa za kinyaninyani, wajumbe nasikia wanatumia neno la "manyani" ila Kwa muda mfupi tumeanza kuziacha na kubadirika kitabia hii inaingia kwenye gene.

With time utaona Hata vidole vinakuwa vyembamba kama pin, ili tuweze ku type vizuri kwenye keyboard ya simu, Kwa Sasa vidole ni vipana unakuta unataka P unabonyeza O.
 
Level ya hormones za kiume ni ndogo Sana leo !

Zamani hasa miaka ya tisini kurudi nyuma pombe nyingi zilikua na hormones za kiume kibao (testosterone)ugomvi ukawa mwingi sana kwa walevi!

Kanisa likalaani,viwanda vikaweka hormones za like kibao na wanaume tukaanza kuwa humble kama wanawake na sio kuwa agressive kama zamani!!

Nakumbuka mitaa ya Bunda pale nikiwa mdogo niliona vurugu sana kukutwa mtu kafia mtaroni ilikua kawaida sana!!
 
daah we jamaa umenikumbusha mbabe wetu legendary kaka mkubwa ahmad huyu kwanza mkwara wake anafunga kitambaa chekundu mkono wa kushoto kama kapteni wa mpira na kingine anazungusha kichwani (usongo).🤣🤣 hapo nyie hata mje shule nzima lazma mchezee kichapo wkt huo sisi tupo nyuma yake tunamtia hasira kwa hype kibao mwamba anashusha kipondo.
 
Level ya hormones za kiume ni ndogo Sana leo !

Zamani hasa miaka ya tisini kurudi nyuma pombe nyingi zilikua na hormones za kiume kibao (testosterone)ugomvi ukawa mwingi sana kwa walevi!

Kanisa likalaani,viwanda vikaweka hormones za like kibao na wanaume tukaanza kuwa humble kama wanawake na sio kuwa agressive kama zamani!!

Nakumbuka mitaa ya Bunda pale nikiwa mdogo niliona vurugu sana kukutwa mtu kafia mtaroni ilikua kawaida sana!!
Yaani ugomvi ni hormones za kiume ?? Acha uongo we jamaa.
 
Wala sio ushamba ilikuwa ni jadi mkuu. Mbona miaka hiyo hata Dodoma mbabe wa mtaa alikuwepo? Arusha Hali hiyohiyo?
Zama zimebadilika. Enzi hizo kulikuwa hakuna sheria kali wanawake wanaliwa sana mande na hawasemi. Huwa ninasema kama sheria zikibadilika zikawa kama za US kuna watu wakubwa na viongozi wataburuzwa mahakamani kama Pdiddy
 
Halafu huwezi amini ninachokwambia!!
Humbleness sio tabia ya kiume Bali agressiveness!!
Sio kweli labda uwe akili mgando ndio utaamini hilo.
Me hutatua matatizo kwa akili na sio maguvu na hasira. Kua aggressive muda wote ni tatizo la akili.

Wapo watu aggressive ukikaa nao kidogo utajua tu huyu umeme mdogo kichwani, ukienda mbali zaidi ukampeleka hospitali itathibitika kua huyu bwana chaji humo kichwani hazishikamani vizuri.
 
Hiki kitu hata mimi nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa...

Kijijini kwetu kulikuwa na mnada wa kila mwezi, ilikuwa ni nadra sana. Angalau kila mwezi lazima ugomvi utokee. Ninapoongea ugomvu siyo wa kupigana ngumi tu, ugommvi wa kuchomana visu. Kiufupi ni kuwa kila mnada ilikuwa lazima mtu afe au ajeruhiwe vibaya sana...

Kwenye mikesha ya sikukuu na sikukuu zenyewe ndo usiseme, zilikuwa zinapigwa sana ngumi mitaani. Kuna mkesha mmoja pardi alizichapa na waumini kwenye kilabu cha pombe.

Wanawake walikuwa wanapigwa sana na waume zao. Ilikuwa ni kawaida kila wiki kusikia mwanamke anapiga kelele yavilio kisa kupigwa. But now nipo mkoani kwetu mwezi wa tanoo huu sijawahi kusikia mwanamke analia kwa kipigo, kweli zama zimebadilika.

Mimi nilikuwa mpole na muoga sana, lakini nilikuwa nalazimika kupigana sababu ya kuwa usipopigana unaonekana kama mtoto wa kike.

Siku hizi hizo mambo zimepungua kwa sababu

1. Ugumu wa maisha; Zamani watu walikuwa na uhakika wa chakula ndo maana walikua wanapata nguvu na mawazo ya kupigana. Siku hizi maisha magumu, mtu anakula mara moja kwa siku nguvu za kupigana anazitoa wapi?

2. Afya: Watu wa zamani walikuwa na afya sana, mnadundana ngumi kavukavu lakini fresh tu. Siku hizi unamuona mtu mzima kumbe ana magonjwa kibao. Ukimpiga ngumi moja kazima. Unapata kesi ya mauaji

3. Polisi kuongezeka: zamani hasa vijijini ilikuwa ni nadra sana kuona polisi. Kwa hiyo ugomvi mwingi ulikuwa unaisha kienyeji tu. Siku hizi polisi wamekuwa wengi na kama mjuavyo kuingia polisi ni bure ila kutoka ndo kipengele. Hii imesababisha watu wapunguze ukorofi...

4. Elimu na kustaarabika: Zamani ilikuwa kawaida kuona mtu anajisifia ubabe wa kupiga watu, lakini siku hizi baada ya watu kuelimika wanaona hayo ni mambo ya kijinga. Ubabe wa sasa ni kuwa na pesa nyingi...

5. Masculinity: Nadhani pia homoni za kiume zilikuwa juu sana zamani na kama tujuavyo uanaume unaendana na kuwa aggresive. Lakini siku hizi wanaume tumekuwa siyo aggresive kama zamani. Unakuta mwanaume yupo tiktok yupo busy anasema 'tap tap screen guy, please send me gifts' Huyu ukimwambia apigane anaona kama unampa laana...​
 
Back
Top Bottom