Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Sasa hivi ukimugusa mtu unakuwa unachezea pochi yako so uchaguzi upo kwako.
Ila zamani tulikuwa tunaishi kibabe sana kuanzia watoto mpaka watu wazima.
Sisi kipindi tunasoma shule ya msingi tulilazimika kuunda vikundi kwa ajili ya kujilinda mitaani,na shuleni kwetu tofauti na hapo kila siku kichapo kutoka kwa wababe wa shule na mitaani kilikuwa kina kuhusu.
 
Mamaeh padre naye anawaonesha waumini wake yey sio mnyonge🤣🤣🤣
Zamani kulikuwa pamechangamka sana, kila mtu hataki kuwa mnyonge. Hilo tukio huwa linanichekesha sana nikikumbuka. Ile parokia ilikuwa na mapadri wawili, so wakati mmoja anaongoza ibada ya mkesha mwingine akaona ngoja akagonge gambe. Na kilabu kilikuwa jirani kabisa na kanisa...
 
Unaongelea mavarangati ya juzijuzi tu, we kumbe bado dogo uliza wakongwe wakuambie vagi za enzi zao kwenye madisko na mikesha nyie mkasome. Unaambiwa hapohapo kwenye madisko ya shuleni wahuni wa mitaani walikuwa wanakuja na kucheza na mademu zenu wa hapohapo shuleni mnanyang'anywa. Mkono ulikuwa unapigwa haswa kati ya ya raia na wanafunzi au wanafunzi kwa wanafunzi kugombea mademu wa kucheza nao disko la welcome form one/form five na lile disco la kuhitimu form four/six
 
Nakumbuka miaka Ile ya 1995 pale Coco beach kulikuwa na beach party watu walikuwa wanakesha lkn ikifika SAA 6 Tu unakuta watu wameshachomana visu.
Zamani kipindi tunakua ilikuwa lazima ujifunze ngumi kidogo ili uweze kuishi mtaani,siku kama za Christmas na mwaka mpya watu waliuana Sana kwenye kumbi za starehe
 
Hii iliwahi kunikuta japo ni majuzi hapa 2013. Tupo kwenye disko la graduation, nimekunja kidogo suruali kwa chini, mhuni mmoja wa mtaani akaja anataka kunipiga kisa nimekunja tu suruali. Ilibini wanangu waje waniokoe kwenye ile dhahama. Kuna siku napita ubungo pale, nasikia mtu ananiita, kugeuka ni huyo jamaa. Kachoka vibaya mno, ananiomba hela ya fegi...
 
Ubabe ndo ulikuwa habari ya mjini. Mwaka mpya bila baruti ilikuwa haijawahi kutokea lakini Kwa Sasa hamna madogo wote wamekuwa wapaka mafuta ya mwamposa nashangaa sana
 
Sisi tulikuwa na zamu kabisa ya kuzipiga. Mnapangiwa Leo mnazipiga familia ya fln na fln na zinapigwa kweli
 
Nikweli kabisa mpira ulikuwa hauishi bila ngumu nakumbuka hapo ngoma tulipigwa vibaya mno baiskeli tulizitelekeza kutoka uhai wetu. Siku hizo police hakuokoi labda ukimbilie kituoni ukaingie ndani mwenyewe.

Kuna siku zilipigwa kati ya Cuf na ccm acha kabisa sisi tulikuwa badobado aiseee watu walitoana damu sana na hakuna hata mmoja alie enda kushitaki Wala police kukamata watu.
 
Ongeza na majambazi, wezi wa Ng'ombe na mauaji ya wazee na wachawi kanda ya ziwa wote wameisha

Miaka 100 ijayo, Duniani patakuwa sehemu salama zaidi sababu ya elimu kuongezeka
 
Enzi hizo magomeni mitaa ya day break uwanja wa zamaleki kukiwa na mechi ngumi kupigwa ni kawaida hadi ndondo zilikuwa ni ngumi tu..pia ya kurushiana mawe watoto wa mwananyamala vs watoto wa magomeni ilikuwa ni hatari..nimemkumbuka mwenzetu mmoja(Abubakari kwa sasa marehemu) alikuwa na ngumu hatari ila kwa bahati alikuwa anasumbuliwa na kifafa..
 
Hii mtandao naamini hao lazima kuna wanao umia mioyo na kuharibu maisha yao kwa hayo kisaikolojia

Huku tu kuna watu wanahatafjga wakiyapata kama hawana mioyo inakuwa balaaa wakilalamika

Sio nzuri ila ndio maisha hayo
Hata humu mfano wa Lucas mwashambwa wangekuwa wanapigwa Kila siku iendayo Kwa Mungu maana wanakera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…