Sasa imekuwa wazi, kanda ya ziwa ina watanzania asilimia 25 tu

Sasa imekuwa wazi, kanda ya ziwa ina watanzania asilimia 25 tu

Tatizo anataka kulazimisha kwamba Kanda ya Ziwa ni wasukuma pekee. Wasukuma wapo Geita , Simiyu na Mwanza. Ila Kagera na Mara ni makabila tofauti.
Wewe ndiye unayelazimisha kwa vigezo vya hewani.

Kanda, zimegawanywa kwa kuangalia jiografia tu, hakuna kigezo kingine chochote. Ulifahamu hilo.

Tanzania tuna makabila 120, kanda hazifiki hata 10, sasa mgawanyo wa Kanda kwa msingi wa makabila, mqra desturi, sijui muingiliano wa kibiashara, vinatoka wapi?

Sababu kubwa iliyotazamwa katika kugawanya Kanda ilikuwa kukaribiana kwa mikoa ili huduma zile ambazo haziwezi kuwepo kwenye kila mkoa, ziwekwe kwenye mkoa mmoja, na ile mikoa ya karibu, ipate huduma hizo tokea kwenye mkoa huo wa jirani.
 
Ongezaea:-
1. Katavi
2. Simiyu
3. Kigoma
4. Tabora

Hadi Katavi Ni Kanda ya Ziwa? Duh. Naona kwa Sasa kila mkoa Tanzania upo Kanda ya ziwa. Zamani kabla ya Geita na Simiyu kuja, Kanda ya Ziwa ilikuwa Mwanza, Mara na Kagera. Na kila mkoa ulikiwa na makabila yake tofauti. Mwanza wasukuma na wakerewe, Kagera wahaya, wahangaza na Mara wakurya, Wajita, wazanaki etc. Na wakati mikoa hii ikiwa pamoja hakuna aliyekuwa analazimisha Shinyanga na Tabora na Rukwa ziwe Kanda ya Ziwa.

Ila walipoleta mikoa miwili mipya ya Geita na Simiyu basi, ikaoneka Kanda ya Ziwa ni mikoa yenye kabila Fulani na tamaduni Fulani.
 
Ukweli ni kwamba kanda ya ziwa ndo sehemu ambayo mgombea Urais yeyote lazima aitupie macho vya kutosha.
Kanda ya ziwa ina idadi ya watu 12m+, hiyo ni chini ya 25%. Hakuna mtu anaweza kuwa Rais kwa kupata 25%.

Kanda ya Ziwa ina wakazi wengi lakini kimaamuzi, haina uwezo wa kufanya maamuzi yoyote yanayoweza kuwaburuza zaidi ya 75% waliobakia.
 
Jumlisha hapo[emoji116]
1667230775006.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha fix bhana, Kigoma na Mwanza wapi na wapi?? Mnalazimisha kanda ya ziwa iwe eneo kubwa bila sababu za msingi.
Basi endeleeni kuelewa kama unvyoelewa ila siku mkianza kuleta maswala ya ukanda katika kufanya mamuzi kama uchaguzi ndo mtaelewa kwanini tunawambia kwamba ni zone hatarishi.
 
Tumeanza kuwaiga kenya? Kupiga kura kwa misingi ya ukabila?. Kanda ya ziwa huwa haipigi kura kwa pamoja. Ni mkoa wa Simiyu na Geita pekee ndio ngome za CCM kwa asilimia 100. Lakini Mwanza, Mara na kagera Ni 60 kwa CCM na 40 kwa upinzani. Hasa mkoa wa Mara huwa ni 50 kwa CCM na 50 kwa upinzani CHADEMA.
Siyo Kura tu hata uwaziri hugawiwa kikanda na Kanda ya ziwa hutoa wengi labda wapitishe wabunge wasioenda shule,huko Mara upinzani hupata vitu vingapi bungeni!?..kagera?..
 
Leo ndo nimegundua kwamba Tabora ipo kanda ya kati.
Nilikuwa najua ni kanda ya ziwa kwasababu wanaendana na wasukuma.
Wasikuchanganye bibie,Tabora ni kanda ya magharibi tena ni makao makuu ya kanda.Kanda ya magharibi inaundwa na tabora,kigoma na katavi
 
Back
Top Bottom