Sasa imekuwa wazi, kanda ya ziwa ina watanzania asilimia 25 tu

Sasa imekuwa wazi, kanda ya ziwa ina watanzania asilimia 25 tu

Kanda ya Ziwa ni MARA, KAGERA, MWANZA, GEITA, na SIMIYU.

Ingawa kuna mikoa iko kanda ya magharibi lakini haina tofauti na kanda ya ziwa kama KIGOMA, TABORA na KATAVI.

Kuhusu siasa sioni sababu ya hofu kwasababu kanda ya ziwa hawajawahi kuoiga kura kama BLOCK ingawa lolote linawezekana.
Halafu mkoa wa Shinyanga uko kanda ipi?
 
Naona somo la kanda limekuwa tatizo kwa nchi hii

Chukua hii

1. Kanda ya Ziwa
Mwanza
Kagera
Shinyanga
Geita
Simiyu
Mara

2. Kati
Dodoma
Singida

3. Mashariki
Morogoro
Pwani
Dar

4. Magharibi
Kigoma
Tabora
Katavi

5. Nyanda za juu kusini
Njombe
Iringa
Mbeya
Songwe
Ruvuma
Rukwa

6. Kusini
Lindi
Mtwara

7. Kanda ya Kaskazini
Tanga
Kilimanjaro
Arusha
Manyara
 
Umekosea. Kagera siyo Kanda ya Ziwa. Ipo Kanda ya Magharibi. Naona Wahaya hawakutaka kujumuishwa na wasukuma.

Mgawanyo wa Kanda:

Kanda ya Kaskazini (Arusha, Manyara, Kilimanjaro)

Kanda ya Mashariki (Pwani, Morogoro, Dar)

Kanda ya Kusini (Mtwara, Lindi, Ruvuma)

Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa)

Kanda ya Magharibi (Kagera, Kigoma, Katavi)

Kanda ya Kati (Dodoma, Singida, Tabora)

Kanda ya Ziwa (Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Mara)
We kiazi Tanga iko wap
 
Tabora kuna ziwa gani?kutoka tabora mpaka uliguse ziwa victoria ni km 500,tabora ni jirani na kigoma,labda uongelee ziwa tanganyika
MMMMM!!Mkuu unajua jiografia ya nchi hii lakini?!!Yaani Tabora iko jirani sana na Kigoma kuliko Mwanza?!!eti km 500!!Mwanza na tabora ni karibu zaidi kuliko Tabora kwenda Kigoma.
 
Jumla ni around milioni 15 ambayo ni kama robo tu ya watanzania wote.
Swali dog la ulinganifu; ni kanda gani yenye idadi kubwa ya watu kuliko Ziwa, au inayokaribiana na hiyo mikoa iliyotajwa kwa idadi ya watu?
 
Kuhusu siasa sioni sababu ya hofu kwasababu kanda ya ziwa hawajawahi kuoiga kura kama BLOCK ingawa lolote linawezekana.
Kadri mambo yanavyokwenda, utafika wakati wataamka toka kuwa 'sleeping giant' (kama alivyoitwa na mkoloni mwingereza) wataamua kufanya mambo as a block!
Na kwa jinsi wanavyozaliana kwa kasi (jamaa hawana mchezo na hiyo kitu 😂😂) na kusambaa, morogoro, mbeya, rukwa, katavi, nk zitakokwa upande wao muda siyo mrefu.
Dawa nzuri inatofaa ni kuendelea kuvunja nguvu za tribal identification.
 
Sisi kanda ya ziwa tunataka hii nchi igawanywe kila watu wapate kipande chao. Tuna madini ya kutosha, tuna maji ya kutosha, tuna samaki kibao, tuna mifugo na ardhi ya kutosha vilevile ni wachapa kazi na tuna upendo na nidhamu. Huko kunakobaki tunawaachia nyie mafisadi, tuone nani ataendelea. Huyo bibi kila siku safari zake ni kanda ya ziwa tu hamshangai? Mbona haendi bumbuli kwa kina mikamba au singida kwa kina machemba? Lake zone taifa kubwa, na sahizi tuna hasira tunawachekiii tunasema hiii bangosha!
 
Huu ndio urithi aliotuachia Hayati Mwl Nyerere.
Kwani alisema "urithi" huo hauwezi kupunguzwa au kuongezwa kadri ya matakwa yatakavyohitaji kufuatana na mabadiliko yaliyopo kwa wakati husika?

Sentensi imekuwa ndefu, lakini inaeleweka.

Visingizio vya namna hii ni kukosa fikra.
 
Huwa najiuliza sijui ni kwanini watanzania wa mikoa mingine Sana Sana watu wa mkoa wa arusha hawaipendi mikoa ya Kanda ya ziwa especially mwanza
Em tuambizane sababu ni nini?
Hadi mnakua kama wakenya vile hawaipendi Tanzania.
 
Kumbe usafiri wa reli mpya utapoanza tutasafiri Tabora - Mwanza kwa masaa manne!
Masaa manne mengi mno .... tabora to mwanza ni karibu ....ukiwa kahama na tabora ni pua na mdomo ..mfano isaka unaweza kuishi mkoa wa tabora ukanunulia mahitaji mkoa shinyanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Masaa manne mengi mno .... tabora to mwanza ni karibu ....ukiwa kahama na tabora ni pua na mdomo ..mfano isaka unaweza kuishi mkoa wa tabora ukanunulia mahitaji mkoa shinyanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Masaa manne si mengi. Vituo vya treni ni vingi njiani, na vyote lazima isimame.
 
Back
Top Bottom