econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Hoja za kipuuzi kabisa.
Ukienda Mwanza sasa hivi, hasa jijini Mwanza, miongoni mwa wafanyabiashara, hasa wakubwa na wa kati, wapo wa makabila mengi, wakiwemo wachaga, wameru, mpaka wakenya. Sasa muingilioni wa kikanda unaousema sijui ni upi.
Sioni utofauti wowote wa Kanda ya Ziwa na Kanda nyingine. Na wala Kanda hazikugawanywa kwa kufuata makabila au desturi za wahusika.
Ebu niambie muingiliano wa watu wa Iringa na Rukwa kidesturi, au watu wa Ruvuma na Lindi, jadi wawe kwenye Kanda moja. Au niambie desturi za watu wa Kagera zinazoshabiahiana na za watu wa Shinyanga. Au watu wa Tabora Vs Kigoma.
Leo hii, mbao zilizojaa Mwanza, Shinyanga, Tabora, zinatoka Iringa na Mbeya. Hayo ni maingiliano ya kibiashara. Kwa hiyo tuseme na Mbeya na Iringa ni Kanda ya Ziwa? Mahindi yanayoliwa Mwanza na Shinyanga, zaidi yanatoka Singida, maharage na viazi mviringo vinatoka Arusha, kwa hiyo hii mikoa ya Arusha na Singida, nayo ni Kanda ya Ziwa kwa sababu ina muingiliano mkubwa wa kibiashara na mikoa ya Kanda ya Ziwa?
Tatizo anataka kulazimisha kwamba Kanda ya Ziwa ni wasukuma pekee. Wasukuma wapo Geita , Simiyu na Mwanza. Ila Kagera na Mara ni makabila tofauti.