Sasa inakuwa rasmi mafuta bila stakabadhi

Sasa inakuwa rasmi mafuta bila stakabadhi

Tangu Rais wetu mpendwa aingie madarakani baadhi ya vituo vya mafuta havitoi receipt za ki eletronic. Mfano ukienda PUMA kawe unaambiwa karatasi zimeisha, siku nyingine hakuna wino, ni mwezi sasa. PetroAfrica Bunju, unambiwa hakuna karatasi, Oilcom unaambiwa machinembovu. Ni vituo vingi vinafanya hivyo.

TRA MPOOOOO
Ni kweli kabisa. Vituo vingi vya mafuta hawatoi risiti siku hizi. Waziri wa fedha, TRA naona mmejitoa ktk jukumu lenu la kuwaangalia hawa jamaa. Au mnataka Mama aonekane hafai. Kwa kifupi ni hujuma inayoendelea Sasa hivi.
 
Naomba basi nichangie haya!
Hii haiko kwenye mafuta tuu bali kuna mabadiliko kila mahali, chanya na hasi..na hili ndio tatizo la kuwa na oneman show! Akiondoka mambo yanaparaganyika.. Hili si tatizo la mtu mmoja bali ni udhaifu wa kanuni na sheria zetu tulizojitungia wenyewe
Wanasiasa ni wapitaji tuu lakini sheria na kanuni zikiwa nzuri hutaeza kuona mtikisiko kukiwa na mabadilko
Lakini hilo la kulipa kodi lipo kisheria hapa diniani na mbinguni.
 
Kikubwa umepata mafuta mengine hayakuhusu
we ni tatizo kubwa kuliko hata wasiotoa risiti. kweli elim ya kodi na rushwa ianzie chekechea. kama hujui hata umuhim wa kodi nimehurumia sana ubongo wako! pole
 
Yan huyo Magufuli mtamlilia sana, lakin iwe iwavyo, watu wafanye wafanyavyo..abaki hivyo hivyo amekufa
 
Bado tunahitaji elimu ya umuhimu wa kodi.....

Ila tena ukiwaza tena kodi yenyewe inavotumika na manasiasa unaona vyovyote poa tu.
 
Elimu ya kodi hamna kwa wananchi, halafu pia hiyo hiyo inayolipwa inapigwa sasa hapo uzalendo(unakufa) ndio hapo mtu kulipa inakuwa kazi
Kwakweli inakera, kuwaza kodi inatafunwa na watu wanajilipa wanavotaka...inapunguza hata uzalendo kwa walipa kodi
 
Ulifuata mafuta au risiti........!


Hausikii ule msemo wa "Mama kasema wafanyabiashara tusisumbuliwe" mwisho wa kunukuu.
 
Tangu Rais wetu mpendwa aingie madarakani baadhi ya vituo vya mafuta havitoi receipt za ki eletronic. Mfano ukienda PUMA Kawe unaambiwa karatasi zimeisha, siku nyingine hakuna wino, ni mwezi sasa. PetroAfrica Bunju, unambiwa hakuna karatasi, Oilcom unaambiwa machinembovu. Ni vituo vingi vinafanya hivyo.

TRA MPOOOOO
Poa tu. TRA wenyewe ni wezi tu wenye vibari
 
Hayo mafuta yanapoingia tu hapo Bandarini yanalipiwa kodi. Huwezi kukwepa kodi Tanzania labda upitishie mafuta angani.

Utakwepa kodi moja ila nyingine lazima ulipe.
 
Tangu Rais wetu mpendwa aingie madarakani baadhi ya vituo vya mafuta havitoi receipt za ki eletronic. Mfano ukienda PUMA Kawe unaambiwa karatasi zimeisha, siku nyingine hakuna wino, ni mwezi sasa. PetroAfrica Bunju, unambiwa hakuna karatasi, Oilcom unaambiwa machinembovu. Ni vituo vingi vinafanya hivyo.

TRA MPOOOOO
Haya ndio tunayapenda na kuyachekelea, sasa ni wakati wa maneno matamu na kuwaridhisha majizi.Tusilalamike huu ndio uhuru tunaoupenda,uhuru wa kufanya tupendavyo.
 
Back
Top Bottom