Sasa inakuwa rasmi mafuta bila stakabadhi

Ni kweli kabisa. Vituo vingi vya mafuta hawatoi risiti siku hizi. Waziri wa fedha, TRA naona mmejitoa ktk jukumu lenu la kuwaangalia hawa jamaa. Au mnataka Mama aonekane hafai. Kwa kifupi ni hujuma inayoendelea Sasa hivi.
 
Lakini hilo la kulipa kodi lipo kisheria hapa diniani na mbinguni.
 
Kikubwa umepata mafuta mengine hayakuhusu
we ni tatizo kubwa kuliko hata wasiotoa risiti. kweli elim ya kodi na rushwa ianzie chekechea. kama hujui hata umuhim wa kodi nimehurumia sana ubongo wako! pole
 
Yan huyo Magufuli mtamlilia sana, lakin iwe iwavyo, watu wafanye wafanyavyo..abaki hivyo hivyo amekufa
 
Bado tunahitaji elimu ya umuhimu wa kodi.....

Ila tena ukiwaza tena kodi yenyewe inavotumika na manasiasa unaona vyovyote poa tu.
 
Elimu ya kodi hamna kwa wananchi, halafu pia hiyo hiyo inayolipwa inapigwa sasa hapo uzalendo(unakufa) ndio hapo mtu kulipa inakuwa kazi
Kwakweli inakera, kuwaza kodi inatafunwa na watu wanajilipa wanavotaka...inapunguza hata uzalendo kwa walipa kodi
 
Ulifuata mafuta au risiti........!


Hausikii ule msemo wa "Mama kasema wafanyabiashara tusisumbuliwe" mwisho wa kunukuu.
 
Poa tu. TRA wenyewe ni wezi tu wenye vibari
 
Hayo mafuta yanapoingia tu hapo Bandarini yanalipiwa kodi. Huwezi kukwepa kodi Tanzania labda upitishie mafuta angani.

Utakwepa kodi moja ila nyingine lazima ulipe.
 
Haya ndio tunayapenda na kuyachekelea, sasa ni wakati wa maneno matamu na kuwaridhisha majizi.Tusilalamike huu ndio uhuru tunaoupenda,uhuru wa kufanya tupendavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…