Kuna kijiji kinaitwa Kitagata nilikuwa pale 2017. Ni kipande cha kati ya Kasulu na Kibondo. Hivi ndipo inapopita hiyo barabara?Kuna mambo tunaweza kubishana au kubishania ila sio kazi kubwa alizofanya Rais Samia ndani ya Miaka 4.
Rais Samia kwa Ushirikiano na AfDB wanajenga Barabara yenye urefu wa kilometa 305 kutoka Kabingo–Kasulu–Manyovu hadi Burundi kwa thamni ya TZS800bn
Tunafahamu barabara ya Kabingo–Kasulu–Manyovu katika Mkoa wa Kigoma inahusisha kipande cha Kabingo kabla ya Kasulu hadi Manyovu, chenye urefu wa jumla ya 260 km, ambacho ni sehemu ya awamu ya mradi wa upandishaji wa kiwango hadi bitumen standard, zikitumia mkandarasi na ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Kipande cha Kabingo–Kasulu kina urefu wa takribani 184 km, kikitolewa katika Lot 1 na kukusudiwa kuimarisha usafiri wa kawaida kwenda mpaka wa Burundi kupitia Manyovu-Mugina
Gharama za jumla za mradi wa upandishaji wa barabara ya Nyakanazi–Kasulu–Manyovu zilikadiriwa kuwa karibu USD 322 milioni (sawa na takribani TZS800bn, ikijumuisha sehemu zote mbili za Tanzania (260 km) na Burundi (45 km) pamoja na kubuni na kujenga One‑Stop Border Post Manyovu–Mugina Mkataba wa Kiufundi na utekelezaji wa mradi ulifanywa kwa ushirikiano wa TANROADS na AfDB.
Mana nilipita hali ilikuwa mbaya sana. Vumbi zito, jekunduuuu na usafiri ni vimchomoko (Toyota probox)