Sasa ni dhahiri Bungeni kuna kundi la Rais Samia na kundi la Hayati Magufuli. Spika Ndugai awataka wabunge wa CCM kuitisha kikao cha usuluhishi

Sasa ni dhahiri Bungeni kuna kundi la Rais Samia na kundi la Hayati Magufuli. Spika Ndugai awataka wabunge wa CCM kuitisha kikao cha usuluhishi

Waache wamalizane wenyewe kenge hao si walitaka bunge la chama kimoja?? Waendelee na ushetani wao

Maneno ya Lissu na Lema yanatimia!!!Walikuwa wanawapiga Vita sana na kuwabagua sana Wabunge wa Upinzani hasa CHADEMA na ACT Wazalendo.

Lisu na Lema waliwaambia wakishawamaliza Wapinzani Watageukiana WAO KWA WAO!!!
Mwalimu Nyerere(RIP) aliwahi sema ukianza KUBAGUA NI SAWA NA KULA NYAMA YA MTU...Ukisha onja huwezi kuacha....!!!!
 
Ina maana hao wabunge hawakuelewa jana alivyosema yeye na Magufuli ni kitu kimoja? wana vichwa vizito sana.

Hii inathibitisha Ndugai ni kiongozi dhaifu wa bunge, ameshindwa kurekebisha hali kwasababu nae anaingia kwenye kundi mojawapo kati ya hayo, dawa ni kulivunja hilo bunge tu.
 
Speaker ni dhaifu mno. Naibu wake even worse.

Yaani jambo hili mpaka waende wakazibane midomo kwenye party caucus? Speaker angekuwa strong angewadhibiti mulenule ty. Strong hapa haimaanishi kufokafoka kibabe bila kuishirikidha halmashauri ya kichwa
Wangekuwa Chadema wahusika wangetolewa nje.
 
Unaleta habari ya upotoshaji inakusaidia nini? Sawa kuna makundi haya wewe inakusaidia nini?
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana.

Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu baada ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lucy Mayenga kudai kuwa kuna kundi la wabunge wa chama hicho ambalo linamsifia Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kudhoofisha alama zilizoachwa na Hayati Rais John Magufuli.
Tena ikibidi hata Wachinjane tu kabisa.
 
Mbunge wa viti Maalum Lucy Mayenga amedai leo Bungeni kuwa kuna kundi la wabunge wengi ambao wanamepanga kuhujumu legacy ya Magufuli na kutaka kutenganisha Urais wa Samia na urais wa Magufuli

Amedai wabunge hao wanamsifia Samia Suluhu kwa lengo la kuonyesha kuwa Maguuli alikuwa akifanya vibaya na tangu awali wanafahamika kuwa walikuwa wakimpinga Magufuli.
Ameongezea watu hao kuwa wanamchonganisha Samia na watu wa Magufuli ambao alikuwa amewapanga na mikakati yao wanaijua

Zaidi unaweza kumsikiliza hapa

She is right, kuna jitihada kubwa sana zinaendelea za kumchafua Magufuli
 
Wamwagane hata damu,hio mishahara si ni zao za kumwaga damu za watanzania kwenye uchaguzi
 
Mbunge wa viti Maalum Lucy Mayenga amedai leo Bungeni kuwa kuna kundi la wabunge wengi ambao wanamepanga kuhujumu legacy ya Magufuli na kutaka kutenganisha Urais wa Samia na urais wa Magufuli

Amedai wabunge hao wanamsifia Samia Suluhu kwa lengo la kuonyesha kuwa Maguuli alikuwa akifanya vibaya na tangu awali wanafahamika kuwa walikuwa wakimpinga Magufuli.
Ameongezea watu hao kuwa wanamchonganisha Samia na watu wa Magufuli ambao alikuwa amewapanga na mikakati yao wanaijua

Zaidi unaweza kumsikiliza hapa

Hivi haya makunguni hayasikiagi eti?
 
Kuna dalili zote za kuzaliwa upinzani ndani ya Bunge lisilo na upinzani. Mawazo mbadala hayaepukiki kwenye siasa!
Fisi wameanza kuumana
EzEbMraWYAMjajW.jpeg
 
Back
Top Bottom