Sasa ni rasmi January Makamba Waziri wa ovyo kuwahi kutokea kwenye sekta ya Nishati

You are not serious dude..! Hata kama ni chuki hii yako imezidi, yaani unamlaumu Waziri wa Nishati kwa kupanda bei ya mafuta.? Unajua bei ya mafuta kwa sasa kwenye soko la Dunia?
Mkuu hivi hilo soko LA dunia liko wapi? Mbona bei za mafuta nchi nyingine mfano Rwanda inayopitisha mafuta kwenye bandari ya Dar es salaam iko chini? Au wao hawanunui kwenye hilo soko LA dunia.
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
Udhaifu au uimara wa Waziri wa Nishati na kukatika umeme uhusiano wao ni wa kisiasa zaidi kuliko kiutendaji.
Tanesco ndiye mhusika na mtuhumiwa mkuu.
Kibaya kuliko kitu chochote ni pale umeme unapokatika kila siku, na watumiaji hawaambiwi sababu wala hawana mahali pa kutafuta taarifa.
Wateja wa Tanesco hawana hata mahali pa kueleza madhila yanayowafika.
Hii ni dharau kubwa sana kwa wateja wa Tanesco.
 
Mimi sio muumini wa watu Bali mifumo ya uongozi,unaweza kuwa kiongizi mzuri mfumo ukakukaba.....isijeikawa anchokisema Makamba akitaka kukiweka kwenye matendo,anakutana na mfumo
 
Habari wanabodi naandika hapa nikiwa Na masikitiko makubwa Na huyu Waziri aliyepewa wizara nyeti kabisa


MAKAMBA HII WIZARA IMESHAKUSHINDA IACHE KWA AMANI KABLA HAIJAKUHARIBIA ZAIDI
Ila yote Kwa yote TANESCO Rudisheni umeme Dumila
Wewe haupo dumila hii habari yako umeitunga. Wewe ni pro-Kalemani mnaumia sana kuona wizara ipo mikononi mwa mtu msiyempenda.
 
Alituhakikishia kwamba ndani ya wiki mbili suala la kukatika umeme lingebaki kuwa historia. Mambo yakawa kinyume cha hapo. Kabadilisha gia na kuweka historia ya watangulizi wake na kuwatwisha zigo hilo.
 
Changamoto za Dumila zipo kila kona ya Tanzania. Maendeleo ni mchakato wa muda mrefu. Na suala la nishati siku zote ni nyeti sio kama masuala mengine.

Tuwe wavumilivu tu.
 
Changamoto za Dumila zipo kila kona ya Tanzania. Maendeleo ni mchakato wa muda mrefu. Na suala la nishati siku zote ni nyeti sio kama masuala mengine.

Tuwe wavumilivu tu.
Kwamba alipoingia alikuta umeme upo wa uhakika hata kama unakatika Ila Ni Kawaida Tu. Na Dumila ameikuta hata itokee nini Ila Ni ngumu kulala Giza yaani Ni suala lisilowezekana kutokana Na usalama wa Eneo husika

Halafu kuingia yeye Tu Mwanzoni Hali ilikuwa vizur Sana Ila baada ya Muda mchache Kata Kata ikaongezeka mwishowe kulala bila umeme ikaanza kuwa Hali ya kuzoeleka Na tumefikia kipindi tulikaa siku 4 mfululizo bila umeme yaani hata kurud Kwa dk Hakuna halafu unasema niwe mvumilivu wakati huo TRA ukiwaambia wanivumilie au mwenye pango anivumilie hataki ?

Swali Ni moja Kwa nini asingeendelea alipoishia Kalemani ?

Sisemi kuwa Kalemani alikuwa mzuri kihivyo la hasha ? Ila Kwa nini yeye kuingia kila kitu kimevurugika?

Na aliahidi Wiki 2 mgao ungekuwa Historia

Akaja akasema siku 10 Za ukarabati baada ya hapo kukatika katika kungepungua

Wakaona haitoshi Tanesco wakasema Morogoro tunaongeza siku 1 ili wanaotumia kituo cha Msamvu kukatika katika kutaisha Ila pamoja Na yooote hayo

Dumila Hali kila siku Ni kukata yaani ukiona umeme Dumila haukatiki katiki Basi ujue Ni haupo kabisa?

Na kama Hyo switch ya Dumila inasumbua si waifungie mipira kabsa itulie
 
Mimi sio muumini wa watu Bali mifumo ya uongozi,unaweza kuwa kiongizi mzuri mfumo ukakukaba.....isijeikawa anchokisema Makamba akitaka kukiweka kwenye matendo,anakutana na mfumo
Kama Kalemani aliweza...yeye anashindwaje!?
Hapo ndipo ubovu wake ulipo.
 
Mahitaji ya umeme huenda yakiongezeka na vyanzo hubaki pale pale, hapo ndio pa kuanzia.

Kumbuka kuwa miaka ya nyuma JPM alikuwa akiogopwa na watendaji wa TANESCO, kila mtu analinda ajira yake hivyo wakawa hawafanyii matengenezo miundo mbinu ya shirika lao.

Hakuna namna shirika litakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa ongezeko la wateja ili hali miundo mbinu haifanyiwi ukarabati mkubwa utakaoiwezesha kufanya kazi kulingana na wakati tuliopo.

Siasa ni nyingi kwa January Makamba, kama alivyosema apewe muda ili ahukumiwe kutokana na kuweza au kushindwa kulimudu shirika.
 
No way out. Makamba inabidi aendelee kuwa waziri nje ya hapo KIGOGO ataingia mitamboni kumchafua mama.
 
Jamaa una malalamiko ya msingi ila kuna wanaojidai vichwa ngumu hawataki kukuelewa.
 
Magu akaogopwa mpaka na mitambo na ndio maana Makamba alipo hojiwa alisema kwa kinywa chake "zamani umeme ulikuwa haukatiki mara kwa mara sababu kulikuwa hakuna schedule maintenance.........".

Juzi wabunge wamemuomba awape ripoti ya mantainace zilizokuwa zikifanyika miaka mitano iliyopita, anabaki anabwabwaja tu. Zamani kweli umeme ulikuwa unakatika ila sio kwa style hii ya Makamba sasa hivi too much.
 
Aliongelea schedule maintenance akiwa bado mgeni tofauti na hali alivyoikuta. TANESCO ni shirika linalohitaji kuwa na mshindani wa sekta ya nishati wao wenyewe wataendelea kulalamikiwa mpaka Mitume watakaporudi.
 
Aliongelea schedule maintenance akiwa bado mgeni tofauti na hali alivyoikuta. TANESCO ni shirika linalohitaji kuwa na mshindani wa sekta ya nishati wao wenyewe wataendelea kulalamikiwa mpaka Mitume watakaporudi.
Kwahiyo hii kauli yake ya "zamani umeme ulikuwa haukatiki mara kwa mara sababu kulikuwa hakuna schedule maintenance.........".

ALIROPOKA.
 
Kwani enzi za kalemani umeme ulikuwa haukatiki? ni lini Tanzania umeme ulikuwa haukatiki?, ni lini tanesco ilikuwa imara?.

Tusitake kumbebesha mtu mzigo kwasababu ya propaganda za kipumbavu kwa maslahi ya wajinga wachache..
Makamba mwenyewe alisema umeme ulikua haukatiki sababu ya kutishwa na kutokua na maintenance
Wewe unasema ulikua unakatika. Sasa hapo tuelewe vipi, mbona mnajichanganya wewe na makamba mwenyewe?
Unayemtetea ndio alituambua ulikua haukatiki
 
Wewe haupo dumila hii habari yako umeitunga. Wewe ni pro-Kalemani mnaumia sana kuona wizara ipo mikononi mwa mtu msiyempenda.
Kwa nini kila anayetoa dukuduku lake mnakimbilia kusema ana chuki kwa makamba?
Mbona watu wanapotoa dukuduku kuhusu maji hamsemi wana chuki na aweso?
 
Hii, nimeipenda harafu imenifanya nicheke saana, hadi hapa pembeni watu wamegeuka kunitazamana na kushangaa kwa mcheko.
 
Tukubal tukatae hii nchi ni masikin mno mno,kwahyo mambo kama haya ya umeme hatutayaweza kwa uchumi huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…