Sasa ni wakati Sahihi wa Simba na Yanga Kuunganisha Silaha, Kupambana na Waarabu

Hakuna kitu kama hicho.Watakubaliana leo, halafu kesho kuna timu itawapokea wageni,kuwapa mbinu za mkinzani huku wamevaa jezi za mgeni.Mazuzu!
 
Kama Yanga hamna fanbase kubwa msianze kulilia mashabiki wa timu zingine pambaneni kivyenu tu
 
Sisi kama Yanga hatutaki kuungana na yeyote, kila mtu ashinde mechi zake.
Vibe letu latosha, uwanja huwa tunaujaza wenyewe.
 
Kila mtu apambane na hali yake.
Siwezi kuishangilia Simba hata ikiwaje.

Niko tayari ninyang'anywe mke, lakini sio kuishangilia Simba, mutanisameh.
 
Labda unasahau B..., ila ninyi huwa mnashida sana ya kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ova
H… hilo haliko kwenye kila game, unakumbuka tulivyokichafua CAFCC? Uliona fainali watu walivyokufa kugombea kuingia baada ya uwanja kutapika?
Nyie lini imetokea kwenu hivyo? Ile siku ningechelewa kidogo tusingekuwa tunaongea hapa…

Hiyo mechi ya juzi tu Vs Ahly ingekuwa sisi historia ingeandikwa.
Subiri Dec. uone.
 
Kila mtu apambane na hali yake.
Siwezi kuishangilia Simba hata ikiwaje.

Niko tayari ninyang'anywe mke, lakini sio kuishangilia Simba, mutanisameh.
Mimi naweza kuishangilia kinafiki, mtoto wa mama mkwe nampenda sitakubali kunyang’anywa!
 
Umetisha
 
B... ile mechi ilikuwa ya tiketi za bure za kugawiwa mtaani kwa kila atakaye ni rahisi kujaza, maana hata wageni Mazembe kwenye AFL walijaza kwa tiketi bure pale kwa Mkapa.

Kwa kulipa viingilio mna shida kwenye hilo. Sisi ndiyo huwa hatuna shida kwenye hilo.

Ova
 
Hizo tiketi za bure mbona mimi na jamaa zangu hatukuziona? Kuna rafiki yangu alichelewa kukata tiketi siku 2 kabla ya match tulitafuta tiketi kwa msako mkali VIP C ilipatikana tiketi kwa 80K!
Hapo tuliwatumia wahuni wa K/Koo… acheni bwana nyie.

Okay, vipi robo na nusu ilikuwaje? Ile mechi ya makundi Mazembe je? Ile siku ya Monastir pamoja na mvua kali kunyesha je?
Acha zako h…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…