Wewe sio Mzanzibar... Umeweka bandiko hili kusudi ili kuamsha hisia za chuki dhidi ya Mama yetu! Bila shaka wewe ni Sukumagang au Tagas, hakunaga mzanzibar mwenye ujasiri wa kuharibu au kunajisi jina la Mwenyezi Mungu kama ulivyofanya wewe hapo!
CHADEMA mbona mnahangaika sana kumchonganisha mama na Watanzania? mnatafuta ajenda ya kuja kushinda 2025.
Mlianza na gia ya kumtaka mama ajitenge na mwendazake yeye ni tofauti kana kwamba hakuwemo Serikalini,mkitegemea akimsema vibaya mwendazake atapoteza uungwaji mkono wa wapiga kura walio wengi.Nani asiyejua CCM ilikuwa kwaheri 2015 mwendazake akaiokoa,wabunge hili wakaliona wakachachamaa.
Mkaja na propaganda kila aliyeachwa na mwendazake atamhujumu mama,ili atumbuetumbue ili atumbue na watu wazuri aweke wapigaji baadaye mje na gia huyu ni rais dhaifu zaidi kuwahi kutokea rushwa kila sehemu.
Mkaitumia ripoti ya CAG kufanya propaganda kila palipo onekana hasara basi mwendazake aliiba,huku mkisahau kila mwaka ripoti ya CAG huibua uozo,na ndiyo maana mwendazake aliendelea kutumbua majipu mpaka alipotwaliwa na Muumba.Hilo nalo likashindikana.
Mmekuja na gia ya kumchonganisha mama na kanda ya kati mikoa ya Dodoma na Singida kuliko na ngome ya CCM eti mama aondoke Dodoma ahamie Dar huko abaki Makamu wa rais,mkijua kabisa kuhamishia makao makuu Dodoma mikoa hiyo imenufaika sana na makao makuu kuwa Dodoma. Akifanya hivyo mnajua atawaudhi wapiga kura wa kanda hiyo.Hili sisemi halijafanikiwa yetu macho.
Mmekuja na propaganda ya corona,wakati wa mwendazake alipofunga shule mlitaka lockdown,tukaona wabunge wa CHADEMA wakakimbia bunge,wakikimbia corona wakajifungia wanakojua wenyewe.Mwendazake akausoma mchezo akakataa lockdown.Sasa mnasapoti kila kitu ili tu mama aachane na taratibu zilizotumika kutufanya tuwe huru na maisha yetu pamoja na uwepo wa corona.
Hili sisemi lolote machungu yote yatakayowapata watanzania watamlaumu sana mama na kumkumbuka mwendazake,mtakuwa mmefanikiwa.
Sukuma gang hii ni gia mnayotumia kumfanya mama awachukie wasukuma,na mkifanikiwa hili mtakuwa mmemtenga na wapiga kura wa kanda ya ziwa wote.Na nyie mna ngome yenu ya mikoa ya kazikazini mnajua huko mtapata tu ushindi.Dar wapiga kura mtagawana hivyo mtakuwa mmechuka nchi.
Nachojua mimi chui hawezi badilisha madoa yake,nyie wapinzani hamuwezi kumpenda mama ila mna ajenda yenu.
Rais wetu mpendwa hao wanaokuunga mkono kwenye mitandao wengi wao ni wapinzani.Hebu zunguka mikoani utajua wananchi wako wanataka nini hasa.
Hawa wa kwenye mtandao wa upinzani ndo walimwaminisha Lissu atashinda akaja spiidi kama ametiwa moto,kumbe hata hajulikani kwa wapiga kura,watu wakawa wanauliza huyu ndo nani alikuwa wapi? Kura alizopata hata hakufikia za Slaa.