Sasa ni wakati wetu Zanzibar kuitawala Tanganyika

Kwa ardhi ipi hiyo ya kujenga mahospitali makubwa kuliko Muhimbili , chuo kikuu kubwa kuliko Udom n.k , labda wakajenge baharini huo umaskini wa fikra.
 
Tunahitaji raisi anayewaheshimu WANANCHI na kuiendeleza, kuitunza na kuilinda Tanzania, haijalishi anatoka Tanzania bara au Visiwani, na MAMA akifanya vizuri kwa miaka 4 iliyobaki utaona jinsi Watanzania watakavyompa kura 2025, na hata 2030 akipatikana mwingine mzuri kutoka visiwani Watanzania watamchagua. Hii nchi imeshapita ktk wakati wa ubara na uvisiwani iko kwenye wakati wa maendelo ya watu,vitu na usalama wa Nchi na Wananchi wake.
 
Wewe sio Mzanzibar... Umeweka bandiko hili kusudi ili kuamsha hisia za chuki dhidi ya Mama yetu! Bila shaka wewe ni Sukumagang au Tagas, hakunaga mzanzibar mwenye ujasiri wa kuharibu au kunajisi jina la Mwenyezi Mungu kama ulivyofanya wewe hapo!
Thread closed! 😇
 
Kiutawala nchi,inabidi uwe na nguvu za kiuchumi,kitekinolojia,kijeshi,uwe na taasisi za kiintelijensia zilizobobea,sasa Zenj,kwa uchumi wa karafuu,utaweza vipi kiutawala Bara,jengeni kwanza nchi yenu,viwanda,tekinolojia,jeshi,Elimu,Ili muweze kuingia bara kwenye kila sekta,
Swala dogo kama utamaduni tu linawashinda,ukitaja wanamuziki 10 wa bongo fleva wenye mkwanja mrefu ni wangapi wanatoka Zenj?hakuna,anayevuma zenj huku bara ni underground wa Lindi au mtwara.bado sana wazee,
 
Tofauti ya ya maandishi kati ya Mzanzibar na Mtanganganyika ; subaana huwataala = Subhaanahu Wataala
ZANZIBAR HOYEE = ZANZIBAR OYEE
Angeandika Mzazibar angeandika hivo
 
Hizi ndizo athari za uhuru bila mipika....mleta mada na baadhi ya wachangia mada ni waathirika wa uhuru wa namna hii!
 
Tofauti ya ya maandishi kati ya Mzanzibar na Mtanganganyika ; subaana huwataala = Subhaanahu Wataala
ZANZIBAR HOYEE = ZANZIBAR OYEE
Angeandika Mzazibar angeandika hivo
Ni kweli baadhi yetu hatujui kiswahili, Halima twamuita Alima, na chuo cha kiswahili tunacho.
 
Haitokaa itokee
 
Usituletee Uzanzibari na Uzanzibara! Tutaendelea kuuenzi Muungano wetu kwa faida ya Watanganyika na Wazanzibar.
 
Kuitawala tanganyika kupitia huyo rais aliyebebwa na katiba? Kweye kura hapati hata theluthi..
Kwanini asipate?kama hata siku 100 tu hajamaliza lakini ameleta amani mioyoni mwa watu, kuliko hata hilo lia na kijiji lenzetu!!sisi hatuangalii anatoka wapi cha msingi aongoze sio kutawala!!na huyu mama kwa mwanzo huu kama akienda hivyo bora kikomo kile kitoke tu hadi atakaposema basi!!japo yeye hawezi kupenda, sio ile MIJAMBAZI, eti mitano tena!!atake asitake!!jitu linakuwa hata roho ya kibinadamu halina!!
 
Tanzania haitawaliwi inaongozwa naona kuna watu wana fikra za kiarabu. Tawala ni neno la kiarabu hatuna tawala sisi
Acha ujinga Tanzania kuna watawala hatuna viongozi.
 
Wewe sio Mzanzibar... Umeweka bandiko hili kusudi ili kuamsha hisia za chuki dhidi ya Mama yetu! Bila shaka wewe ni Sukumagang au Tagas, hakunaga mzanzibar mwenye ujasiri wa kuharibu au kunajisi jina la Mwenyezi Mungu kama ulivyofanya wewe hapo!
CHADEMA mbona mnahangaika sana kumchonganisha mama na Watanzania? mnatafuta ajenda ya kuja kushinda 2025.
Mlianza na gia ya kumtaka mama ajitenge na mwendazake yeye ni tofauti kana kwamba hakuwemo Serikalini,mkitegemea akimsema vibaya mwendazake atapoteza uungwaji mkono wa wapiga kura walio wengi.Nani asiyejua CCM ilikuwa kwaheri 2015 mwendazake akaiokoa,wabunge hili wakaliona wakachachamaa.
Mkaja na propaganda kila aliyeachwa na mwendazake atamhujumu mama,ili atumbuetumbue ili atumbue na watu wazuri aweke wapigaji baadaye mje na gia huyu ni rais dhaifu zaidi kuwahi kutokea rushwa kila sehemu.
Mkaitumia ripoti ya CAG kufanya propaganda kila palipo onekana hasara basi mwendazake aliiba,huku mkisahau kila mwaka ripoti ya CAG huibua uozo,na ndiyo maana mwendazake aliendelea kutumbua majipu mpaka alipotwaliwa na Muumba.Hilo nalo likashindikana.
Mmekuja na gia ya kumchonganisha mama na kanda ya kati mikoa ya Dodoma na Singida kuliko na ngome ya CCM eti mama aondoke Dodoma ahamie Dar huko abaki Makamu wa rais,mkijua kabisa kuhamishia makao makuu Dodoma mikoa hiyo imenufaika sana na makao makuu kuwa Dodoma. Akifanya hivyo mnajua atawaudhi wapiga kura wa kanda hiyo.Hili sisemi halijafanikiwa yetu macho.

Mmekuja na propaganda ya corona,wakati wa mwendazake alipofunga shule mlitaka lockdown,tukaona wabunge wa CHADEMA wakakimbia bunge,wakikimbia corona wakajifungia wanakojua wenyewe.Mwendazake akausoma mchezo akakataa lockdown.Sasa mnasapoti kila kitu ili tu mama aachane na taratibu zilizotumika kutufanya tuwe huru na maisha yetu pamoja na uwepo wa corona.
Hili sisemi lolote machungu yote yatakayowapata watanzania watamlaumu sana mama na kumkumbuka mwendazake,mtakuwa mmefanikiwa.

Sukuma gang hii ni gia mnayotumia kumfanya mama awachukie wasukuma,na mkifanikiwa hili mtakuwa mmemtenga na wapiga kura wa kanda ya ziwa wote.Na nyie mna ngome yenu ya mikoa ya kazikazini mnajua huko mtapata tu ushindi.Dar wapiga kura mtagawana hivyo mtakuwa mmechuka nchi.
Nachojua mimi chui hawezi badilisha madoa yake,nyie wapinzani hamuwezi kumpenda mama ila mna ajenda yenu.
Rais wetu mpendwa hao wanaokuunga mkono kwenye mitandao wengi wao ni wapinzani.Hebu zunguka mikoani utajua wananchi wako wanataka nini hasa.
Hawa wa kwenye mtandao wa upinzani ndo walimwaminisha Lissu atashinda akaja spiidi kama ametiwa moto,kumbe hata hajulikani kwa wapiga kura,watu wakawa wanauliza huyu ndo nani alikuwa wapi? Kura alizopata hata hakufikia za Slaa.
 
Duh..,, umepata Breakfast kweli Mkuu?
 
Huyo mama mvaa ushungi ni screen tu kisimbusi & remote viko Msoga


Kwani kuna ubaya gani akiwa role model wake?

Kama ulichoandika ni kweli basi itakuwa kheri maana uzoefu unaonesha enzi za uongozi wa Msonga Neema zilitamalaki kuanzia juu hadi chini!

Hapo vipi?! [emoji2369]
 
Kwa iq zipi sasa[emoji23][emoji23][emoji23]

Mlivyo ma bogus na ubaguzi mwingi mtamuongoza nani

Hapo mentality yako ni ubaguzi tupu umebagua m bara haya umebagua mpemba na bado utabagua koo na koo.
 
pumbaf kabisa, ninyi ndo maanithi mnaotafuta mbinu na chokochoko ili muanze kumchafua mama, mawazo mfu kabisa. Fyuuuuuu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…