Sasa nimeelewa kwanini Lema haijishughulishi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Sasa nimeelewa kwanini Lema haijishughulishi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Hata huyo chatanda keshachemka na inaonekana anatumika na wapinzani wa makinda..alishindwa kulalamika kwenye vikao vya ndani vya chama badala ya kuita press?
Ile haikuwa press wewe. Ule ulikuwa mkutano wa ndani wa wabunge na mdiwani wa viti maalum wa ccm. Sasa unaachaje kuamini na kuita kikao cha chama ???
 
Mary Chatanda ni kakosea sana, tena kafanya makosa makubwa. Makonda alichoongea kilikuwa utani wa kawaida wa watanzania. Hata Dkt Magufuli alishawahi sema anapenda wanawake weupe akimtania Dkt Samia.
Mhu! Utani gani unaweza ukamwambia mtumishi wa umma, mwenye familia maneno ya kudhalilishwa hivyo?
 
Salaam, Shalom!!

Ni muda sasa tangu RC wa Arusha aingie kwa mbwembwe kama kawaida yake katika maeneo mengi aliyokwenda baada ya kuteuliwa kuongoza,

Umati mkubwa wa watu waliokusanyika kumpokea na kuhudhuria utatuzi wa case za wananchi hadharani ambao haujawahi kufikia mwisho, Bado haukumstua Mh Lema.

Wakati Mh Lema akiwa kimya, Mh Gambo naye Yuko kimya, nadhani akiamini ujio wa RC utamrahisiahia njia mbele yake.

Sasa nimeamini Mh Lema, ukimya wake Si wa Bahati mbaya, ni calculated move, kumjibu au kumuongelea RC ni kumpa coverage, Mh Lema ameamua kunyamaza.

Matokeo ya ukimya wa Lema, RC ameanza kuharibu na anasemwa na kushtakiwa na viongozi wenzie ndani ya chama, Ndugu Mary Chatanda, ametoka hadharani kumtuhumu RC Kwa udhalilishaji wa Mtumishi wa Serikali katika hadhara iliyokwenda Kwa Jina la wiki ya HAKI.

Kumbe ukimya una nguvu sana.

Kongole kwako Mh Lema.

Salamu zimfikie Mh Gambo kuwa, kibarua Bado kigumu Arusha, na KAZI ndio kwanza imeanza.

Mungu ubariki Mkoa wa Arusha,

Abarikiwe Nabii Lema.

Ubarikiwe Tanganyika,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿. Amen

Karibuni🙏
Vijana wanasema ni laana ya kumpiga mzee warioba.
 
Mary Chatanda ni kakosea sana, tena kafanya makosa makubwa. Makonda alichoongea kilikuwa utani wa kawaida wa watanzania. Hata Dkt Magufuli alishawahi sema anapenda wanawake weupe akimtania Dkt Samia.
Hakuna utani wa vile,

Mwambie aombe radhi hadharani ikiwa unamhurumia.
 
Mary Chatanda ni kakosea sana, tena kafanya makosa makubwa. Makonda alichoongea kilikuwa utani wa kawaida wa watanzania. Hata Dkt Magufuli alishawahi sema anapenda wanawake weupe akimtania Dkt Samia.
Kimsingi Makonda anamuiga Magufuli, lakini kiukweli hata Magufuli alikuwa hajui utani kwa sababu ni mtu wa jazba na kiburi Cha madaraka. Kilichokuwa kinambeba Magufuli ni kwamba alikuwa rais mwenye kiburi Cha madaraka, hivyo hakuna aliyethubutu kumwambia ukweli maana angeishia kutekwa ama kukuta ya Lisu.
 
Wakimla kichwa makonda kisa vijimaneno kama vile,trust me nitaidharau Sana sekretarieti ya samiah !!!

"Kasema ana mke mzuri nyumbani" hapo kamdhalilisha nani!!?kwani mke wa makonda SI mwanamke kama huyo mama!!!?

Mi naona samiah akae kimya TU apotezee ampigie simu amwambie "chapa kazi lakini kuwa makinj watesi wako ni wengi sana"

Makonda ana mapungufu yake lakini kiutendaji namkubali !nataka mind strong sio legelege kama baadhi ya watumishi was umma!!
 
Salaam, Shalom!!

Ni muda sasa tangu RC wa Arusha aingie kwa mbwembwe kama kawaida yake katika maeneo mengi aliyokwenda baada ya kuteuliwa kuongoza,

Umati mkubwa wa watu waliokusanyika kumpokea na kuhudhuria utatuzi wa case za wananchi hadharani ambao haujawahi kufikia mwisho, Bado haukumstua Mh Lema.

Wakati Mh Lema akiwa kimya, Mh Gambo naye Yuko kimya, nadhani akiamini ujio wa RC utamrahisiahia njia mbele yake.

Sasa nimeamini Mh Lema, ukimya wake Si wa Bahati mbaya, ni calculated move, kumjibu au kumuongelea RC ni kumpa coverage, Mh Lema ameamua kunyamaza.

Matokeo ya ukimya wa Lema, RC ameanza kuharibu na anasemwa na kushtakiwa na viongozi wenzie ndani ya chama, Ndugu Mary Chatanda, ametoka hadharani kumtuhumu RC Kwa udhalilishaji wa Mtumishi wa Serikali katika hadhara iliyokwenda Kwa Jina la wiki ya HAKI.

Kumbe ukimya una nguvu sana.

Kongole kwako Mh Lema.

Salamu zimfikie Mh Gambo kuwa, kibarua Bado kigumu Arusha, na KAZI ndio kwanza imeanza.

Mungu ubariki Mkoa wa Arusha,

Abarikiwe Nabii Lema.

Ubarikiwe Tanganyika,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA [emoji1241]. Amen

Karibuni[emoji120]
Sisi wana Arusha tunaelewa sana umuhimu wa mh Lema.

Lema ni Kati ya viongozi bora kabisa ambaye huwa hakurupuki ktk maamuzi yake.
 
Kwani Makonda alishawahi kujishughulisha kumtaja hata Lema kwa jina?

Makonda tukubali tukatae, ni jitu. Ni mkubwa sana kwa Lema.

Kumbe mlikuwa mnahara, ila baada ya Chatanda kuongea mmepata ahueni.

Makonda haondoki Arusha.
Ajiandae kurudi Koromije kuvua samaki maana habebeki hata kwa turubai
 
Makonda sio mtendaji, Hana kipya anacholeta kwenye understand uongozi, sio mifumo, taratibu, wala nini?! Ni, maneno, ya, mikwara, kutisha watu, just busy body! Ni sawa sawa, na kubeba jiwe uweke kichwani, ubaki umesimama! Utachoka, lakini work done ni zero! Maana no movemwnt
Pamoja na kuwa ndani ya ccm hakuna aliye msafi kutokana na mfumo mzima wa uendeshaji ndani ya chama.

Lkn Makonda ni mbovu kuliko wana ccm wote na hakuna mtanzania yeyote mwenye akili anamkubali Makonda.
 
Mpa mseme na mtasema sana. Eti ukimya siyo wa bahati mbaya. Ngoja ncheke mie
Sasa Makonda ndiyo anagukuzwa kwa aibu kutokana na mdomo wake usiyo na staha.

Yaani mtu hana elimu hana akili ,hana heshima,mwizi wa rasilimali za watanzania.
 
Aondoke mara ngapi?

Dunia ya sasa, umdhalilishe mwanamke hadharani utatokea wapi?

Kama una namba yake, mwambie atoke hadharani kuomba radhi ingawa sidhani kama atakusikia.
Wacha afukuzwe tu maana hana hadhi ya kukalia kwenye ofisi za serikali na kulipwa mshahara.

Hana sifa hizo za kuwa mtumishi wa wananchi
 
Nitaomba JF tuwe na madaraja
Wenye super mind
Simple na lowest

Hatuwezi kuwa jukwaa Moja na mtu kama wewe unawaza vyeo sisi tunawaza nchi

Katiba mpya ni sasa
Sidhani kama umesoma uzi wote wa unaye mhukumu
 
Back
Top Bottom