Kumekuwa na malalamiko hata baada ya kufanyika marekebisho ya mikataba ya HGA na IGA .na wengine wakifikia Kuilaumu TEC kwa kutokuwa na msimamo.
Bila kujua kuwa TEC walisema kuwa kama mkataba utaendelea kuwa hivyo ni bora kufutwa na Serikali iwasikilize wananchi.
Wananchi walitaka maboresho ya kimktaba.
TLS ilitaka maboresho ya mkataba na ASASI zote za kiraia na zisizo za kiraia zilitaka Mabiresho ya mkataba na TEC na TAAsisi zingine hazikupinga Uwekezaji.
MABORESHO YA MKATABA
Wamebadilisha vipengere vyote tata…
- Mkataba maximum miaka 30
- Watalipa kodi zote za Serikali kwa mujibu wa Sheria
- Wamewekewa performance key indicators na watakuwa accessed kila baada ya miaka 5
- Serikali itachukua 60% ya mapato ya faida
- Serikali inauwezo wa kuvunja mkataba muda wowote
- Mkataba huu sio wa gati zote za Bandari ya Dar es Salaam gati ambazo hazipo kwenye mkataba huu zinatafutiwa Mwekezaji mwingine (hata huyu wa sasa)
- Mkataba huu hauhusishi Bandari yoyote mwambao Bahari ya Hindi wala maziwa makuu.
Sasa kwa maboresho hayo Bado wengi nimeona wamefungua Nyuzi za kuilaumu TEC na baadho ya Wananchi na ASASI nyingine za kiraia.
Naomba kuwauliza kuwa Tatizo ni MKATABA AU Tatizo ni waarabu kuwekeza??