Sasa nimegundua, tatizo sio uwekezaji wala Mkataba bali ni Waarabu kuwekeza

Sasa nimegundua, tatizo sio uwekezaji wala Mkataba bali ni Waarabu kuwekeza

Naelewa na nimeshaeleza post za nyuma Na Nikushauri wewe usome na uelewe zaidi Tofauti ya IGA na HGA na ioi inanguvu kuliko nyingine..
Nilichoeleza ni kuwa IGA imefanyiwa ammendments tayari ili mikataba ya HGA ipate nafasi ya kusainiwa
SSH jana kasema kuwa mikataba imetokana na IGA, hajasema kuwa IGA imefanyiwa amendments, kama imefanyiwa heb leta hio iliyofanyiwa amendments tuione
 
Mie haya ya banadari yameshapoita, napiga chapuo tu, kimeeleweka.

Sasa hivi nipo huku:

Unadai upo huku, na hiki ulichokiandika kwenye post yako #58 ni nini?

1698042620072.png

Acheni kutetea mambo yasiyo na maslahi..!!!!

Saa hizi unajifanya eti wangeongea na serikali kimya kimya, hivi unadhani TEC wanakurupuka? Ukiona wanakuja hadharani ujuwe huko kwenye kimyakimya watu wamekaza shingo..!!
 
Ukweli mchungu ni kwamba mapendekezo yote ya TEC yamefanyiwa kazi, wewe bibi na waislam wenzio mliousifia na kusema hauna kasoro yoyote kisa wawekezaji ni waislam jana mmevuliwa nguo na mwislam mwenzenu mama Samia. Polen sana, TEC 3- Faiza 0. Hii imeenda, kula chuma hiko bibi
TEC walitaka bandari wapewe wazawa kwa kuwa uwezo huo tunao wa kuiendesha, hawakutaka kabisa wawekezaji mkuu
 
SSH jana kasema kuwa mikataba imetokana na IGA, hajasema kuwa IGA imefanyiwa amendments, kama imefanyiwa heb leta hio iliyofanyiwa amendments tuione
IGA kuonekana mtaani ilivuja na wala haikuwahi kuonekana kwa kupenda hta sasa huwezi kuiona watu wamekula kiapo kuilinda!
 
Kwa maoni yangu kongole nyingi sana ziende kwa TEC kupitia WARAKA wao.

Naamini bila jicho lao la tatu la kuonya hayo maboresho yasingefanyika.

Ni ushindi mkubwa sana kwa wote waliosimamia maslahi ya nchi kwa kutoa ushauri mbalimbali na umeshafanyiwa kazi.
 
Kwa hiyo wewe na akili zako tuseme za kuzaliwa tu ulidhani issue ilikuwa mkataba mbovu? Huo mkataba ulikuwa na ubovu gani hadi ukaamini?

Watanzania mnapaswa kujifunza sana kuhusu siasa za nchi yenu na ujinga wa wananchi. Na siku mkijua siasa zenu za hovyo na ujinga wenu ndo chanzo cha umaskini wenu hapo ndo mtakapogomboka.

Kiufupi hakuna shida yeyote kwenye uwekezaji wa DP World nchini Tanzania. Ni chuki, uzandiki, siasa za hovyo na ujinga tu ndo zilisababisha kelele zote zile
Wewe ndiye huna akili. Kama mkataba haukuwa na tatizo kwa nini umerekebishwa?
Tukubali kuwa ule mkataba wa mwanzo ulikuwa wa hovyo na maoni ya wananchi yamesaidia kuingia mikataba hii mizuri.
 
TEC walitaka bandari wapewe wazawa kwa kuwa uwezo huo tunao wa kuiendesha, hawakutaka kabisa wawekezaji mkuu
Hiyo kwa upande mmoja, na upande wa pili mkataba urekebishwe. Serikali ime-opt upande wa kurekebishwa. To me sioni shida.

Tatizo lako unataka ionekane kuwa waraka wa TEC hauja-impact chochote..!!
 
Mkuu nilikuwa mmoja niliyekuwa nakupinga sana ila kwa sasa nimegundua kuwa ulikuwa sahihi...
Tatizo sio Mkataba Tatizo ni uwekezaji na Taifa linalowekeza..

Maana Nimeona serikali imefanyia kazi malalamiko yote ya wananchi pamoja na Waraka wa TEC na Mkataba umeboreshwa na umekuwa na maslahi mapana kwa nchi..

Ila bado watu wanahoji kwanini TEC anajihusisha na serkali...na kwanini Serikali bado wanasign Mikataba..

Kwahyo Hata baada ya kurekebishwa kwa mkataba unatka Uadui?

Mkataba umerekebishwa ila bado watu wanajipa umuhimu usio stahili..
Hivi kma mkataba haukuwa na shida wamerekebisha nini? Mbona ni kawa haueleweki hoja yako? Maana mara haukuwa na shida ila waarabu...
 
Kwa hiyo wewe na akili zako tuseme za kuzaliwa tu ulidhani issue ilikuwa mkataba mbovu? Huo mkataba ulikuwa na ubovu gani hadi ukaamini?

Watanzania mnapaswa kujifunza sana kuhusu siasa za nchi yenu na ujinga wa wananchi. Na siku mkijua siasa zenu za hovyo na ujinga wenu ndo chanzo cha umaskini wenu hapo ndo mtakapogomboka.

Kiufupi hakuna shida yeyote kwenye uwekezaji wa DP World nchini Tanzania. Ni chuki, uzandiki, siasa za hovyo na ujinga tu ndo zilisababisha kelele zote zile
Aiseee..!!! Mbona TEC waliorozesha mapungufu yote?? Mwenzetu ulikuwa wakati waraka wa TEC unatoka?
 
Kumekuwa na malalamiko hata baada ya kufanyika marekebisho ya mikataba ya HGA na IGA .na wengine wakifikia Kuilaumu TEC kwa kutokuwa na msimamo.

Bila kujua kuwa TEC walisema kuwa kama mkataba utaendelea kuwa hivyo ni bora kufutwa na Serikali iwasikilize wananchi.

Wananchi walitaka maboresho ya kimktaba.

TLS ilitaka maboresho ya mkataba na ASASI zote za kiraia na zisizo za kiraia zilitaka Mabiresho ya mkataba na TEC na TAAsisi zingine hazikupinga Uwekezaji.

MABORESHO YA MKATABA
Wamebadilisha vipengere vyote tata…
  • Mkataba maximum miaka 30
  • Watalipa kodi zote za Serikali kwa mujibu wa Sheria
  • Wamewekewa performance key indicators na watakuwa accessed kila baada ya miaka 5
  • Serikali itachukua 60% ya mapato ya faida
  • Serikali inauwezo wa kuvunja mkataba muda wowote
  • Mkataba huu sio wa gati zote za Bandari ya Dar es Salaam gati ambazo hazipo kwenye mkataba huu zinatafutiwa Mwekezaji mwingine (hata huyu wa sasa)
  • Mkataba huu hauhusishi Bandari yoyote mwambao Bahari ya Hindi wala maziwa makuu.
Sasa kwa maboresho hayo Bado wengi nimeona wamefungua Nyuzi za kuilaumu TEC na baadho ya Wananchi na ASASI nyingine za kiraia.

Naomba kuwauliza kuwa Tatizo ni MKATABA AU Tatizo ni waarabu kuwekeza?
Fuatilia kisa hiki cha mhaya na mdigo, kwa akili huru. Hii siyo hadithi bali tukio halisi na la kweli lililowahi kutokea:

Mjomba wa rafiki (mdigo) walikubaliana na jamaa mmoja mhaya, washirikiane kufanya biashara. Mdigo hakuwa ameajiriwa popote, hivyo yeye ndiye alikuwa wa kuhangaika huko na kuke. Biashara haikwenda vizuri, mtaji wote ukapotea.

Mhaya akaja juu sana, akampeleka mahakamani mdigo. Mdigo alikubali yote, kuwa pesa imepotea mikononi mwake akiwa anafanya biashara. Akaomba apewe muda wa kumlipa mhaya ndani ya miezi 4. Suala likamalizwa nje ya mahakama. Mhaya akashikilia hati ya nyumba ya mdigo aliyokuwa amepangisha eneo la Buguruni, huku wakiandikishana kuwa asipolipa ndani ya miezi hiyo 4, mhaya ataichukua nyumba.

Baada ya miezi mitatu, mhaya akamwambia mdigo kuwa amejifikiria sana, na kwa kuzingatia uhusiano mzuri wa zamani, ameamua suala liishe, waendelee na biashara, na kwamba amehakikishiwa kuna biashara nzuri ya mahindi nchini Kenya, na sasa anashughulikia mkopo, hivyo mdigo asijishughulishe tena na ulipaji fidia. Mdigo akafurahi. Baada ya miezi miwili tangu alipomtaarifu mdigo asimlipe, mhaya akaenda kwa mdigo na kumwambia ameamua kuchukua mkopo mkubwa benki wa shilingi milioni 200, sasa dhamana ya nyumba yake haitoshi, itabidi waweke dhamana na nyumva yake (mdigo) pia. Mdigo akakubali.

Kesho yake mhaya alienda kwenye nyumba anayomiliki mdigo na watu aliowatambulisha kuwa ni maafisa wa benki, mdigo akaoneshwa sehemu ya kusaini kwenye makaratasi aliyokuja nayo mhaya. Mdigo hakupoteza muda wa kusoma, akasaini.

Baada ya wiki 2, wale jamaa waliokuwa wamekuja na mhaya siku ya kusaini, wakawaambia wapangaji wa nyumva ya mdigo kuwa, wanawapa mwezi mmoja wa kukaa bure, kisha waondoke, na kwamba nyumba imeuzwa.

Mwishoni ikaja kugundulika kuwa hakukuwa na mkopo wa benki bali mdigo alisaini karatasi za kuhamisha umiliki. Na huku kulikuwa na back up ya document ya mwanzo kuwa miezi 4 ikipita bila ya mdigo kumlipa mhaya, basi nyumba itakuwa imeenda. Mdigo alienda mahakamani, lakini alishindwa kwa sababu aliahidi mwenyewe kuwa asipolipa deni ndani ya miezi 4, nyumba ichukuliwe na mhaya, na baada ya miezi 6 kupita, alisaini documents za kuhamisha umiliki.

SOMO KWETU:

HGA iliyosainiwa jana ni nzuri, lakini IGA ambayo ilikwishasainiwa awali inasema nini? IGA imefutwa? IGA imerekebishwa? Maana HGA haipo juu ya IGA bali kinyume chake. Kama IGA imebakia vile vile, tusishangae siku moja, huenda hawa waliosaini wakiwa hawapo, nchi ikaburuzwa mahakamani kwa kukiuka mkataba mama.
 
Hivi kma mkataba haukuwa na shida wamerekebisha nini? Mbona ni kawa haueleweki hoja yako? Maana mara haukuwa na shida ila waarabu...
Mkataba ulikuwa na Shida na Hoja zimerekebishwa kipi usichoelewa Ndugu yangu au umequote wrong person!
 
Hivi kma mkataba haukuwa na shida wamerekebisha nini? Mbona ni kawa haueleweki hoja yako? Maana mara haukuwa na shida ila waarabu...
Kuandika hapo ina maana kwamba Wamedhihirisha watu tatizo sio mkataba kwa sababu baada ya kurekebishwa kwa mkataba bado wanalalamika kuwa itakuwaje warabu kupewa uwekezaji watatuleta uislamu na hilo ndo tatizo la kuona kumbe tatizo halikuwa mkataba ila ni waarabu kuwekeza kuna kitu hujaelewa nikusaidie
 
Mimi niseme nilikuwa miongoni mwa waliopinga uwekezaji wa DP World. Japo sijaona hiyo mikataba ila kama yanayosemwa yamefanyiwa marekebisho basi waje wawekeze. Kwa hiyo sioni kama kuna watu wataendelea kulaumu kama waliyoyataka yamefanyiwa kazi, otherwise ni hisia tu za kwamba bado watu wanapinga DP World kuwekeza
 
Kwa hiyo wewe na akili zako tuseme za kuzaliwa tu ulidhani issue ilikuwa mkataba mbovu? Huo mkataba ulikuwa na ubovu gani hadi ukaamini?

Watanzania mnapaswa kujifunza sana kuhusu siasa za nchi yenu na ujinga wa wananchi. Na siku mkijua siasa zenu za hovyo na ujinga wenu ndo chanzo cha umaskini wenu hapo ndo mtakapogomboka.

Kiufupi hakuna shida yeyote kwenye uwekezaji wa DP World nchini Tanzania. Ni chuki, uzandiki, siasa za hovyo na ujinga tu ndo zilisababisha kelele zote zile
Usijitoe ufahamu chief. Kwenye mkataba kulikua na shida za wazi na zimerekebishwa .
 
Hahaha sikwenda mkuu niliishia darasa la pili ila nilikataa historia ya uongo ya kupandikizwa chuki hivyo nikapata historia yenye facts na ukweli wenye ushawishi..
Usionipandikiza chuki zisizo na sababu
Kama hukwenda shule hilo ni tatizo lako ndio maana mambo madogo madogo kama haya yanakushinda.
 
Mimi niseme nilikuwa miongoni mwa waliopinga uwekezaji wa DP World. Japo sijaona hiyo mikataba ila kama yanayosemwa yamefanyiwa marekebisho basi waje wawekeze. Kwa hiyo sioni kama kuna watu wataendelea kulaumu kama waliyoyataka yamefanyiwa kazi, otherwise ni hisia tu za kwamba bado watu wanapinga DP World kuwekeza
Pitia huu uzi mkuu kuna watu wanatoa Kauli za kidini kwamba Dp world ni mwislam so Hawamtaki kutokana na uislamu wake na mengine mengi ya kibaguzi
 
Kama hukwenda shule hilo ni tatizo lako ndio maana mambo madogo madogo kama haya yanakushinda.
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… Asante mkuu haya nifanyeje ili mambo madogo madogo kma haya yasinishinde 🀣🀣
 
Kwa hiyo wewe na akili zako tuseme za kuzaliwa tu ulidhani issue ilikuwa mkataba mbovu? Huo mkataba ulikuwa na ubovu gani hadi ukaamini?

Watanzania mnapaswa kujifunza sana kuhusu siasa za nchi yenu na ujinga wa wananchi. Na siku mkijua siasa zenu za hovyo na ujinga wenu ndo chanzo cha umaskini wenu hapo ndo mtakapogomboka.

Kiufupi hakuna shida yeyote kwenye uwekezaji wa DP World nchini Tanzania. Ni chuki, uzandiki, siasa za hovyo na ujinga tu ndo zilisababisha kelele zote zile
Wow!!!!
 
Back
Top Bottom