Sasa nina hakika CHADEMA haitakufa tena kwa matakwa ya binadamu

Kazi yetu kutoa rambi rambi tu
Ha ha ha haa.
Wamejaribu kumchukua Mzee Mdee na wenzake,huku nyuma akina mama wanapigana vikumbo kuchukuliwa fomu za kugombea nyadhifa mbalimbali..
Kama aliyekua Amiri Jeshi Mkuu alitolewa machozi wakati wa kampeni na kuishia kuruhusu aibu ya kimataifa ya kuyatumia majeshi kukimbia na mabox ya Kura wakati alishawaaminisha watu wake kuwa keshaua upinzani je Kuna mwingine Tena zaidi ya Amiri Jeshi Mkuu katika nchi?
Chadema ikifa Mungu kapenda.
 
Chadema imewekeza kwenye mioyo ya watu,sio kwenye majengo.
Ukitaka kulifahamu kuwepo na Tume huru ya Uchaguzi na misingi ya Demokrasia ifuatwe.
Mpango wa Mungu mwanadamu hawezi kuzuia!Unapigwa Chepe, CDM inaenderea mbere.
CCM inatetewa/inalindwa na vyombo vya dola kujihami dhidi ya CDM na ndiyo salama yao.Ukitaka kuwafahamu CCM kwenye kundi la watu tamka CDM,PEOPLES, Mbowe,Lissu ama Heche!Utawaona wanavyoweweseka.
CCM ni kinyume cha Haki?Maana kila mtetezi wa Haki ataitwa CDM.
 
Sahihi kabisa,siyo maneno ya wanasiasa uchwara
 
Aliseme Kikwete "Fikra haipigwi rungu"

Fikra za kutaka mabadiliko ya kweli haziwezi kufa hata siku moja. Kinachobadilika ni gari tu ambalo watu wanatumia kuelekea mabadiliko. Ilikuwepo NCCR, wapenda mabadiliko wakaiamini, NCCR ilivyo-prove kwamba ni gari bovu; wakashuka wakaamia CUF, nalo lilivyokuja kuonekana halifai; watu wakaamia CHADEMA. Na siku CHADEMA ikija kupoteza direction watahama pia.

Kwa ufupi, Osama amekufa, lakini ugaidi haujaisha.
 
CDM inawapa CCM na viongozi wake Stress ya kiwango cha 4G.Hawana hamu,ilibidi kutumia instruments zote kujitangazia ushindi wa kishindo kifigisu figisu.Hiyo pekee ndiyo ilikuwa salama yao vinginevyo tungeshakuwa na CCM chama kikuu cha upinzani.
Muwashukuru Watanzania kuwa mazwazwa,ingekuwa kwingineko mhhh!
 
Kwa ccm wao wanataka cdm ife hata kutajwa isitajwe.

Sasa sijui watatumia njia gani kuimaliza kama wanavyotaka wao
 
Pangechimbika
 
Kitu kilichonivutia Sana ni kampeni za 2020. Mgombea wa Chadema aliweka historia ya kutokuwa na bango hata moja, kutokutangazwa kwa mikutano yake mingi, kutokuwa na hela za kutosha za kampeni, kutokuwa na wasanii wakubwa na wengi, lakini mikutano yake ilikuwa ina hamasa ya Hali ya juu sana.
 
Kwiyoooo.
Nyumbu wa Ufipa mnaliwazana eti?
Haaaa,,,,hongera Bavichaa kwa kupumbazana.
 
Ni Tanzania pekee ambayo haiwezi kufa,

Vyamavyama hivi ni rahisi Sana kufa!!

Kwa mfono mdogo tu, Ikitokea Chadema imekufa utahama nchi??
"Temea chini ndugu" usikalili,sijui elimu yako wala umri wako,Wala upeo wako wa kujua Mambo.
Ingawa sipendi itokee na pia naogopa hata kuandika.
Unajua na ninakuhakikishia kuwa Tanzania inaweza kufa ndani ya saa moja tu.
Muungano unaweza kuvunjika wakati wowote ule na Tanzania ikawa Historia.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio unazaa Tanzania na kwa bahati mbaya muungano wetu uko very delicate.
Pia kwa kukusaidia nakupa baadhi ya nchi zilizokufa.
Ndio maana nikatilia mashaka ufahamu wako.
1.USSR
2.Yugoslavia
3.Sudan
4.chekoslovakia
Kwa uchache.
Usikalili.
 
Mbowe yuko wapi?
 
Mbona unang'aka kama nh'ungo?

Narudia tena, Ni Tanzania pekee itakayodumu, vyamavyama hivi vinamwisho wake,

Na ikitokea Chadema imekufa, Je, utajitundika??
Tanzania inaweza kufa ndugu acha kukariri maneno ya akina kibajaji.
Hujawahi kusikia nchi Fulani majimbo au mikoa inajitenga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…