Sativa alipia matangazo Instagram kuanika uchafu wa Jeshi la Polisi

Sativa alipia matangazo Instagram kuanika uchafu wa Jeshi la Polisi

Dogo kapoteza uelekeo huwezi kushindana na watu wazima Muliro jana kamprovoke dogo kama mzazi na dogo kaingia upepo vibaya mno
Wazazi jitahidini kukaa na vijana wenu muwafundishe ukakamavu namna ya kusema na kujibu watu wazima
Kwamba watu wazima wamuambie akae kimya ?

Kwamba kimya chake kitamfanya aishi milele au apone majeraha ? Huyo murilo yeye ataishi milele ?
 
Sio chadema ni maria ana kakesi kake amemfungulia IGP akishinda alipemwe tubilioni kana mvimbisha kichwa shauri yake
Dogo yuko kina kirefu cha bahari time will tell
Wakili wake amasidie dogo namna wa kujibu na kubehave makubwa mitandaoni anaharibu sana
Ana haribu nini ?
 
Mkuu,
Unazijua BTX, VX, POLONIUM 201, RICIN, BOTOX ni Jambo la muda TU.

Haki hui nua Taifa.
Mawazo yako siafikiani nayo. Kwamba binadamu tuogope kuanika maovu kwa sababu ya kuogopa kuuawa. Dunia imefika hapa ilipo kwa sababu ya watu majasiri kama Satifa. Woga hauna nafasi. Yaani mtu walipanga kuumua, akapona kimuijuza halafu eti aogope kutetea haki kwa sababu ya woga. Hvi unajua kuna wengi tu wanakufa kwa sababu ya kuogopa kama unavyotaka wewe?
 
Edgar Mwakabela maarufu kama Sativa ambaye ni muhanga wa matukio ya utekaji, leo hii amelipia matangazo ya Instagram ili kuanika uhalifu unaofanywa baadhi ya askari wa jeshi la polisi.

Haya ameyaeleza Sativa katika ukurasa wake wa Twitter (X) leo tarehe 06/10/2024, ambapo ametenga bajeti ya Tshs. 135,000/= kwa muda wa siku tano kulipia matangazo hayo.

Ifuatayo ni nukuu kutoka kwenye ukarasa wa X wa Sativa:

MULILO TIME YO SHINE.🔥
Mnalipa CHAWA 20k wanichafue.

Mimi nawalipa INSTAGRAM kuaniaka uchafu wenu.

@tanpol u messed w/ GEN Z.

Budget $50 = 135,000/= TSH.
Duration: siku 5.

@tanpol shindaneni na Technology.😁

Let's Cruise🤝

Mwisho wa kunukuu.
PoliCCM nizaidi ya magaidi.
 
Ipi bora, awe eliminated akiwa kimya au akiwa anapambana?
Huyo walishamuua, na yeye amelipokea hilo na ndiyo maana anatumia makosa waliyoyafanya ya kudhani wamemaliza kazi, hivyo muache awafichue, kupona kwake siyo jitihada za binaadam yoyote bali ni Mungu wake ametaka awafichue hivyo muacheni awafichue, mlishindwa kuifanya kazi yenu so muacheni aiganye ya kwake
Kina nyinyi endeleeni ku "MPAMBILA" sativa ataendelea kua yeye ie.anaishi na Maumivu na anatumia dawa mpaka muda huu hapa unajifanya kum support but really hujamsaidia chochote.
Walitaka kuchukua wanamchukua na itabaki history.
Ajifunze kwa kina Dr.ulimboka, kubenea, mwakyembe, Roma, kabendera na wengineo walio wai kupitia hayo mazila.

Kunguru mwoga huepusha mbawa zake mapema.
 
Aende tume ya haki za binadamu na utawala bora ili akasaidiwe kufungua shauri na watuhumiwa wake wataitwa mahakamani, mahakama ndo muhimili wa mwisho wa kuamua haki hapa Tz.

Ila akienda na upepo wa kushangiliwa mtandaoni na kuanza kumchafua kila mtu na hana ushahidi hata mmoja huenda yeye ndo akarudishwa tena gerezani maana anao wafanyia hivyo wao wanakusanya ushahidi.

Kama ilivyokawaida ya wa Tz wanaokushangilia mtandaoni siku ukibananishwa hakuna hata mmoja anaeweza kutoa mguu wake kuandamana barabarani kwaajili yako
 
Kina nyinyi endeleeni ku "MPAMBILA" sativa ataendelea kua yeye ie.anaishi na Maumivu na anatumia dawa mpaka muda huu hapa unajifanya kum support but really hujamsaidia chochote.
Walitaka kuchukua wanamchukua na itabaki history.
Ajifunze kwa kina Dr.ulimboka, kubenea, mwakyembe, Roma, kabendera na wengineo walio wai kupitia hayo mazila.

Kunguru mwoga huepusha mbawa zake mapema.
Wewe ulimsaidia nini? Kama kuna sheria anaivunja ningekuelewa, ila kwa kuwa hakuna sheria anaivunja basi usimfundishe jinsi ya kulia kwa maumivu waliyomsabanishia.
Uoga wa hao akina Mwakyembe, Ulimboka umelisaidia nini taifa?
 
Kwani sasa hivi hajaumia ?
Mfano sisi wengine ambao tumepata body fracture kwa ajari still tunaishi na Maumivu na dawa.

Huwezi kunishaur kuhusu Maumivu najua vizuri yanafananaje unameza madawa makali ya Maumivu na Maumivu yanabaki pale pale.

NB
Sifundishi watu kua manyumbu au kutoku kudai haki zao ama kuwavika uoga lazima tujue kuzichanga karata zetu vyema na kufanya measurements and evaluation kwenye mambo yetu tunayo panga kuyafanya binafsi naona wazi mbinu anayo tumia sativa haito mpa matokeo chanya.
 
Ukiogopa utakufa usipoogopa utakufa kwa sababu Kufa ni lazima lakini kuwa muoga au jasiri ni hiari yako unapochagua kuwa muoga usiwatishie kifo waliochagua kuwa majasiri kwa sababu nyote meeting point yenu isiyo na option ni KIFO

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom