Pre GE2025 SATIVA: Mbeya Mjini Haina Faida kuwa na Mbunge Ambaye ni Spika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Eti Spika wa mabunge, kumbe ni hovyo kabisa
hakuna spana hapo ujinga mtupu

kwamba kwa kuwa mbeya wamebahatika kupata spika basi maendeleo yote yaelekezwe huko tu

sisi ambao hatuna viongozi wa ngazi za juu kwamba ndo hatustahili maendeleo

wote tupewe maendeleo bila kuangalia huyu katoa kiongozi huyu hapana
 
Umewahi kusikia hata siku moja anatetea wananchi?
 
Mbona kama Sativa anajipa Sana umuhimu wenye Hana

 
Mbona kwa Pinda kuna uwanja wa ndege wa kimataifa,kwa Philip Mpango mambo yamepamba moto,kwa Mwigulu Nchemba ndio usiseme kabisa Tanzania imehamia pale,Chato kwa marehemu kuna ikulu na uwanja wa ndege wa kimataifa.Wewe acha kujifariji kwa siasa mfu zisizo na tija.
 
M
Mbeya ndo mkoa wenye miundombinu mibovu kabisa ya Barabara. Alichofanikiwa Tulia nikuanzisha mikopo ya kausha damu akijinufaisha na umasskini na uhitaji wa wakazi wa mbeya. Tulitegemea kuwepo huko bungeni kama msikamizi wa moja ya mihimili kungesaidia lakini wapi
 
Huyo mtekwa Sina hakika kama akili imekaa sawa ila ilitakiwa kabla ya Kulaumu Tulia mwenye miaka 5 Kama. Mbunge wa Mbeya Mjini angeonesha walichofanya Sugu na Chadema Kwa miaka 10..

Barabara za Tulia hizi hapa zinaendelea na ujenzi πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://www.instagram.com/reel/DA2bxrMNBRK/?igsh=MThiZ2psOTBweGJ5MA==
 
Mbeya naona kuna gen-z wengi saana akina pididi hawapo huko.2025 patachangamka sana pataeleweka ila Arusha naona kama imetekwa na wasiojulikana.
 
uwanja wa ndege katavi haikuwa sababu ya pinda mkuu, ingekuwa hivyo angetandaza barabara za lami mji mzima cha ajabu hadi anaondoka madarakani hakuna barabara za maana zilizo jengwa ni vumbi tupu

uwanja wa ndege wa kimataifa mkuu umedata ndo uwanja wa ndege wa kimataifa unakuwaga vile ama ujawahi hata kufika
 
Sativa ana hoja. Wapambe wa Tulia wamekuwa wakitumia nafasi yake ya USPIKA wa Bunge na Urais wa Bunge la Dunia kama sababu ya kuwashawishi watu kuwa ni mtu wa maana kuwa mbunge wa Mbeya Mjini.

Kama angekuwa mtu wa maana mwenye uwezo basi leo Mbeya ingekuwa na barabara nzuri na miradi ya maendeleo.

Kwa hiyo Mbeya haihitaji mbunge ambaye ni Spika kuwa mwakilishi wao.
 
Mbona kama Sativa anajipa Sana umuhimu wenye Hana
Sativa amepiga palepale. Huyu kigagula hatoboi 2025. Uspika wake hausaidii chochote kwa maendeleo ya Mbeya.

Tunahitaji Spika atakaye pigania haki za wana Mbeya Bungeni
 
Kwa taarifa yako hizo kilometre 22 za barabara toka Uyole hadi Songwe, hakuna kinachoendelea kwa zaidi ya miezi 10 sasa
Una uhakika au unaropoka tuu? Harafu nani kukwambia ni km 22?

Mwisho kwani hujui kwamba Kuna km zingine 15 za Tactic,stendi na soko?

Mwambie Sugu aoneshe miaka 10 alijenga kipi? Naona unakuwa mjinga
 
Mbona kama Sativa anajipa Sana umuhimu wenye Hana
TULIA hakubaliki kabisa na wapiga kura wa kawaida ukiacha wapambe wake wachache huko Iduda, Itezi, Igawilo Uyole ambako ndiko wajinga wamejaa. Kama utashindanisha hawa wachovu 2 kati ya Sugu na Tulia nakuhakikishia Sugu ataibuka kidedea
 
Una uhakika au unaropoka tuu? Harafu nani kukwambia ni km 22?

Mwisho kwani hujui kwamba Kuna km zingine 15 za Tactic,stendi na soko?

Mwambie Sugu aoneshe miaka 10 alijenga kipi? Naona unakuwa mjinga
Haijalishi ni kilometres ngapi? Ila kimsingi Mbeya mumetapeliwa tu. Maana Mkandarasi alichofanya ni kupitisha grader toka Uyole hadi Songwe na kutimua vumbi tu. Hakuna kazi inayoendelea, hiyo ndiyo hoja kuu unayopaswa kuijibu achana na urefu wa barabara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…