Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Clip tu kuingalia inasikitisha but lijitu linaacha kumpeleka hospitali linamuuliza maswali ya ki wack
 
Wakuu Salama,

Sativa amekuwa akitafutwa toka weekend (Jumapili - 23/6/2024), baada ya ndugu zake kumtafuta bila mafanikio.

Watetezi wa haki za binadamu wamepiga kelele kuhusu hili hata mmojawapo wa viongozi wa ACT Wazalendo Rahma Mwita alizungumza suala hili kwenye kwenye XSpaces jana 26/6/2024 kuwa yupo tayari kujiyolea muda wake kuambatana na ndugu wa kijana huyo kwenda kwenye vyombo vya habari na asasi mbalimbali za kiraia kupaza sauti kuhusu kupotea kwa kijana huyu.

Edgar anaishi Kimara kwa Msuguli na amepatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.


Kama kelele zisingepigwa huyu ndio ilikuwa ntolee, halafu kuna chawa wanaotetea ujinga kila siku.

Aisee, wakati wa kubadilika ni sasa, mtu akipotea wote tupige kelele, serikali ikienda kushoto wote tupige kelele. Isiwe kazi ya wanaharakati wachache au watetezi wa haki za binadamu, peke yao hawawezi. Tukiungana wote tunakuwa na nguvu.

Tuendeleze hashtag Wakuu, #KataaMachawa #KataaUozo2025, amsha kila utakayeweza kumuasha, tushikamane na kuteteana wakati wote kuleta uwajibikaji nchini.

HAWA WANYAKYUSA HUWA NI WAKAIDI WAMESHINDWA KABISA UCHAWA WAPUUZI HAWA. MNASHINDWA KUJIPENDEKEZA MUENDELEZE MKOA WENU?????????????????KWA NINI HILI KABILA WABISHI SANA?
 
Hapo wanapanga kumpelekw police kwanza kabla ya kumfikisha hospitali!
Unbelievable.
Hospitali zetu unaweza kumfikisha wakakataa kumtibu mpaka awe na PF3


Kuna jamaa yetu alishavamiwa akachomwa na visu tumekimbia police haraka kupitia pf3 hapo tumepanic balaa akatoka askari ile tunamwambia tuandike haraka jamaa linajibu "huyo mbona bado mpya, hata hajapigwa sana, Kuna watu wanaletwa hapa wamechakaa" 😃
 
Shughuli kuu ya vyombo vya habari duniani kusema mazuri ya Serikali.Ikikosoa tu kesho leseni haipo
 
Back
Top Bottom