Saudi Arabia, UAE, Iran, Egypt, Ethiopia na Argentina zakubaliwa kujiunga BRICS

Nilimaanisha kwenye biashara ya mafuta kama vile ambavyo sasa hivi Russia na China; Russia na India wanatumia sarafu zao..
Kuna mambo mengi sana yanaoifanya dollar ya Marekani kutumika kama sarafu ya kimataifa, mojawapo muhimu ni soko huru la fedha na mitaji la Marekani lisiloingiliwa na serikali. Hizo sarafu nyingine kama za China, Urusi na Saudia serikali ina mikono mirefu sana kuzifanyia devaluation na revaluation.

Sababu nyingine kubwa ni udhibiti wa fedha na mitaji. Kuna sheria na vikwazo vingi sana kutoa au kuingiza viwango vikubwa vya Yuan halali huko China kwa sababu serikali ina mkono wa moja kwa moja katika masoko ya fedha na mitaji.
 
Kama BRICS wataendelea na juhudi zao kwa kasi hii, halafu US iamue kubweteka, yaani isifanye chochote kile, narudia tena, yaani isifanye chochote kile, basi, by 2050 Dollar itakua imeshaanguka.

Ila bahati mbaya au nzuri tayri kinyume na matarajio yap wengi, by just this 2023, tayari US imebadili the Major trading partner na sasa Mexico ndiye Major trading partner nafasi ambayo ilikua ikishikiliwa na China.

Wakati huohuo, kasi ya matumizi ya nishati mbadala wa mafuta ikizidi kukua kwa kasi kote duniani.
 
Unajua kuwa kiwango cha reserve ya US Dollars katika foreign currency reserves za mataifa mbalimbali duniani kinapungua

Unafikiri sababu ni nini?
 
Kumbe mpaka USA waamue kubweteka... Unadhani watabweteka? Unadhani hawana watu wenye uwezo wakuangalia future ya dollar yao?
 
Haijabadili ni vile China hawaku-import bidhaa nyingi kutoka Marekani kama Mexico
 
Haya mataifa yote 6 waitagemea US kwa kila kitu uchumi wao
 
Haijabadili ni vile China hawaku-import bidhaa nyingi kutoka Marekani kama Mexico
Kukukumbusha tu, tangu enzi za Trump, US ilishaanza kuhamisha viwanda vyake from China to Mexico na India na akapunguza vipao mbele vyake vingi kwa China.
Hiyo BRICS inaendelea sasa kwa kuwa ilisshaanza, ola imeanza kupata mwitikio wakati China kaanza kutikiswa, ndani ya miaka miwili hadi mitano Ijayo, US atakua ameshamtengeneza India kiwa mbadala wa China huku mataifa yanayozalisha mafuta nayo yakianza kupigania pumzi zao baada ya mahitaji ya bidhaa zao kupungua kwenye mbalimbali duniani.
Huu mchezo huchezwa na Werevu
 
Naamini bricks hawadhani hivyo. Ila wanachama wake wakwamtogole, kwatumbo, kwampalange, kwamama kibonge ndio wanaodhani USA ametulia tu anasubiri dollar yake iporomoke
BRICS hawana mpango wa kuishusha dollar ya Marekani. Taifa lolote linaweza kuwa mwanachama wa BRICS hata Marekani. Hiyo ni economic cooperation
 
Unajua kuwa kiwango cha reserve ya US Dollars katika foreign currency reserves za mataifa mbalimbali duniani kinapungua

Unafikiri sababu ni nini?
Kinapungua kwa kiwango gani na ukilinganisha na sarafu zipi??

US Dollars katika foreign currency reserves zinazohifadhuwa na nchi mbalimbali duniani ni takribani 60% kwa sasa, inafuatiwa na Euro 20%, Yen ya Japan 6%, Paundi ya UK 5%, Yuan ya Mchina ni 3%
 
Sasa mbona bado Marekani ni importer mkubwa wa bidhaa za China? Katika trade partners wakubwa wa China, Marekani ndiye kinara.
 
Ikitokea US naye akaomba kujiunga inabidi naye wamkubalie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…