Tetesi: Saudi Arabia yapewa haki ya umiliki na uendeshaji wa bandari ya Bagamoyo kama sehemu ya mradi wa East Gate

Hawa wanajenga, wazungu wanakomba mali yote migodini wanatuwschia mashimo na wajivuni wanachekelea tu.

Ushari ni kwamba bila kujali mwekezaji katoka wapi kuwe na uwazi kwenye mikataba ya kitaifa. Magufuli aliweka mikataba ya madini wazi. Utekelezaji hatujui lakini Mama yetu ni msiri msiri bila sababu. Ingawa huu uwekezaji tumegundua sio wa kweli ni vizuri kuongeza uwazi. Watu wana lalamikia uwazi sio nani kapewa.
 
Hebu nitajie mkataba mmoja wapo ambao Magufuli aliweka wazi!!
 
Nitajie mkataba mmja tuu ambao wewe unaujua uliwekwa wazi awamu ya Magufuli
 
Kwani Loliondo kimeuzwa? Si Kuna waliojenga mahoteli na waliochukua leseni za uwandaji au?

Kiasi gani mnapata nenda mamlaka husika ya Ngorongoro watakupa hesabu.
Huwa nasikiliza sana bunge letu na Huwa naona hesabu kutoka taasisi mbali mbali lakini za hapo nilipo sijawahi sikia Mkuu ndo maana nimeuliza ili kupata ufahamu tu!
 
Hiyo tarehe ya barua February 25 imefika lini na leo ni 14th February, mbona wanatuchanganya na kutuvuruga? Inaonekana kuna uchafu mwingi unafanywa serikalini hivi sasa
 
Hili limekaaje wandugu. Huku nchini hatujaambiwa ila huko Saudia wanasherehekea kupewa bandari yetu ya Bagamoyo. Ni ile wanaita concession. Yale ya Dubai kupewa bandari zetu zote ilibidi ushirikiano na speaker ili kupitisha sheria iliyoonekana baadae kuvunja sheria nyingine hivyo tunatumaini ikawa 'non and void'. Sasa hawa Saudia concession yao wenye kujua watujuze na pia kwa nini humu nchini kuna ukimya.
Samia kwa hakika anauza nchi yetu na ndio maana hataki kusikia jina la Magufuli likitajwa kwa vile sera zake za kizalendo alikua hazipendi.
Wabara tufungue macho. Tumeona mama akiorodheshwa kama rais wa saba Afrika kwa utajiri. Hiyo taarifa inaweza ikawa ya uhakika. Tumeona pia mama akipora kwa hila ugombeaji urais kinyume na katiba ya chama chake cha ccm. Nchi inauziwa waarabu na wahindi jamani tulitambue hilo.
 





kuna mipango ni kwamba tu wametoa mapema habari
 
Swali, je tunaruhusiwa kula nguruwe zetu bila masharti?
 
Waarabu ni wajomba zetu.

Muda si muda tutawapa tena uwanja wa ndege wa DSM-JNIA.

Pia tuko na mazungumzo na wajomba wetu wa Oman tuwape moja kwa moja SGR yetu... maana Kidogosana anaelekea amechemka
Kila kitu omani sasa mna wajomba wapya mungu amipe kheri na baraka
Sasa basi haina haja kusema omani omani
 
Kweli Mjomba Ana heshims yake lakini mmetusema saana hata wajomba wakahuzunika tunawaombea kheri na baraka
Subiri mwezi ujao uone baraka za wajomba: watashusha land cruiser LC 300 kwa kila kiongozi wa ccm kuanzia wilaya hadi taifa.
 
Wenyewe saudia wanadai washapewa bandari. Vigogo nchini tunawatahadharisha kuacha ubabaishaji. Tunajua uroho wao na kukosa uzalendo mbele ya ushawishi wa kifisadi. Huku duniani waafrika hatuna wajomba. Ikiwa viongozi wetu watakosa uzalendo na kutuuza utumwa kama machifu wetu enzi za kale kwa kukosa maarifa haitawezekana maana watalipa. Tutahakikisha wanawajibika hapahapa duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…